Katibu Mkuu wa Mchezo wa Pool Taifa (TAPA),Amos Kafwinga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mchezo wa Pool unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho katika mikoa ya Kagera, Morogoro, Temeke, Ilala na Kinondoni.kulia ni Innocent Melleck wa Intergrated.


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager ambayo ni mdhamini mkuu wa mashindano ya Pool yajulikanayo kwa jina la Safari Lager pool national championship leo imetangaza rasmi kuanza kwa mashindano ya Safari Lager National Pool Championship- 2010 kwa ngazi za mikoa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Meneja wa Bia ya Safari lager Fimbo Buttallah alisema mashindano hayo kwa mwaka huu yanatarajia kuanza kutimua vumbi tarehe 22.07.2010 mpaka tarehe 08.08.2010 na fainali za kitaifa zitafanyika katika jiji la ARUSHA kuanzia tarehe 15.09.2010 mpaka 19.09.2010.

Akizungumzia udhamini wa mashindano ya mwaka huu, bwana Butallah alisema “Bia ya Safari lager imekuwa mdhamini mkuu wa mchezo wa Pool hapa nchini, na imeweza kuleta mapinduzi ya kweli katika mchezo huu, hivyo ni dhamira ya bia ya Safari kuendelea kudhamini mashindano hayo.

Alisema maandalizi kwaajili ya mashindano hayo yamekalika ikiwa ni pamoja na malipo kwa chama cha mchezo huo nchini TAPA na pia vifaa vyote vimeshakabidhiwa hivyo kinachosubiriwa ni kuanza tu kwa mashindano hayo.

Bwana Buttah aliwataka wapenzi wa mchezo huo na wapenda michezo kote nchini kuhudhuria kwa wingi ili kupata wasaa wa kushuhudia namna mchezo huo unavyokuwa kwa kasi.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama cha Pool Taifa Bw. Amos Kafwinga alisema,

Mashindano katika ngazi ya mikoa yatafanyika kama ifuatavyo:
Tarehe 22.07.2010 mpaka 25.08.2010 ni mikoa ya Kagera, Morogoro, Temeke, Ilala na Kinondoni.julay 29,2010 hadi Aug 01,2010 mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Dodoma,Iringa ,Temeke na Shinyanga nazi zitafanya fainali zake katika ngazi ya mikoa.

Aidha bwana Amos alisema mikoa ya Manyara,Mwanza ,Arusha ,Mbeya na Ilala inatarajiwa kufanya fainali zake kati ya Aug5,2010 na Aug 08,2010.

Katika ngazi ya mikoa mashindano yataendeshwa kwa club na hatimae Mikoa yote itaunda timu zao za mikoa ambazo zitawakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa zitakazofanyika Mkoani Arusha mwishoni mwa mwezi wa Septemba.

Aidha Bwana Kafwinga aliishukuru bia ya Safari Lager kwa juhudi zake za kuuendeleza mchezo huo nchini “Taswira ya mchezo wa pool hapa nchini imebadilika kwa kiasi kikubwa na sasa inwavutia vijana wa rika mbalimbali kwani si mchezo wa kupotezea muda tena kama Wengi walivyoudhania, bali ni miongoni mwa michezo inayokua kwa kasi kubwa na kuwapatia kipato wachezaji na vijana kwa ujumla.

Ningependa kutoka shukrani za kipekee kwa Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa kuweza kuleta mapinduzi haya makubwa katika mchezo wa Pool hapa nchini. Ni dhahiri kuwa mchango wa mdhamini ndio umeleta matunda yote haya ambayo tunayaona hii leo TAPA inaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri na mdhamini kwa kusimamia na kuendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2010

    Hivi "Pool Table" ni mchezo gani? Pool naijua, na unacheza kwenye meza. Watu tubadilike na kutumia terms ipasavyo, jamani, ah!

    Vilevile, kwa mastaa wetu wa film za kibongo (Bongowood?) Hivi kwa nini Vincent Kigosi mpaka leo anaitwa "Ray" hata kwenye matangazo na habari za sinema zingine? Na yule "Cloud" vilevile. Haya majina ni kwamba waliact sinema fulani wakatumia majina hayo - sasa sinema imekwisha toka, imepita, move on, khaaa!! Sijawahi kuona leo hii Sylvester Stalone akiitwa "John Rambo" kwenye sinema ingine au habari zake zingine! Sasa iweje sisi tunang'ang'ania majida ya characters wa mwaka 47!

    Tubadilike, jamani, tubadilike!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...