Salaam mkuu wa libeneke.
Hongera kwa kazi nzuri ya kutuletea habari mbalimbali za nyumbani. Siasa, burudani, uchumi, jamii, .... furaha na huzuni.
Katika kupekura bei za madafu mtandaoni, nimeona tofauti kubwa ya bei za fedha kati ya BOT (Bank of Tanzania) ukilinganisha na bei katika mabenki ya ndani, maduka ya kubadilishia fedha na soko la kimataifa. Mfano nimeonyesha hapo chini, kwa tarehe 29/7/2010.
Yahoo: 29/07/2010: 1USD =1518.5 Tsh.
http://finance.yahoo.com/currency-converter/#from=USD;to=TZS;amt=1
NBC-TZ: 30/07/2010: Buying 1.426,42: Selling 1.546,42
http://www.nbctz.com/
BOT: 29/Jul/2010: Buying 1.368, 2466: Selling 1. 396,1700
http://www.bot-tz.org/
Kwa tarakimu hizo ina maana mtu unaweza kununua USD 10.000 kutoka BOT na kuziuza NBC na kupata faida ya zaidi ya T.Sh. 300.000 ghafla! Je hilo linawezekana? Ikiwa biashara hiyo haiwezekani, Viwango vya kubadilishana fedha vya BOT ni vya uongo au vinaonyesha nini?
Zaidi, nijuavyo mimi, ukituma fedha kutoka nje, fedha itabadilishwa kwa viwango vya BOT. Hivyo ukituma Tanzania SEK 20.000 za Sweden leo, kwa mfano, utapata Tsh. 3.760.000, wakati thamani yake katika soko la kimataifa ni T.Sh 4.200.000. Je hii si dhuluma? Kwa nini BOT isiwe na viwango vizuri vya kubadilishia fedha (Buying rate) ili kuwavutia watanzania walioko nje kutuma fedha nyumbani, badala ya kuweka viwango vya kukatisha tamaa na kuzikosesha familia zetu maisha bora na pia kulikosesha taifa fedha za bure kabisa za kigeni?
Ni imani yangu tutapata maelezo ya kitaalamu kutoka kwa wajuzi wa mambo ya fedha, au BOT wenyewe!
Nakutakia kazi njema,
Mdau MCL
Hongera kwa kazi nzuri ya kutuletea habari mbalimbali za nyumbani. Siasa, burudani, uchumi, jamii, .... furaha na huzuni.
Katika kupekura bei za madafu mtandaoni, nimeona tofauti kubwa ya bei za fedha kati ya BOT (Bank of Tanzania) ukilinganisha na bei katika mabenki ya ndani, maduka ya kubadilishia fedha na soko la kimataifa. Mfano nimeonyesha hapo chini, kwa tarehe 29/7/2010.
Yahoo: 29/07/2010: 1USD =1518.5 Tsh.
http://finance.yahoo.com/currency-converter/#from=USD;to=TZS;amt=1
NBC-TZ: 30/07/2010: Buying 1.426,42: Selling 1.546,42
http://www.nbctz.com/
BOT: 29/Jul/2010: Buying 1.368, 2466: Selling 1. 396,1700
http://www.bot-tz.org/
Kwa tarakimu hizo ina maana mtu unaweza kununua USD 10.000 kutoka BOT na kuziuza NBC na kupata faida ya zaidi ya T.Sh. 300.000 ghafla! Je hilo linawezekana? Ikiwa biashara hiyo haiwezekani, Viwango vya kubadilishana fedha vya BOT ni vya uongo au vinaonyesha nini?
Zaidi, nijuavyo mimi, ukituma fedha kutoka nje, fedha itabadilishwa kwa viwango vya BOT. Hivyo ukituma Tanzania SEK 20.000 za Sweden leo, kwa mfano, utapata Tsh. 3.760.000, wakati thamani yake katika soko la kimataifa ni T.Sh 4.200.000. Je hii si dhuluma? Kwa nini BOT isiwe na viwango vizuri vya kubadilishia fedha (Buying rate) ili kuwavutia watanzania walioko nje kutuma fedha nyumbani, badala ya kuweka viwango vya kukatisha tamaa na kuzikosesha familia zetu maisha bora na pia kulikosesha taifa fedha za bure kabisa za kigeni?
Ni imani yangu tutapata maelezo ya kitaalamu kutoka kwa wajuzi wa mambo ya fedha, au BOT wenyewe!
Nakutakia kazi njema,
Mdau MCL


mdau naona umepoint out inconsistency vizuri kabisa hapo kwa kusite kabisa sources mbalimbali. Ila USIJIDANGANYE kwamba higher exchange rates is good for the country. Uchumi 101 ndugu yangu! unapoona kwamba dola, au yen au yuro zinakuwa na thamani ya juu (unabadilisha na kupata shilingi nyingiiiiii) ujue hali yako kama mtanzania ni mbaya kiuchumi! your currency is getting weaker relative to other currencies. Kitu mbaya sana hiyo!
ReplyDeleteMheshimiwa kwani wewe hujui kwamba BoT ndiye wholesaler wa forex na pia mabenki yote huwa wanaenda kununua forex BoT kwa njia ya mnada fulani hivi.
ReplyDeleteMie sioni tatizo lolote ni kwamba hukuperuzi vizuri kabla ya kupost dukuduku lako.
Mdau wa Fri Jul 30, 08:13:00 AM'...Wholesale...', uko sahihi kabisa. Hizo ni average interbank rates na sio za rejareja. mtu binafsi hawezi kwenda kununua pesa ya kigeni benki kuu, unanunua toka kwa wauzaji wa rejareja ambao ni mabenki na bureau de changes
ReplyDeleteDuh..
ReplyDeleteMkuu imekuwaje umeweza kuperuzi hizo info kwenye internet lakini ukashindwa kuperuzi jinsi Maduka ya kubadilisha fedha yanavyofanya kazi na kupata faida??!!
BoT au Benki Kuu yoyote ndiye Muuzaji wa Jumla (Whole Seller) wa Fedha za kigeni kwa nchi husika. Benki Kuu wao "wanasimamia" viwango vya kubadilisha fedha kutokana na hali ya uchumi (kununua na kuuza nje ya nchi).
Maduka ya Fedha za kigeni yanaenda kununua fedha BoT kwa bei ya jumla, kisha wanakwenda kukuuzia wewe na mimi kwa faida. Faida kiasi gani wataweka nadhani ni juu ya mwenye duka/ benki (sina uhakika sana kwenye hili) ila bei yao ni lazima iwe na ushindani na kuvutia wateja wao.
Hiyo ndiyo sababu BoT hawauzi fedha za kigeni kwa mimi na wewe/ reja reja. Na ndio sababu kwa hesabu zako unaona hiyo faida ya 300K.
Nina imani nitakuwa nimechangia kidogo.
dawa hapo ni kuwaambia ndugu zako wawe na account za dola.Ukishamuwekea USD anaenda kubadilisha mwenyewe kwenye viosk.BOT ni nyumba ya ufisadi.
ReplyDeletekwanini uweke nukta (.) katikati ya pesa ulizoandika?
ReplyDeleteunajua maana yake?
BoT sio bank ya biashara (commercial) kwa hiyo mtu binafsi hawezi tu kuingia BoT na kununua madola kwenda kuyauza.
ReplyDeleteBoT inatunza fedha zote za nchi (local na forex).
BoT wanasimamia banks zingine na kutunza pesa za bank hizo.
BoT ina-rgulate mzunguko wa pesa ikiwa ni pamoja na uuzaji wa Forex kwa banks zingine.
Anon wa kwanza na wa pili, suala linaloongelewa hapa halihusu thamani ya fedha jinsi tunavyotaka, bali thamani halisi ya wakati huo. Ikiwa BOT watauza 1USD kwa T.Sh 1396 na wao wakanunua kwa T.sh 1518 huko zinako patikana, hiyo itasaidia vipi thamani ya fedha yetu? Je CRBD wanaweza kununua fedha BOT na kuwauzia NBC na kupata faida kubwa?
ReplyDeleteWadau wa kwanza hapo juu nadhani hamjaelewa anachosema mtoa mada.Yeye anadai kwanini nini BOT wawe exchange rate "n"
ReplyDeletehalafu taasisi nyingine za fedha ziwe na exchange rate "n"+K(YYY)where n=positive,K=Positive CONSTANT and YYY=Positive!na kwamba mtu unaweza kununua dola kutoka BOT na kwenda kuziuza kwenye mabenki au bureaux de change ukapata faida kubwa.Tunaelewa taasisi zinafanya biashara BUT kazi mojawapo ya blog ni kuelimishana,kwa hiyo tuwaachie watalaam wa uchumi na fedha watuelimishe.Siyo vizuri kumshambulia aliyeuliza.Mimi binafsi sina uhakika kama mtu binafsi unaruhusiwa kwenda kununua pesa za kigeni BOT.
Hivi nyinyi nani kawaambia shillingi ikishuka thamani ni mbaya? Kuna kiwango kikipindukia ndio inakuwa mbaya but kama imeshuka kidogo kuna faida na hasara zake.
ReplyDeleteWewe Anonym wa Tarehe Fri Jul 30, 09:46:00 AM, uko myopic kisawasawa. Wafikiri kuwa ushahitimu elowai! Kwa ufupi, ilimu yako ni loko!
ReplyDeleteKuna nchi, kama vile EU, wao hutumia coma (,) kwa decimal point, na nukta kwa thousands grouping symbol. Ok sasa nakupa digirii, yaani unastahili kugradjueit! Hahaaa
Chiaaaz Mchizi
Kama nilivyosema kwenye anony #2, BoT ni W/saler na yeye anaweka utaratibu tu wa uendeshaji, na mabenki wanaweza nunua na kuuziana wenyewe kwa wenyewe hakuna tatizo mradi hawavunji sheria. ni soko huria
ReplyDeleteUkweli ni kwamba, thamani ya pesa kushuka au kupanda kunawze kuwa na faida na hasara pia. Labda nitolee mfano wa China, fedha yake inaonekana kuwa undervalued. Mataifa na mashirika ya Kimataifa yamekuwa yakipiga kelele ili nchi yao ipandishe value ya ile pesa. Faida hasa kwa china katika hili ni kwamba nchi inaweza kuexport zaidi kuliko kuimport na hivyo kuwa vyema kwenye balance of payment. Kwa lugha rahisi ni kwamba bidhaa zinazotoka China zinakuwa nafuu kuliko bidhaa zinazotoka kwingineko.
ReplyDeleteSasa tukija kwenye exchange rates ni kweli BOT hawauzi rejareja na pia wao wanatoa indicative rates tu. Lakini pia kuna tatizo katika soko la fedha bid-ask spread (bei ya kuuzia na kununulia zinatofautiana mno. Kuna hitajika control fulani. Mdau kazungumzia suala la ndugu zake kupata pesa ndogo, si kweli kwamba pesa inayotoka nje exchange rates inatathminiwa na BOT. Atazame upya njia nyingine za kutuma pesa zake.
Mimi naona mdau ametoa issue mwafaka kabisa ingawa inawezekana amechemka hasa kwenye swala la yoyote kwenda kununua dola BOT na kuuza. Maumivu ya BOT yanawakumba hasa, pamoja na wengine watumishi wa serikali. Unaposafiri nje unapwea allowance in terms of dollars na rate zake zinachukuliwa BOT. Kwa kusema hivi, aloyaeleza muibua mada ni sahihi kabisa.
ReplyDeleteIt is true that BOT is the wholeseller of foreign currency. HOWEVER the exchange rate of BOT may influence the behavior of certain stakeholders. For that reason, it is valid to ask 'who is benefiting from such rates????'. Certain individual companies? or the country as a whole???
ReplyDeleteKwa wale wanaotaka kusoma zaidi kuhusu maswala hili, the appropriate literature is called: MICROFOUNDATION.
by Dr. xxx
Nadhani wataalamu wanahitajika kujibu hili swali. Inawezekana vipi bei ya kununulia fedha BOT (Mnunuzi awe Bank, taasisi ya fedha kampuni au mtu binafsi) wakauza fedha za kigeni kwa bei ndogo kuliko ile ya kuuza katika Mabenki na Bureau de change? Ikiwa ni hivyo kwa nini mabenki wahangaike kununua fedha hizo kwa bei ya juu kutoka kwa wateja wa rejareja wakati wanaweza kupata BOT kwa bei chee?
ReplyDeleteNakumbuka siku za nyuma wakati $1 was Tsh/=600.00, when Mkapa was in the office. Kwa sasa fedha za kigeni zina wabenefit watu wanaofanya kazi kwenye mashirika ya kigeni na kulipwa in term of their currencies and for those who works in abroad. Kwa wenzangu na mimi wamachinga, Mungu atusaidie.
ReplyDeleteMdau uliyeuliza swali pamoja na wengine ambao wameomba ufafanuzi zaidi wa majibu yaliyotolewa.
ReplyDeleteKwanza naomba niseme kwamba quotations za exchange rate ambazo zinaonyeshwa kwenye website ya BoT, ni INDICATIVE. Naomba uelewe maana ya indicative, kwamba taasisi zote za fedha ambazo zinajihusisha na kufanya biashara ya kuuza na kununua fedha za kigeni wanaangalia hiyo rate kwanza ndipo wanapopanga bei zao.
Pili, hiyo indicative exchange rate huwa inapatikana kwenye mnada wa soko la fedha za kigeni ambalo linahusisha taasisi zote za fedha ambazo zinajihusisha na kuuza/kununua fedha za kigeni. So, ni swala la market forces. Kama wananchi wana fedha nyingi za kigeni, maana yake wataenda kuziuza au kama wanahitaji fedha nyingi za kigeni, maana yake wataenda kununua. Sasa kinachofanyika, bureaux ambazo zina fedha za kigeni zinapeleka kuuza kwenye huo mnada, na kama wanahitaji wanaenda kununua kwenye huo mnada. Siku inapoisha, BoT wanakaa chini na kuona average price ya kuuza na kununua fedha za kigeni kwenye mnada ilikuwa kiasi gani na kesho yake ndio wanachukua hiyo bei kama indicative.
Individual financial institutions wanahaki ya kujipangia exchange rates zao kwa kuangalia soko likoje (yaani uhitaji ama uwepo wa fedha za kigeni ni mkubwa kiasi gani), ambayo ni maswala ya demand and supply ambazo ndiyo hu-determine bei ya kitu chochote sokoni.
Pamoja na hayo, kuna tatizo la kimfumo wa uchumi hasa ukiangalia kwamba kwanini kuwe na gap la shilingi mia au zaidi kati ya indicative exchange rate na bureax exchange rate. Hili linatokana na soko letu la fedha za kigeni kutokuwa la kiushindani zaidi na ndiyo maana wenye maduka ya fedha za kigeni na mabenki, wanaweka rates za juu zaidi ukilinganisha na rates zinazoonyeshwa na BoT.
Mfano, mwaka 2000 nilienda Arusha kutembea, nikaamua kwenda Ngorongoro kutembelea mbuga za wanyama. Nilipofanya booking ya hoteli Arusha mjini, niliambiwa bei zao ziko kwenye dollar lakini ninaweza kulipa kwa madafu. Nikawa ninataka kulipa kabisa, mhudumu wa hapo Arusha mjini aliniambia usilipie hapa, nenda kalipie huko huko Ngorongoro. Nilipomuuliza ni kwanini, akasema nikilipia Arusha mjini rate ya dollar ni kubwa, so nitaishia kulipa hela nyingi sana. Nikamuuliza ni bei gani hapa, nadhani ilikuwa kwenye around shilingi 860 kwa dollar. Nilipoenda Ngorongoro nililipa kwa rate ya shilingi 790 kwa dollar. Nilibaki na maswali mengi sana, kwamba wote wako Arusha, why Ngorongoro wawe na rate ndogo na mjini wawe na rate kubwa? Kibaya zaidi hoteli zote mbili ziko chini ya kampuni moja.
Kwa hiyo tatizo kubwa la soko la fedha za kigeni hapa kwetu ni imperfect market, information haiko wazi na pia wanaojishughulisha na biashara hiyo wana mambo mengi na hasa kwenye bureaux. Kuna baadhi ya bureaux ukienda wanakuuliza kama unataka receipt, ukisema NO, wanakupa rate nzuri, ukisema YES wanakupa ile waliyoweka kibaoni. Pia ukienda na hela nyingi za kigeni ama unahitaji fedha nyingi za kigeni unaweza kuuziwa/kununua kwa rate ambayo ni tofauti na ile iliyoandikwa kwenye ubao nje.
Hapo ndipo BoT wanatakiwa kufanya utafiti wa kina na pia wawe wanachunguza kwa makini.
Sheria ya fedha za kigeni inasema mtu akitaka kutuma fedha nje ya Tanzania lazima apeleke uthibitisho (documents) kuonyesha anataka kuzituma kwa ajili ya nini. Sasa ukienda Bureaux na ukaulizwa kama unataka/hutaki receipt ni kwamba mwenye duka anataka kufanya transactions ambazo zitamsaidia kutorosha fedha nje ama kukwepa kodi kwa kuwa kila transaction anayofanya lazima ina faida, na faida hiyo lazima itozwe kodi. Huo ndio uhuni ambao unafanywa na baadhi ya wamiliki wa maduka ya fedha za kigeni.
KAMA HUJASOMA BANKING AND FINANCE HUTAELEWA HATA MTU AKIKUELEZAJE, NA HASA INTERNATIONAL BANKING ND INTERNATIONAL FINANCE. EBU TUONGEE KWA NDANI TU. CENTRAL BANK KAMA BANK KUU NI BANKER WA BANKS ZOTE KATIKA NCHI NA NI DUKA LA PESA KWA MABANK, BANK ZOTE HUIFADHI PESA ZAO ZA ZIADA NA ZILE AMBAZO WANATAKIWA KUZIWEKA BANK KUU KWA MUJIBU WA SHERIA ZA KIBANK. NA ILE RATE YA BANK KUU NI RATE KARIBU NA UKWELI NA HIZI ZA MABANK NI ZA BIASHARA WALA HAZIWI CONTRILLED NA MTU YOYOTE ZINATAWALIWA NA SUPPLY NA DEMAND KATIKA SOKO LAKE. HIVYO HIVYO KWA MIKOPO UNTAONA BANK ZINAKOPA BANK KUU KWA RATE NDOGO NA PESA HIZO HIZO WANAKOPESHA WATU KWA RATE KUBWA. KWA MFANO RATE YA BANK OF LONDON KWA MABANK NI 0.5% LAKINI BANK MJINI WANAKOPESHA WATU PESA HIYO HIYO KWA RATE PENGINE ZAIDI 20% KIFUPI NI BIASHARA SAWA NA MKULIMA WA MUHOGO MKURANGA ANAUZA GUNIA LAKE LA MUOGO SHS 10 NA MCHUUZI WA KARIAKOO ANAKUJA UZA GUNIA HILO HILO SHS 20 KWA HILI LA MUHOGO PENGINE UNA ALTERNATIVE UNAWZA KWENDA MWENYEWE MKURANGA NA KUNUNUWA KWA BEI RAHISI LAKINI LA DOLAAR HUWEZI KWENDA KUNUNUWA KAMA INDIVIDUAL BILA KUPITIA BANK ZA MTAANI. SO SIMPLY NI BIASHARA YA KUUZA NA KUNUNUWA BANK ZA MTAANI WANAWEKA BEI JUU KUPATA FAIDA KAMA BISHARA. JARIBU KIDOGO KUTAFUTA VITABU VINAVYOZUNGUMZIA MASWALA YA PESA ZA KIGENI NA MAMBO YA EXCHANGE RATES UTAELEWA
ReplyDeleteKuna wadau wawili hapo juu wameongea point za maana kwenye kuelimisha umma.
ReplyDelete1) 'quotations za exchange rate ambazo zinaonyeshwa kwenye website ya BoT, ni INDICATIVE.'
Tarehe Fri Jul 30, 10:35:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
2)'..ILE RATE YA BANK KUU NI RATE KARIBU NA UKWELI NA HIZI ZA MABANK NI ZA BIASHARA WALA HAZIWI CONTRILLED NA MTU YOYOTE ZINATAWALIWA NA SUPPLY NA DEMAND KATIKA SOKO LAKE.'
Tarehe Fri Jul 30, 11:13:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Japokuwa kunakaukweli kwenye discussion za wadau hapo juu, mimi naona bado hawajamjibu mdau MCL.
1) Mimi nilitegemea kusikia kuwa rate ya Central Bank si tu INDICATIVE , but also it is a rate which is set appropriately to stabilize the economy and set the country into development and growth.
2) Pili tuwe makini hapa. kwenye macroeconomics (whether it is keynesian or monetarist school of thought) you will be aware of the fact that cetral bank is also the regulator of supply and demand. mdau kwenye quotation ya pili angetakiwa kusema nini maana ya RATE KARIBU NA UKWELI. Je hii ndiyo hiyo hiyo rate ambayo mdau MCL ana wasiwasi nayo??
Dr. xxx