Trupu zima la FFU wa Ughaibuni The Ngoma Africa Band

Kikosi kizima cha FFU wa Ngoma Africa Band kinatarajiwa kutua kwa nguvu zote katika maonyesho ya Afrika & karibik yatakayofanyika jumamosi 7-08-2010 katika viwanja vya Robestock Park,mjini Frankfurt,Ujerumani. Maelfu ya washabiki wa mziki wanaisubiri kwa hamu bendi hiyo maarufu barani ulaya kwa kuwapandisha mzuka! washabiki na mdundo wao maarufu kama "Bongo Dansi". Baada ya onyesho hilo ! Kamanda wa kikosi hiko Ras Makunja ataliongoza karandinga la FFU.

Katika onyesho lingine kubwa la wazi Music Festival,litakalo fanyika mjini Kaiserlautern, Ujerumani siku ya Jumapili 8-08-2010 ambako washabiki washajiweka tayari tayari kwa kwenda mchaka mchaka na mdundo wa Ngoma Africa band. FFU wa "Ngoma Africa Band" sasa wanatamba na singo CD mpya "Jakaya Kikwete 2010" CD ambayo inasemekana imeshaweka wingu nchini Tanzania na wakati wowote inaweza kutingisha anga za mziki za Afrika mashariki na popote pale !
CD ambayo ukisikiliza utapata vitu vyote kuanzia mziki mkubwa,ujumbe ambao utakupa majibu ya maswali mengi unayojiuliza moyoni mwako!
Jipe Raha at www.myspace.com/thengomaafrica

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2010

    Ndio Kaka yangu nakuona

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2010

    mkuu kamanda naona virungu vinanukia huko frankfurt,najua hapalaliki....unaponiacha hoi unapomaliza kazi lazima utokee mlango wa nyuma sijui kwa nini?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2010

    vichaa kazi yenu inakubalika kimataifa kazeni buti

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...