Babu yake na Happiness Watimanywa mzee Shem Kalenga, mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Tabora Jazz, akimpongeza mjukuu wake katika hafla ya kumpongeza iliyofanyika kwenye hoteli ya Lamada.
Mtoto Happiness wa pili kushoto akiwa katika picha na wazazi wake na wadogo zake katika sherehe ya kumpongeza iliyofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya Lamada.

Mkurugenzi wa ukaguzi wa shule za sekondari nchini na kaima kamishna Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Mama Wasena akitoa hotuba ya kumpongeza mtoto Happiness Watimanywa kwa kufanya vizuri katika mitihani yake ambapo mtoto huyo ameongoza katika shule 150 duniani za mtandao wa IGCSE. Happiness alikuwa akisoma katika shule ya Saint Constantines International School ya Arusha.

Kaimu Kamishna Mama Wasena amempongeza mtoto huyo na kumpa sifa nyingi lakini pia amesifu kwa kuwa ameiletea sifa Tanzania na Wizara ya Elimu kwa ujumla jambo ambalo lilithibitishwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Mwatumu Mahiza ambaye alimpongeza mtoto huyo wakati alipokuwa kiwasilisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka huu wa fedha. Picha na John Bukuku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2010

    Kwanza kabisa nampongeza sana tena sana mtoto Happiness kwa mafanikio makubwa aliyopata.

    Pili wizara ya elimu tanzania hamna haki ya kujisifia mafanikio ya mtoto huyu kwani sio matunda ya shule za serikali. Mafanikio yake yametokana na jitihada za wazazi wake kuweza kumlipia kusoma shule ya kimataifa pamoja na jitihada zake mwenyewe.

    Sioni ni kwa vipi wizara ya elimu inataka kuvaa kofia hapa na kutaka kujipatia sifa.

    Hebu tuelezeni basi ni kivipi wizara ya elimu inastahiki kusifiwa hapa?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2010

    BRAVOOOO, SAFI SANA DADA, UTAFIKA MBALI MNO, USIDANGANYIKE TU! TUNAKUTEGEMEA IKULU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2010

    anon wa kwanza umenena huyo mtoto hajasoma shule ya msingi kawe,ni juhudi za wazazi wake na kwanini wizara hawakuuliza mama kwanini alimpeleka mwanawe shule ya private wakati kuna shule za serikali kila kona na ada karibu na bure?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2010

    Hongers sana Happiness Watimanywa,

    Kuongoza katika shule 150 duniani kamwe si jambo lelemama bali lenye kuhitaji juhudi kubwa na umakini wa hali ya juu huku ukijua na kutambua umuhimu wa kile ufanyacho,

    Mungu akutangulie na huu usiwe mwisho bali mwanzo tu wa nyota yako ya safari ya mafanikio na uongozi kung´aa zaidi,


    Well Done,
    Matukio

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2010

    Please let us know what has exactly happened? Tell us about how many Tanzanian students were allowed to participate and which criteria has been used to get Fatma as the best student in the world?

    Although I do not much about this event, but I do congratulate you for what you have achieved. Thank you and keep on.

    Matukio 1

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2010

    SERIKALI YETU BWANA, KWENYE MAFANIKIO WAKO KIMBELEMBELE KAMA WAO NDO WALIOTIA CHACHU YA MAFANIKIO, ILA KWENYE MAANDALIZI na KUWEZESHA AHHAAAA HUWASIKII, MIFANO MINGI IPO TU......HUU HAPA, HASHIM,..........ETC

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2010

    Kuchi Kuchi Hotahe.

    Tunaomba vigezo vilivyotumika.

    Amepambanishwa na shule zipi? Maana shule za chini ya viwango pia zipo. Mtu unaweza ukashika nafasi za juu katika shule zzzz, ikatokea ukahamishiwa katika shule yyyy, ukarushwa huko, ukawa unashika mkia tu, then inakubidi u-struggle kweli kweli ili u-catch up na wenzako. NAONGEA KUTOKANA NA UZOEFU.

    Point yangu ni kwamba, watu tusidanganyike na nafasi (position), kuwa sijui nimekuwa wa ngapi, no. TUANGALIE UWEZO WA MTU.

    Ila hongera Kadadaa.

    Ze Comedy,
    Ukonga.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2010

    well done young lady well done parents and teachers ju ju ju zaidi!!!

    Most of us old folks did our Cambridge International General Secondary Education from london.
    all government schools were very good and we all did this exams 'O'Level and 'A'LEVEL.my good old days.GOD BLESS YOU.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2010

    Humu kwa bwana misupu kuna watu wengine wavivu. Ikiiandikwa IGCSE ina maana ukiingia mtandaoni utapata kila kitu. Bwana misupu anatupa kwa taarifa tuu na mengine tufanye research wenyewe. Kabla hujaaandika tafuta kidogo tuu upate ukweli alafu toa maoni. Mdau nenda "www.igcsemaths.pbworks.com" utaona kwa mfano wanavyo "grade" asante kwa ushirikiano.

    ReplyDelete
  10. Hongera sana binti! Lakini kama mhusika hapa juu ningependa kujua pia shule zilizoshiriki katika mashindano hayo (duniani) ni zipi?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 24, 2010

    Wewe anon wa Sat Jul 24, 02:15:00 PM aka Matukio 1, jina la mtoto ni Happiness Watimanywa. Sasa jina la Fatma linatoka wapi? Are we reading the same thing?!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 24, 2010

    Hongera zake amejitahidi .. hiyo IGCSE scores are sufficient for entry to university in Swaziland, Lesotho, Zambia and Botswana. Nadhani ni kama SAT in the US...lakini kweli Serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania inajua kujisifia wakati watu wanatoa mihela yao kupata good education. Angetoka mtoto kufnaya vizuri mbuyuni primary basi ningewaelewa kwa kujisifia. Lakini st Constantine? hebu wakae kimya kabisa wampongeze na mzazi kwa hili..

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 25, 2010

    kwanza hongera sana dada kwa kuwa namba moja duniani. Kweli we ni noma na endelea hivohivo...you will go places!

    Pili, hawa wizara ya elimu wanatafuta nini kwenye ujikjo wa binti wa watu? Haya ndio mambo ya Kanye West kumwibia Taylor Swift her moment of glory siku ileeeee!

    Pumbaf kabisa! Huyu mama wa wizara sikumwona akiwa accountable matokeo ya form four yalipotoka earlier this year maana 17% tu ndio walipata kati ya div-I na div-III. 83% waliondoka na div-IV au zero! Where was she? mbona hatukuona sura yake ikisema kwamba anajiuzulu kwa kushindwa kufanya kazi yake? wote yeye na waziri wa elimu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...