Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa wanafamilia ya Mzee Ally Sykes kufuatia kifo cha mpendwa wao, Bwana Addah Sykes, kilichotokea Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Bwana Addah Sykes alifariki dunia Ijumaa, Julai 2, 2010, kwenye Hospitali ya Kijitonyama, Dar es Salaam na kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni jana, Jumapili, Julai 4, 2010.

Katika salamu zake kwa wanafamilia hao, Rais Kikwete amesema kuwa ameguswa sana na kifo cha Bwana Addah Sykes akifafanua, “Nimepokea kwa mshutuko mkubwa na huzuni nyingi habari za kifo na msiba wa Bwana Addah Sykes. Napenda kwa dhati ya moyo wangu kuwatumieni nyote wanafamilia ya Mzee Sykes salamu zangu za rambirambi kutoka moyoni kutokana na msiba huo.”

Ameongeza Rais Kikwete katika salamu zake za rambirambi: “Msiba wenu ni msiba wetu. Namwomba Mwenyezi Mungu awapeni nguvu na subira ili muweze kuvuka katika kipindi hiki kigumu cha majonzi makubwa ya kupotelewa na mpendwa wenu.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
05 Julai, 2010

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2010

    RIP

    By the way who is Addah Skyes?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2010

    RAIS KASAHAU KUTUMA RAMBIRAMBI KWA NDUGU NA JAMAA WA YULE ASKARI ALIYEJIBANJUA KWA RISASI BAADA YA KUHUJIWA NI KWA NINI ALIUPOTOSHA MSAFARA WA RAIS, RIP Ras Makunja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...