Ndugu Wazalendo nchini Uholanzi,
Mnakaribishwa kuhudhuria na kushiriki kutoa michango ya mawazo yenu katika kipindi cha Television (Star TV) kitakachorekodiwa hapa Uholanzi na kurushwa Tanzania katika kipindi cha kila wiki kinachojulikana kwa jina la Mayrose TV Talk Show. Kwa habari zaidi zuru:

www.mayrosetalkshow.hostoi.com
TV Talk Show hii itafanyika katika ukumbi wa Cultuur Centrum, Helftheuvelpassage 38, 5224 AP. Den Bosch saa 9.00 alasiri (15.00hrs) siku ya Jumapili tarehe 11/07/2010.
Tutajadili mada tatu:
i) Imeonekana kwamba tafiti nyingi zilizopo Tanzania hazijafanyiwa kazi ipasavyo katika kusaidia maendeleo ya nchi yetu, nini kifanyike?
ii) Mchango wa Watanzania walio nje ya nchi ni muhimu katika kusaidia maendeleo ya nchi. Ni vipi unatambulika na kutumika?
iii) Katika mchakato wa kuboresha au kuanzisha miradi mbalimbali, ni changamoto gani tunazopata katika mahusiano na wabia au mashirika ya nje? Nini kifanyike?
Tafadhali sana zingatia muda kwani tutaanza kurekodi saa 10 kamili jioni na tukianza hakutakiwi mwingiliano wa mambo.
Karibu ushiriki kwa ukamilifu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu Tanzania.
Tafadhali sana thibitisha (confirm) kabla ya tarehe 08/07/2010 kwa ajili ya maandalizi .
KIINGILIO NI EURO 5
USIKOSE!

Kwa kujiandikisha kushiriki tuma jina lako kwa:
Mayrose Kavura Majinge,
Email: mayrosekm@gmail.com
au tuma sms au piga simu namba 0685093826.
Mayrose uko juu dada, kaza buti, show zako tunazikubali na tunasubiri kusikia mawazo ya Watz wa Udachini.
ReplyDeleteDada mara hii uko Uholanzi tena? Mi naonaga tangazo lako kwenye mazingira ya kibongobongo nikajua unafanyia shughuli bongo.
ReplyDeleteKumbe na wewe umekuwa kama Sporah.