Makao Makuu ya TTCL jijini Dar
Kwi kwi ya mtandao iliyokuwa inawakabili watumiaji wengi hapa nchini tangu siku ya Jumatatu imemalizika.

Kwi kwi hiyo ilisababishwa na kuharibika kwa kifaa kwenye kebo ya SEACOM inayopita chini ya bahari huko karibu na pwani ya Djibouti.

Wahusika wamefanikiwa kurejesha huduma kwa kupitia kebo tofauti kwa muda mpaka hapo kebo ya SEACOM itakaporejea hewani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2010

    Habari njema, ila wateja wenu tunaomba mtufidie kwa muda tuliolazimika kukaa bila internet.

    Msijitetee kwamba sio kosa lenu, ila ni kosa la SEACOM. Bali na nyinyi waambieni SEACOM wawafidie.

    Fidia mojawapo inaweza kuwa punguzo la bei kwa malipo ya mwezi wa August. Punguzo liwe equivalent na bei ya siku 5 tulizokuwa offline.

    Asante.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2010

    Naomba ieleweke kuwa siku hizi intaneti ni sawa na uji na mgonjwa na ni vema wahusika wakaweka tahadhari makini ili iwepo njia kamili ya dharura nyakati zote kwa kuwa samahani haifuti madhara yaliyojitokeza.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2010

    MDAU WA KWANZA HAPO JUU UMESEMA VYEMA KABISA.KWA HAPA USA NDIVYO ILIVYO JAPO UNAHITAJIKA UIPIGIE SIMU KAMPUNI HUSIKA ILI KUPATA CREDIT KWA SIKU ULIZOKOSA HUDUMA KAMA INTERNET,SIMU,TV ETC.USIPOPIGA SIMU HUPATI KWANI UMESHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WAKO.
    MDAU WA USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...