Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa akiteta jambo na Mwenyekiti wa chama hicho Mh. Freeman Mbowe (shoto) na Zitto Kabwe kwsenye moja ya mikutano yao ya hadhara

BAADA ya kutafakari na kujaribu kushawishi watu mbalimbali, hatimaye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilikutana kutafuta wa kukibebea bendera katika kinyang’anyiro cha urais.

Hata hivyo, jina la Katibu Mkuu wake Dk. Wilbroad Slaa, ndilo pekee ambalo hadi jana lilikuwa linatajwa kuombwa rasmi na Chama hicho ili abebe bendera hiyo.

Kamati Kuu ya Chadema ilikuwa na kikao ambacho pamoja na ajenda zingine, moja ya ajenda hizo, ilikuwa ni kuteua jina la mgombea urais ambaye atachuana na wagombea wa CUF, CCM na TLP.

“Ninachoweza kukwambia ni kwamba Kamati Kuu imemwomba Dk. Slaa awe mgombea urais wa Chadema na amekubali,” alisema mpasha habari wetu ambaye anahudhuria vikao vya chama hicho vinavyofanyika katika hoteli moja ya Dar es Salaam


Kwa habari kamili tembelea HabariLeo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2010

    Ushauri wa bure kutoka kwa mwananchi (sio CCM). Kama viongozi wa upinzani wanataka madaraka au heshima lazima wajionyeshe kama ni viongozi wenye heshima kuanzia na mavazi kwanza. Timieni PR wazuri ili picha zenu zipendeze. Jaribuni kuwasoma wenzenu. Hapa mnaonekana kama mmechoka sana na sio viongozi wa kupewa nchi pamoja na elimu yenu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2010

    Nimeifurahia sana habari hii.. Lakini hata hivyo inanisikitisha kuuona mwisho wa jasiri wetu huyu bungeni .... Tafakari makini inatakiwa juu ya uamuzi huu mzuri - yawezekana huu si wakati mwafaka...Nawasilisha Naomba maono yenu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2010

    Ok ... Lakini kwanini tusipambane kwa nguvu zetu hizi ndogo dhidi yao ila zenye kutosha kutujaza kwa wingi zaidi bungeni - kwa wakati huu kwanza??? huko tutawatikisa sana na hayumkini watasalimu amri 2015!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2010

    Dr.SLAH ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kuongoza nchi.Ni mzalendo wa kweli na ni mtu makini sana.
    HOFU YANGU;CCM na mafisadi wake hawatakuwa tayari kuona mtu huyu akiingia ikulu kwani kitakuwa kiama kwa waliowahi kuibia nchi hii.
    Huenda tukapoteza mtu makini sana bungeni.Dr.SLAH ni mbunge wa nchi nzima.
    Mungu mbariki dr Slah.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2010

    Nilikuwa sijaamua kupiga kura Oktoba hadi leo asubuhi nilipopata habari za Dr. Slaa. Kwangu mimi huu ni ushindi wa demokrasia. Nina imani tukijipanga vizuri na kuwaelewesha watz atashinda, la asiposhinda upinzani utakuwa umepata nguvu. Tuna viongozi wasomi wengi, wenye kipaji cha uongozi wengi, lakini hatuna wazalendo, watu wenye uchungu na hii nchi, waadilifu, wasio waoga, wanaothubutu kujitolea kwa ajili ya nchi na watz maskini. Lakini Dr. Slaa ingawa sio perfect ana nyingi za sifa hizi nzuri na anawazidi wenzake kwa asilimia nyingi. I will vote 4 him.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2010

    sasa mnataka kuleta masihara hakuna chochote cha zaidi hapo, ndio maana tunasema ccm ipo kila mahari sasa wanataka kumuondoa kinamna Dk Slaa bungeni maana kwa nguvu waliyonayo ccm muda huu kuangusha serikali yao ni kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano wacheni mzaha tunamtaka Slaa Dodoma tamaa zenu wekeni pembeni,kama Chadema ipo imara yoyote anaweza simama mkianza chagua basi hamuwezi..DK SLAA FOR PM NOT PRESIDENT

    ReplyDelete
  7. Dr Slaa ni mzalendo na mpiganaji wa kweli. Taifa letu linahitaji watu kama akina Dr Slaa ili tuweze tokomeza ufisadi na umasikini.

    ReplyDelete
  8. anony 7:38 - hakuna mtu asiyejua uwezo wa kina slaa na wenzake hawauzi sura bali sera.
    Slaa huraah! ila tutammiss sana bungeni nani atakuwa mpiganaji wa chdema jimbo la karatu??

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2010

    ANON WA KWANZA KABISA,BADO UNAANGALIA SURA NA MUONEKANO KUCHAGUA KIONGOZI WAKO?POLE NDUGU.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 21, 2010

    we anyny wa kwanza acha ushamba kwani wako uchi? mbona CCM wakivaa magwanda yao ya kijani husemi? mi napenda mtu asiye na makuu ninayeweza kujifananisha nae hata kimazi! na kwa mavazi yao hao wakuu ni Watanzania wengi huvaa hivyo!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 21, 2010

    tunakosa tena mtu muhimu kwenye bunge letu mbowe acha kumchuuza huyo mzee unajua hawezi pata wewe mwenyewe umeona huwezi pata uraisi umeamua kwenda kugombania ubunge mwenzako aache ubunge akagombanie uraisi sindio unataka kumtoa kisiasa mwanzako?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 21, 2010

    Faida ya kugombea ni kwamba chama kitakuwa na nguvu hivyo kukiwezesha kupata wabunge wengi zaidi wa upinzani. Hasara ni kwamba Slaa hatakuwa Raisi wala Mbunge. Tunamuhitaji Slaa Bungeni pamoja na wabunge wengi zaidi wa Upinzani. Hata hivyo naona wanachelewa sana, maana maandalizi ya mahasimu wao yameanza mapema na yako juu kwelikweli!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 21, 2010

    GO !! GO !! Dr. Slaa. GO!!
    Tupo pamoja nawe!

    ITS OUR TIME TZ, ITS OUR TIME 4 REVOLUTION !!

    Tusiwe waoga wa maamuzi, kwanini nnchi waweze sisi tushindwe??

    Sasa ni wakati wa mabadiliko..mwisho wa mafisadi.

    Let me tell u something, its only ur "single vote" can change everything.ni hiyo tu itaondoa mafisadi...just a VOTE!!

    HONGERA DR.SLAA, HONGERA CHADEMA!! TUPO PAMOJA !!

    ReplyDelete
  14. Hivi watu wanadhani Urais ni URAHISI tu, kila mtu awe RAHISI! Dr. Slaa amechemsha bora angebaki kutetea wanyonge bungeni lakini sasa ameshaingiwa na tamaa ya kutaka kwenda kunufaisha familia yake Ikulu ambazo ni ndoto za mchana.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 21, 2010

    MIMI SI MCHANGIAJI WA HOJA KWA HILI DR SLAA AU CHADEMA MMECHEMSHA,NINA UHAKIKA 99%UBUNGE WAKO UTAUTETEA VIZURI,KAMA MBOWE AMEKUPISA ILI AGOMBEE YEYE UBUNGE ANAJUA WAZI KATU HUWEZI KUKWAA URAISI HIVYO UTAMTUMIA YEYE KUWASILISHA HOJA ZAKO NA HAPO NDIO UTAKUWA MWISHO WA UMAARUFU WAKO KWA WANANCHI NA NDIO MWANZO WA MBOWE KUJIPATIA UMAARUFU WA KISIASA AMBAO HANA.TAZAMA NAIBU WAKO ZITO ALIVYOMALIZWA MPAKA AKAWA HANA UHAKIKA AKAGOMBEE WAPI.TATIZO LA VYAMA VYETU VYA UPINZANI VIMEKAA KISANII MNO NA NDANI YA VYAMA VYENYEWE HAKUNA DEMOKRASI.MIMI BADO NASHAWISHIKA UPINZANI WA KWELI UTATOKA NDANI YA CCM 2115.CHANGE YOUR MIND MY FRIEND SLAA RUDI JIMBONI UGOMBEE UBUNGE,TUONGEZE NGUVU YA UPINZANI BUNGENI PLS'E.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 21, 2010

    Dr Slaa, you run, i vote, we win. GO GO GO GO Dr

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 21, 2010

    H.MAULID unaonyesha ni jinsi gani ulivyo na mawazo mfu, na taifa lililojaa watu wa aina yako lazima liwe masikini milele

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 21, 2010

    hii ni moja ya mistake kubwa sana chadema kufanya,karatu inarudi ccm,na moshi mjini pia ndesamburo ameshasarenda maana ccm wamevunja makundi yao.sasa jimbo mlokuwa na uhakika nalo chadema ni kigoma na tarime,hizi wapinzani mmelogwa,huwezi kumtoa dr slaa kwenye ubunge umpeleke akagombanie urais,wapinzani mmeweka watu wawili wenye ushawishi mkubw kwenye siasa za tz,pro lipumba na slaa,matokeo yake ni kugawana asilimia kumi kila mmoja na kumuachia kikwete zaidi ya asilimia 70.kipindi hiki mngekitumia kujaza wabunge sio kufikiria ruzuku

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 21, 2010

    karatu hiyo kwa ccm.chadema mmechemsha,

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 21, 2010

    Wapinzani Tanzania Kwa Ukweli Wanawachosha Wanachama wao. Naona kuwa wanatakiwa Kugombea Ubunge kuwa wengi bungeni ili kuweza kuwatetea wananchi wao si Uais. Urais Tanzania CCM lakini Ubunge kuna Chance ya kupata. Lazima wawe wabunge wa upinzani kama 45% hapo kuna chance ya Uraisi lakini si muda huu kwa hivyo lazima waweke nguvu zao zote kugombea ubunge ili waweze kujinadi zaidi kwa wananchi wa Tanzania nzima. Fikiri kama Uongozi wote wa upinzani ufike bungeni serikari tawara watakuwa macho sana kwani Upinzani utakuwa mkubwa sana kwa nchi yetu wataacha kulala na kula ovyo ovyo. Lipumba ni mtu mwingine ambaye anaitaji kuwa pia mbunge bungenikuweza kuuliza serikari yetu wapi wanatupeleka. Visiwani ni sawa si Bara wapinzani wote wanaitaji kuweka nguvu bungeni.

    ReplyDelete
  21. H. Maulid urais ni kupendwa na kukubalika na watu, pia ni sifa/uwezo wa mgombea katika elimu,uzalendo wa kuipenda nchi, kuchukia rushwa na ufisadi, kuwa na vision ya kuinua nchi kiuchumi,kielimu,jamii na WITO. sifa ambazo SLAA anazo nakuzidi. CCM have the money and power but lack the most important traits that's why they don't qualify

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 21, 2010

    Sikuwa nafikiriakupiga kura, baadaya hii taarifa natangaza nia yakumchagua raisi wangu ambaye ni dk Slaa, hata kama kura hazitatosha, lakini sitajutia maamuzi yangu

    Hondohondo

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 21, 2010

    TO BE HONEST, SIMUUNGI MKONO DR. SLAA KUGOMBEA URAIS. NAWASHAURI WAONGEZE NGUVU ZAIDI BUNGENI THEN BY 2015 NGOME ITAKUWA IMARA SANA KUIANGUSHA CCM, BT FOR NOW MAFISADI WAMESHAJIPANGA KURUDI KWA NGUVU SO CHA MUHIMU NI UPINZANI PIA KUJIPANGA KUPAMBANA NAO KWA KUWA NA SAUTI KUBWA BUNGENI. DR. SLAA, PLZ TUNAKUOMBA USIACHIE JIMBO LAKO LA KARATU, TUNAKUHITAJI BUNGENI TENA.
    MWANACHADEMA DAM DAM!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 21, 2010

    Hongera Dr.Slaa kwa kuteuliwa na chama chako kugombea upresident.Wadau eleweni ya kwamba hata kama akishindwa uraisi Dr.Slaa bado anaweza teuliwa na chama chake kurudi bungeni kwa kupitia nafasi ambazo chama kina pewa.Maana yangu ni hii ninaimani ya kwamba atarudi bungeni kwa mtindo huo.Hata hivyo namuombea ashinde urais!!!!!!!!!long live Dr.Slaa.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 22, 2010

    CCM ina fedha za wananchi kutumia wanavyotaka kupata ubunge na kiti cha Raisi.

    Vyama vya upinzani havina fedha wala nguvu kupata kura za wananchi. Upinzani Tanzania na hata bara la Afrika hatuna bado. Angalia Kenya, Uganda, Rwanda, Angola, Burundi, Zimbabwe mbali za nchi za magharibi yetu. Nchi ikishikiliwa na chama basi ujue sio rahisi kung'atuka Afrika.

    Hatuna historia ya demokrasia na CCM itakuja madarakani tena. Nina uhakika kama vile nina uhakika kesho jua litatoka. Alipokufa Omar Bongo, nilisema kuwa mtoto wake atachukua madaraka kuficha pesa za wizi za baba yake, na akachukua Uraisi kirahisi.

    CCM ni chama cha nguvu kifedha na kimawazo. Kitatutawala miaka 50 ijayo pia.

    ReplyDelete
  26. Wamechemsha vibaya tena wamefulia, huyu Slaa amehongwa na Mbowe. Mbowe ana akili sana, ameshapiga mahesabu ya kutaka aje kufunika Bunge sasa anajua na Slaa akiwemo Bungeni atakwama bora amtose kichwa kichwa na jamaa kauvaa mkenge Dr. mzima!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 22, 2010

    Watanzania wenzangu nawashangaa sana. Kwanza tuwape moyo hawa Watanganyika wachache wanaojitolea kuanzisha upinzani, japo wanapata shida sana. Kwa nguvu wanazotumia CCM na washirika wao ikiwa ni pamoja na mafisadi, ni ngumu kupenyeza... na ni vigumu pia upinzani kukua. Lakini bila watu kama Dr. Slaa lini upinzani utakuwa.. Wito kwa vijana na wazee wa makamo. Tuwapigie kura wapinzani hawa kwa nguvu zote. Ofcourse Kikwete atapita yamkini kwa kura chache. Then 2015 upinzania huooooooo...... Muhimu ili Tanganyika hii na Zanzibar ipige hatua kimaendeleo tunahitaji upinzani uwepo ndani ya serikali tawala.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 25, 2010

    Anonymous wa kwanza hufai kuchangia chochote katika harakati za kulikomboa taifa letu.Ungefaa zaidi kuhukumu mashindano ya warembo na mavazi.Mawazo ya kimaendeleo huna ndugu!Tulia pembeni acha wenye uchungu na nchi wafanye kazi yao.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 26, 2010

    Ndugu Maulid ukue kifikra. Kwani Dr.Slaa muda wote huu aliokuwa bungeni amekuwa akiinufaisha familia yake? Mbona wote (isipokuwa wewe) tumeshuhudia kazi njema aliyoifanya bungeni. Funguka kifikra na kiakili ndugu. Uone mambo objectively na siyo subjectively. Wenye akili na wenye matashi mema na taifa letu wanajua Slaa anafaa kuwa rais wa taifa hili linalohitaji ukombozi. Na atakuwa rais! Ndugu Slaa songa mbele,wanaharakati wa kuiokomboa Tanzania songeni mbele. Wajinga kama akina Maulidi waachani waendelee kulala katika uvivu wa mawazo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...