Waziri Ally akielezea chimbuko la Old Skul
Wasanii wakongwe wa muziki wa dansi SabaSaba hii wanatarajiwa kufanya show moja ya kukata na shoka kusherehekea siku hiyo.
Onyesho hilo la wakongwe litafanyika siku ya kilele cha sikukuu ya Sabasaba na kurindima katika viwanja nja Karimjee ambako kulikuwa Binge la zamani huku ikifahamika kwamba hapo ndipo safari ya Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta ilipoanza ambapo alianzia ukarani hadi sasa amekuwa Spika.
Akifamaisha zaidi kwa niaba ya wasanii wengine wakongwe mratibu mkuu wa onesho hilo Waziri Ally alisema kutakuwa na mambo ya kizamani siku hiyo pamoja na mitindo ya kizamani ya mavazi viatu na nywele pia.
"Mdau njoo na raizoni, bugaluu bila kusahau mitindo ya nywele kama Afro na zile nywele za uzi ndefu walizokuwa wakisuma mama zetu enzi za usichana wao, alisema Waziri ambaye pia ndiye kiongozi wa Njenje.
Amesema kiingilio ni sh. 5,000 tu kwa mtu mmoja ambapo onesho litaanza milango ya saa 12 jiono hadi saa sita.Fedha zitakazopatikana zitapelekwa kusaidia kwenye vituo vya watoto yatima na wazee wasiojiweza.
Wakongwe hao pamoja na bendi wanazopigia ni Waziri Ally,keyboards /Vocal (NJENJE),Muhidini Maalim Ngurumo,Vocals (MSONDO), Bi Shakila Said Vocal (JKT) ,King Kiki Vocal (WAZEE SUGU) Shaaban Dede Vocal (MLIMANI PARK), Mabrouk Hamisi Vocal/Drums (NJENJE),Hamza Kalala Vocal/Guitar (BANTU GROUP) ,Hassan Bitchuka Vocal (MLIMANI PARK) Mafumu Bilali Saxophone (AFRICAN BEAT) ,Juma Ubao Vocal/Guitar (SIX MANYARA).
Wengine ni Said Mabera Guitar (MSONDO) ,Hamisi Mirambo Trumpet (MLIMANI PARK), Abuu Semhando Drums (TWANGA PEPETA), John Kitime Vocal/Guitar (NJENJE), Kabeya Badu Vocal (WAZEE SUGU), Habibu Abbas Jeff Drums (MLIMANI PARK) Abdul Salvador Keyboards/Vocal (HISIA SOUNDS),
Wengine ni Ally Jamwaka Percussions and Congas (MLIMANI PARK) Mzee Juma Sangura Bass Guitar (SIX MANYARA naye ni mpiga bezi wa Salum Abdallah na Cuban Marimba), Mohamed Mrisho Guitar (NJENJE), Shaaban Lendi Saxophone (MLIMANI PARK), Keppy Kiombile Sound Engineer/Bass (NJENJE), Yusuf Bernard Saxophone (MLIMANI PARK), Juma Omari Vocal/Drums (NJENJE), Mustafa Ngosha Bass (MLIMANI PARK), Mbaraka Othman Trumpet (MLIMANI PARK).
PONGEZI SANA VIJANA WA ZAMANI TUKO NYUMA YENU TUTA WASAPOTI KWA HALI NA MALI.VIJANA WA LEO(BONGO FLEVA)JARIBUNI KUWAENZI WAKONGWE HAWA, JIFUNZENI KUPIGA MA VYOMBO KAMA,TUMBA AO CONGAS, TARUMBETA,SAX,TROMBONE,GITAAZ,KINANDA ILI MUZIKI WENU UVUKE MIPAKA KAMA VIJANA WA ZAMANI AKINA DR.REMMY ONGALA WALIVYO TANGAZA TANZANIA KIMUZIKI KIMATAIFA.
ReplyDeleteJamani mwe mkono wangu kichwani. Bongo Oyee! Jamani natamani nipae nipae. Fanyeni kila miezi 3 jamani nami nije. Hongera sana. Tanzania Oyee Old skul oye.
ReplyDeleteOngereni sana. Mi ni kijana 22years old lakini napenda zilipendwa, yani nikizisikiliza nazisikia hadi moyoni, i can feel the words na vyombo. Nipo US ila na cd na tape za zilipendwa nyingi tu.
ReplyDeleteNi kweli, hapo badae kutakua hamna mpiga vyombo watakuwa wachache sana.. mi na mdogo wangu tukiwa wamoja wapo, gita napiga zilipendwa kadhaa kama Georgina,twist ya Daudi kabaka n.k nyimbo za dini na nyimbo chache za bob marley..nikiwa na mda free that's what im doing, playing gita.
Inabidi mngefikiria kuwafundisha watu ili nyimbo hizi za zamani zisipotee...mi nimefundishwa kutumia vyombo na mzee wangu kwani wasanii wazamani walikuwa wanakuja kufanyia mazoezi nyumbani, ambao wengi wao ni marehemu mda huu. Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi.
Mdau,
USA
NILIKUPELEKA KWA WAKWE ZAKOOO UKAONANE NADUGU ZANGU EHEEE
ReplyDeleteATA MAMA YANGU ALIKUPENDA SANA, NA NDUGU ZANGU WALIFURAHI SANA,MAPATANO YETU DADA NIKUONA KAMA TUKICHUNGA HESHIMA YETU EEEEE
OH!!!!!!!!BWANA WAZIRI(BICHUKA HUYO)
CHOURAS......
SASA NASIKIA UMEFANYA VISA VINGI ATA MAMA YANGU HUTHAMINI EEEE,(NILIKONYA KITU KIMOJA UTUNZE HESHIMA KWA WAKWE ZAKOO UKA PUUZA)MAJI YAKISHA MWAGIKA HAYA ZOKI,ILIOBAKIA MAJUTO NENDA UENDAKO SALAMA.HUU ULIKUWA MSONDO WA NUTA NGOMA ZA ASILI AKILI KICHWANI MWAKO(MMOJA KATI YA MUHIMILI WA NCHI HII),TUNGO HIZI AKUNA TENA NA VIJANA SASA TULIO WATEGEMEA KUWA VICHWA VYA NEXT GENERATION WANALENGA KWENYE EASY MONEY,WE WAZA KIKUKU CHA MAMA RODA KIMEKULA MTAMA WANGUUU,BATA KAVAA RAIZONI KUKU KAPANDA BAISKELI,MGEFANYA JAPO MARA 2 KWA MWAKA NA KUWAALIKA VIJANA WETU WAJIFUNZE NA MUWAPE USHAURI NASAA,KWENYE NYWELE(AFRO)MI MGOGORO ENZI YETU UNATIA WELA CRAM KICHWANI IJUMAA JUMAMOSI,NYWELE KAMA JIMY KELLY AU FRED WILLIAMSON,UNAPULIZIA V05 BABAKE ATA UKISIMAMA JUU YA PIK UP JAGWANI AFRO AIYUMBI,SIDEEFFECT IMEKUJA SAA KUMI NAMBILI KASOROBO KIPARA KAMA MACHAVA STADIUM ILA HIVYO HIVYO NTAKUJA KUMSIKA NA KING KIKI NA OHHHH MAGIEEEEEEEE SANGONGAI NA YOKITEEEOHOOOO BALOBI TOBOYANGAA LELELLLEEELLEEEE,NILIEEEEE WATU LIAA NATAKA KUCHEKA WATU HAHAHAHA!!!!!!!!!!!!TELEMUKA,TELEMUKA BISANGALAAA.MZEE MWEMA MUJANGA MZEE CHEKECHA.MBONA AYUPO AU MAMBO YA PEPA BONGO MPAKA LEO AYAJAKAA SAWA.