Mwenyekiti wa Klabu ya Watford, Simon Prodger akimkabidhi jezi ya timu hiyo Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Chabaka F. Kilumanga kama inshara ya kumkaribisha Klabuni kwao. Naibu Balozi amealikwa kuhudhuria hafla rasmi ya kwa ajili ya timu hiyo itakayoandaliwa na Meya wa Mji wa Watford, Ijumaa ya tarehe 6 Agosti 2010. Wakishuhudia kwenye picha hiyo ni Hamisi Abdallah (kushoto mwenye fulana nyekundu) na Khalil Rehmtullah (kulia kabisa) ambao ni wachezaji wa Timu ya Taifa wanaochezea klabu ya Watford msimu huu wa Cricket ulioanza Aprili. Kushoto kwa Mhe. Kilumanga ni mmoja wa makocha wa WTCC Gulfraz Riaz. Pamoja na kuchezea timu hiyo Khalil na Hamis ni makocha wa timu za watoto za mji huo kwa miaka miwili sasa.Klabu ya Watford, inayoshiriki ligi kuu ya England, inayotarajiwa kumalizika mwezi Septemba, mwaka huu imeamua kuitangaza Tanzania, hasa kupitia kituo cha Biashara (London Trade Centre) kwa kuvaa jezi zenye bendera ujumbe wa kuwakaribisha watu kuwekeza (TANZANIA: A Destionation of Choice), kama inavyoonekana kwenye picha. Jezi hii pia inapatikana kwa £25 kupitia Ubalozini (Piga namba 02075691470 au 02077588070).Mchezo wa Cricket ni mchezo wakitimu wa pili kwa umaarufu nchini Uingereza, baada ya soka. Tanzania iko nafasi ya 22 katika International Cricket Confederation (ICC) ranking, inayojumuisha nchi zaidi ya 120.
Timu ya taifa ya mchezo wa Cricket ya Tanzania itatembelea Uingereza ikiwa safarini kwenda Italy kwa mashindano ya kimataifa ya daraja la nne ya mchezo huo (ICC Division IV) Timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo huo inatarajiwa kuwasili hapa Uingereza Ijumaa ijayo (30 Julai 2010) kwa ziara ya michezo ya kirafiki ya wiki moja na mazoezi zaidi kwa mwaliko wa Klabu ya Watford Cricket (WTCC), nje kidogo ya Jiji la London.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2010

    Kwa nyongeza wachezaji hao wa criketi toka Tanzania ktk timu hiyo ya Watford ni wachezaji wa kulipwa, yaani professional players.
    Hongereni kwa kuwakilisha, tupo pamoja.
    Mdau
    Ukerewe.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2010

    Mfano mzuri vijana wetu, pongezi sana.

    Nadhani hata msimbazi watabadilika walipokataa sponsorship toka marekani eti t-shirt ya Simba USDollar 40 litakuwa ghali sana kwa wapenzi!( wapenzi 100,000 tu mara Tshs 60,000 zingeingia Tshs. Billioni 6), wangesaini mkataba mzuri klabu ingeweza kuondoka na billioni 4.
    Mdau
    Jangwani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...