JK na mgeni wake Rais Luiz Inacio Lula Da Silva wa Brazil wakitazama vifaa mbalimbali katika Banda la Jakaya Mrisho Kikwete ikiwa ni sehemu ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya maonyesho ya Mwalimu Nyerere Jijini Dar. Wa kwanza kulia ni Meneja Mkazi wa Brazafric nchini Tanzania Bw. Readou Sakwa.
JK na mgeni wake Rais Luiz Lula Da Silva wakiingia ikulu jijini Dar na kulakiwa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza kumpokea leo mchana.
JK akionesha umahiri wake wa kupiga ngoma wakati alipomkaribisha Rais Luiz Lula da Silva wa Brazil(kushoto) ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.
akionesha umahiri wake wa kupiga ngoma wakati alipomkaribisha Rais Luiz Lula da Silva wa Brazil Ikulu jijini Dar.

Rais Luiz Lula Da Silva wa Brazil akimuangalia Simba dume aliyekaushwa kwa utaalamu na kuwekwa kama pambo katika mlango wa ikulu jijini Dar

Rais Luiz Lula Da silva wa Brazil akimkabidhi JK namba 9
iliyosainiwa na wanasoka wote nyota wa timu ya Brazil
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2010

    Maskini huyu Raisi wa Brazil alikuwa amepanga safari yake Bongo aikujua Brazili wanatinga fainali Sauzi ili aende kuangalia. MAtokeo yake ngoma ni Spain VS Dutch!!! Pole sana Mheshimiwa Raisi Luiz Lula

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2010

    nampa pole sana rais wao alidhan atakuwa hajachoma mafuta ya bure kuja tz akijua anaunganisha mpaka sauzi duh!imekula kwake mpira siku hz sio mazoea ni sayansi mnajipanga na ushindi unatafutwa wao bado wanadhan mpira ni majina!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2010

    Wachangiaji hapo juu mfuatilie protokali basi japo kidogo. Raisi wa Brazil inabidi awepo South Africa siku ya kufunga mashindano ili kupokea kijiti kama nchi mwenyeji wa mashindano yajayo 2014 hiyo ni kawaida. Thabo Mbeki did that before as well japo Sauzi hawakufika fainali. Kwa hiyo Brazil ifike fainali isifike Prez Lula was supposed to be in J'burg this weekend.

    ReplyDelete
  4. Hadj Drogba "mwana chelsea"July 08, 2010

    KAKA JAKAYA NAJUA WEWE HUKOSI KUINGIA HUMU KWA MICHUZI,HIVYO BASI NACHUKUA NAFASI HII KUKUOMBA HIYO JEZI YA BRAZIL UNIPE MIMI IKIWEZEKANA TUBADILISHANE MI NIKUPE YA TAIFA STARZ WEWE UNIPE HIYO AFTERALL WEWE SI UNAYO ILE YA BASKETBALL,YA YANGA NA YA REAL MADRID,SO SIAMINI KAMA UTALETA UPINZANI KATIKA OMBI LANGU HILO,KWA MAWASILIANO YA AWALI NIBONYEZEE HAPA diadolla@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2010

    ANOY WA 12:00 UNA UTULIVU WA AKILI, MUNGU AKUZIDISHIE. NAFIKRI HAO WAJUU YAKO WAMEISOMA JAPO KIMYA KIMYA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2010

    If you look at President Lula he looks rather embarassed in that picture where President Kikwete is fooling around with the drums.

    ReplyDelete
  7. Ndoto ya mchana,Sweden.July 08, 2010

    Rais wetu msanii kweli kweli,hizo ni gia za kuwezeshwa na misaada ya manoti toka Brazili.Hapo Jk anamburudisha Rais wa Brazil ili alainike.hapo Jk ananena '' mimi bingwa sana haya yote madrumm na mangoma nacharaza kisawasawa mimi hapa ndio bingwa wao, beat zote zimetunga mwenyewe na namewafundisha. Anaendelea ''na yale majoka ya mablack dance na majazz yanaruka kisawasawa na nimeanza kucheza ma capoeira kule Bagamoyo wakati wa msimu wa mavuno ya njugu mawe,korosho na nazi.

    tete te Rais wa Brazil '' deni lote nalifuta na nitakualika wakati wa sikukuu yangu ya kuzaliwa ili utuburudishe na kula caruru.
    Ndoto ya mchana,Sweden.

    ReplyDelete
  8. How is Tanzania going to benefit out of that jersey? You could have get that jersey when Brazil came to play in Tanzania which I think was an appropriate time. Mr Lula can teach you 102 things how to get Tanzania out of the ditch just like they did in Brazil.
    Mr. President you can do better, leave that jersey nonsense to your kids deal with the real issues that your citizens are facing, corruption for a starter is that too much to ask?

    ReplyDelete
  9. Aliyewajibu wachangiaji wawili pale juu (Anony), yawezekana ni Mh. JK mwenyewe, akiwaelimisha ndugu zetu hao kuhusu mambo ya protokali yalivyo.

    Blogi ya Michuzi inasomwa na watu wote anzia mkulima hadi Marais wa nchi za Afrika Mashariki kwa vile wanakijua Kiswahili.

    Na huyu "Ndoto ya mchana wa Sweden", ni kweli yumo usingizini, tunamtakia ndoto njema. Akiamka ataona ukweli ulivyo na atajicheka mwenyewe.

    It's Great To Be Black=Blackmannen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...