JK akipungia wanachama wa CCM waliojitokeza wakati akirejesha fomu leo
JK akimkabidhi katibu mkuu wa CCM fomu zake
Katibu mkuu wa CCM Mh. Yusuf Makamba akihakiki fomu za JK

JK akihutubia baada ya kurejesha fomu
pongezi kwa kurejesha fomu

hongera!
Leo tarehe 01 Julai, 2010 Nd. Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kurudisha fomu za kuwania Urais kwa awamu ya pili kupitia Chama Cha Mapinduzi. Zoezi hili litarushwa live na ITV na kwa wale walio nje ya Tanzania wataweza kuangalia kupitia mtandao wa internet. Link inapatika kwenye website ya CCM. Kuona tukio hili live BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2010

    Mh Michuzi
    Mpiganaji wetu Mr II amefikia wapi na vihunzi vilivokuwa vinamkabili? Nafurahi kusikia muda wa kurudisha form umeongezwa.Hatua hii itawawezesha wanyonge kama Mr II kutekeleza malengo ili kilio cha watu wa chini kisikike.
    vijana Kizazi kipya oyeee
    Mr II oyeeeeeee

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2010

    Naona live TBC ktk hiyo linki.

    Mdau
    Reading UK

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2010

    ukubwa unaraha zake hapo kikwete humtowi hata kwa marungu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2010

    Wewe nawe! Mr II na JK wapi na wapi? Mada ni kurudisha fomu za kugombea urais unaleta hadithi za Mr II, kwi kwi kwiikiiii! Afadhali ungeuliza wagombea wa nafasi hiyo kwa kambi ya upinzani wako wapi ningekuelewa.

    Anyway ndo elimu yetu hiyo mada nyingine swali laulizwa la mada tofauti, na kwenye mtihani hali kadhalika

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2010

    Hivi kuna aja gani ya kuwa na mbwembwe zote hizo na matumizi ya ajabu ya pesa za watu maskini kwenye nchi yenye utajiri wakati huna mtu unayeshindana nae?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2010

    Nimeipenda hii.Nampongeza JK.Hamu yangu ni kusikia jina la mgombea mwenza ambaye atakuja kuwa makamu wa raisi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 02, 2010

    Ni kweli kwamba CCM hakuna mtu wa kushindana na JK??? au ndo KUPANGANA huko???????????? Kweli hii siasa ya TZ ni ya aina yake.hakuna democrasia ya kweli !!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 02, 2010

    demokrasia ya kweli maana yake nini? wewe uliye mwanademokrasia kwa nini haukwenda kwa Makamba na kuchukua fomu ukapambane na JK huko CCM? Eboooo .... unataka nani akufanyie kama siyo mwenyewe ... simama mwenyewe acha kulaumu ... Demokrasia demokrasia ... hata haujui maana yake, unaropoka tu!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 02, 2010

    raisi wa tanzania na mwenyekiti wa ccm nini chengine anataka tumpatie,...mfalme wa jamhuri ya watanzania au?

    ReplyDelete
  10. Hv Shibuda ilikuwaje tena? hw watu bwana, makamba anamwita JK ni mtumishi wa mungu...Hahahahahaha.
    I WANNA KILL RIGHT NOW!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...