
Marehemu Mzee JOHN STEVEN MUSHI aka MZEE MIWANI
Ni mwaka mmoja umepita tangu baba yetu mpenzi umetutoka.Majonzi mengi umetuachia lakini kwa sababu ni kazi ya Mungu nasi hatuna budi kumshukuru kwa kila jambo. Baba, pamoja na kwamba haupo pamoja nasi kimwili, lakini upendo wako, busara zako, ucheshi wako, utoaji wako na malezi bora uliotupa bado vipo pamoja nasi na ndio maana hatutakusahau.
Tunaamini kwa mazuri uliyoyafanya sio kwetu sisi tu bali na kwa watu wengine wengi; huko ulipo Mungu amekupumzisha mahali palipo pema zaidi. Baba haukupenda kuona mtu anateseka, ulikuwa tayari kuteseka ili familia yako tunufaike.
Ulitufundisha kuwa elimu ni silaha muhimu sana ambayo mtu hataweza kukunyang'anya: bali itakuwa nawe siku zote. Unakumbukwa sana na mke wako mpenzi Martha John Steven MUSHI, watoto wako Penda, Dr Kunda, Dr Cleopa, Shanande, Ufoo na FranciaWajukuu wako wanaokupenda sana na kuyafaidi matunda mema uliowaachia wazazi wao, Catherine, Ngapani Jr, Michael, Rodney, Mcshield, Moshe, Alinda, Sia na Doreen.
Kutakuwa na ibada ya shukrani itakayofanyika anapokaa mjane wa marehemu
REGENT ESTATE, 236 UKOMBOZI STREET tarehe 29/July saa 11 jioni.
Tunamkumbuka sana mzee mushi, mhangaikaji na mtafutaji sana, kapumzike mzee. Poleni sana wakina doc Kunda
ReplyDeleteMzee wa watu RIP
ReplyDeleteRIP mzee Miwani, tunakukumbuka
ReplyDeleteHuyu mzee kafariki lini tena? namfahamu tokea akiwa meneja wa mamlaka ya pamba, poleni sana wanafamilia
ReplyDeleteMaleo
Babu mzee wa Range mererani tunamkumbuka sana tokea ameondoka vijana wako wamesambaratika sana. Mungu akuleza pema peponi
ReplyDeletePenda,Kunda,familia ya mushi poleni sana
ReplyDeleteMzee Mushi jamani,Mungu akulaze pema peponi. Tunakukumbuka sana na machine za kusaga pale Mwananyamala. RIP
ReplyDeleteMzee Mushi unakumbukwa sana pia na wanaregent wote na majirani wote mwenyezi mungu aistiri roho yako pahali pema panapostahili ,upo kwenye sala na maombi yetu ya kila siku RIP
ReplyDeleteMungu akupe furaha, pumziko na amani ya milele mzee, umesaidia watu wengi Mungu ndiye ayajua. mcheshi mpenda watu na mtoaji asiye kinyongo na mtu, hatutakusahau mzee mushi poleni sana
ReplyDelete