Afrika Ikulu jijini Dar siku JK alipoapishwa rasmi mwaka 2005
Muadhama Kardinali Pengo na viongozi wa kanisa katoliki kwanye hafla ya kanisa hilo


UMUHIMU MKUBWA WA MZEE MWINYI KATIKA NCHI YETU
Ankal naomba uniweke katika globu yako ili walibeneke wengine waweze kuchangia hoja yangu kwamba raisi wetu wa pili alikuwa na umuhimu mkubwa na ni kiongozi pekee wa kuigwa pale nchini kwetu kama kumbukumbu zangu ni mzuri ni kiongozi pekee mpaka sasa aliyeweza kujiondoa katika uwaziri wakati wa mauwaji ya watu wazima bibi zetu kule shinyanga kwa kizingizio cha heti wachawi.
Hicho kitendo kilimuudhi sana mzee mwinyi na kuachia uwaziri wa mambo ya ndani .Leo hii waziri mkuu anajihusisha na kuwaingiza wananchi katika mikataba ya uongo ya umeme na anakuwa mbishi hata kuondoka katika nafasi yake.
Na mpaka leo hakuna kiongozi yoyote aliyejiondoa katika uongozi wake mwenyewe bila ya kusukumwa na wananchi au wabunge
Vilelvile Ally Hassan mwinyi ni kiongozi pekee aliyeona maumivu ya ujamaa kwa wananchi watanzania na kuamua kufungua milango ya biashara kwa watanzania ili waweze kujikomboa katika umaskini.
Vilelvile Ally Hassan mwinyi ni kiongozi pekee aliyeona maumivu ya ujamaa kwa wananchi watanzania na kuamua kufungua milango ya biashara kwa watanzania ili waweze kujikomboa katika umaskini.
Mzee mwinyi huku akisemwa na baadhi ya viongozi kwamba anashauriwa na mkewe, aliweka hayo maneno kando na akaendelea kumkomboa mtanzania aliyekuwa katika kifungo cha ujamaa kwa miaka mingi sana.
Ni kweli kwamba baadhi ya watu wasiokuwa na akili walitumia kipindi kile cha biashara huria kujinufaisha lakini hicho ni kitu ambacho mtu mweusi kazaliwa nacho lakini mzee mwinyi alikuwa na lengo zuri kabisa kumkomboa mwananchi mtanzania.
Katika uongozi wake mzee mwinyi alikuwa ni kiongozi pekee hata kujua kwamba kumbe mashirika mengi ya serikali yalikuwa yanawatia gharama serikali tu kwani kulikuwa hakuna kitu kilichokuwa kinafanyika serikalini ,mashirika ya NMC na NDL sijui yalikuwa yanafanya kazi gani ,vyama vya ushirika sijui vilikuwa na shughuli gani .kwa kweli kulikuwa na maumivu tu kwa wananchi lakini yeye alikuja kuguindua hayo na kufuta mara moja
Nilikuwa hata mimi najiuliza umaana wa kutumia kodi za wananchi katika ukombozi wa nchi kama AFRICA YA KUSINI,ZIMBABWE,MSU

Ankal kwa mimi naona MZEE ALLY HASSAN MWINYI NI KIONGOZI PEKEE KATIKA NCHI ILE AMBAYE HATOSAHAULIKA KABISA
MDAU UNITED KINGOM
MDAU UNITED KINGOM
Ankal hiyo title imekaa vibaya sana...kumkumbuka mtu ni kama ameshaukata vile sasa unamkumbuka...Kama ungeibadili hata kusema kitu kingine tu...Imenikata maini sana...Nilizania nimemiss post zingine zilizoonyesha kuwa huyu keshatangulia...please hebu change tu kukumbuka mtu bado yupo hai you don't say that...
ReplyDeleteHatutamsahau. Alimaliza adha ya foleni za kununua unga, sabuni, chumvi, mafuta, n.k. Enzi yake watanzania wa bara wazawa tuliona TV, friji, n.k. na kujenga nyumba za kisasa kwa mara ya kwanza. Aliruhusu vyombo vya habari huria, watu wa kawaida kuwa na passport, alimaliza ule mtindo wa kuwatia watu kizuizini bila mashtaka, neema ya chakula ilienea, aliwacha strategic grain reserve ikiwa imejaa vyakula mpaka watu wakashindwa kujua vyakula vyote hivyo viwe-stored wapi.Alitukomboa WA-TZ. Hata maadui wake leo wametahayari kuona kwa huyu mzee na familia yake wanaishi maisha ambayo si ya kifahari na ni mtu anyependwa kila kona ya nchi hii. Nimemuona mwaka jana katika hafla moja ya DSM naona bado yuko "fit" sana kimwili na kiakili licha ya kuwa ana miaka 85. Namwomba Muumba ampe mzee wetu A. H. Mwinyi kila la heri. Sosthenes.
ReplyDeleteMZEE A.H.MWINYI ni shujaa wa maisha mapya kwa mtanzania,,,,,hadi leo mnawapata watu kama akina Hasheem Thabit wanacheza Basket ulaya,,,,enzi zile za....walikuwepo wazuri katika michezo lakini nani na wapi wangeonwa.....? leo mtoto amefanya vituko siku ya mechi ya Tanzania na Brazil,,dunia nzima imemuona hadi anafuatwa na wanahabari mbalimbali hadi kaalikwa redio clouds nk,lakini sisi tulifanaya vituko enzi hizo nani alituona....? tuliishia kuchapwa na kuitwa watoto watukutu hatukupongezwa kwa utundu kama wa mtoto wa mechi ya brazil....tulikuwa hatujakombolewa. Hongera baba mzee ruksa MUNGU AKULINDE AKUPE AFYA NJEMA ILI MAADUI ZAKO WAJIONEE WENYEWE ULICHOKIFANYA NDANI YA MATUSI NA KASHIFA,,leo ndo wanafaidi matunda yako,,Hureeeeeee uko juu mzee..nitakuheshimu daima. wapingaji na wabishi walikuwepo tangu Enzi ya YESU hadi akaja mtume MOHAMED bado wanaendelea tu.
ReplyDeleteKUWA UK SI TITLE YA KUWA NA AKILI NZURI,UFAHAMU NA FIKRA PEVU FREEDOM OF SPEKING NANDI MANA BALOZI WA TGT AMEWEKA MADA YAKO ICHAMBULIWE,MWINYI NIKIONGOZI ANAEONGAZA KUPENDWA MPAKA SASA NA LA ZAIDI UCHESHI NA BASHASHA MUNGU ALIOMJALIA.MWINYI NIO BINADAMU KAMA SISI ANA KASORO ZAKE.MWINYI ALIUWA AZIMIO LA ARUSHA NA KULETA AZIMIO LA ZANZIBAR,BILA KUTANGAZIA DUNIA KWAMBA CCM SASA INAFUATA SIASA ZA KIBEPARI(KOSA)NA MPAKA LEO CCM HAITAKI KULITAMKA HILO NA NDIO MAANA KUNA MSUGUANO NDANI YA CHAMA,NDANI CCM KUNA WATU WENYE NGUVU NA WANAMINI KATIKA SIASA ZA UJAMAA NDIO MKOMBOZI WA WANANCHI WAKAWAIDA(WAKO SAWA),MWINYI NDIO ALIE RUHUSU KIONGOZI KUFANYA BIASHA AKIWA KIONGOZI(MAFISADI NDIO WALIPO ZALIWA).MFANO TENDA YA KUPAKUWA MAKONTENA BANDARINI DAR ILITANGAZWA KATIKA GAZETI LA SERIKARI,KUNA WATU BINAFSI NA WENYE UWEZO(WATALAMU)WA KUFANYA KAZI HIYO,MAKAMPUNI YA UHAKIKA KUTOKA NJE YAKIWA NA WABIA WAZAWA WALIKOSA TENDA IKAPEWA KAMPUNI YA WAZIRI,KWAKUWA NI RAHISI WAZIRI KUMUHONGA CHEO MGAWA TENDA AU KUMTIMUA KATIKA NAFASI YAKE KAMA HAKUBALIANI NAO MAANA WAKOWENGI KWENYE LINE.SWALA LA UKOMBOZI WA NCHI ZA AFRIKA NDIO USISEME NA MISTARI YAKO HIYO NIMEPIMA UFAHAMU NA ULEWA WAKO NI DUNI KASI GANI KUNAVITU VINGINE SIO MPAKA UCHANGIE.TANZANIA ISENGEKUWA SALMA KA AFRIKA NZIMA HIJAKUWA HURU KAA NAWAZO YAKO MGADO.
ReplyDeleteNi fahari kuona kuwa kuna watanzania wachache kama wewe unayeweza kukumbuka haya. Wengi wamejaa lawama na kukosa shukrani! Nyerere alicheza vyema karata yake 1985. Lakini 1995 Mh!!
ReplyDeleteNawaomba marais wastaafu wetu kuendeleza kuijenga nchi yetu baada ya kutoka madarkani, kwani inaonekana hakuna kitu kinachosikika kwa Mheshimiwa Mwinyi ambacho kinamuweka kwenye goodoutstanding. Mapesa wanapata mengi, so anzisheni NGO'S LIKE BILL CLINTON, jiwekeni active, clreate New Jobs kwenye NGO'S zenu na mtakumbukwa daima. MWINY FOUNDATION WHERE IT IS!!!!! I BELIEVE MKAPA HAS ONE, MWL.NYERERE HAS ONE, MAYBE KIKWETE WILL HAVE ONE!!
ReplyDeleteMzee Ruksa alipokuwa madarakani na mara baada ya kuondoka tu madarakani yalisemwa mengi kama kujilimbikizia mali, kuhodhi mali nyingi na majengo mengi na hata wabaya kudiriki kumsukuma Mkapa amchukulie hatua, lakini makapa kasema si papo kwa papo na mambo yakaisha.
ReplyDeleteCha msingi ninachojifunza hapa kiongozi ukiwa madarakani ni jungu kuu hutakosa ukoko hata wa kupakwa. Mazuri yote hayaonwi ila tu kupakwa matope na mapungufu ambayo hayakwepeki kibinadamu na binadamu ye yote ndo huwa kitambulisho cha mtu au kiongozi.
Nashangaa kuona mzee Ruksa akiishi maisha ya kawaida tu sasa mali alizoambiwa kajilimbikizia zimeishia wapi?
Tunakumbuka Mkapa alipotoka madarakani alivyorushiwa madongo mazitomazito na kama si busara ya Rais Kikwete angerushiwa kombora la scud na wenye midomo mirefu. Lakini leo tunaanza kuona matunda aliyofanya Mkapa na kumuasi kikwete angetulia na kujifunza baadhi ya mafanikio ya Mkapa kama ukusanyaji wa kodi badala ya kutegemea wahisani watukwamue kimaendeleo na bajeti.
Watanzania tuwe watumiaji wa mizani kuona mema yaliyotendwa na viongozi wetu, na kuwaona ni binadamu ambao katu mapungufu hayawezi kwepeka.
Tunabahati historia ya viongozi wetu wote wasifu nzuri kitaifa na kimataifa, ni jambo la kujivunia na kila mmoja wao ana mazuri mengi tu aliyolifanyia taifa. Kila kiongozi alitengeneza mazingira ya kiongozi mwenzake kurahisisha utendaji. Kwani mazingira ya awali mfumo wa ujamaa ulitujenga watanzania utamaduni wa taifa moja lenye kufuta mnuko wa ukabila, kazi ya Mzee ruksa ikawa imerahisishwa kujenga uchumi, na Mkapa kawa mwongozaji katika kujenga uchumi wa kujitegemea, ya Kikwete tusubiri muda wake uishe ndo tutamwainisha vizuri.
Alamsiki watanzania wenzangu.
"TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE"
lakini hili suala la kurekebisha uchumi aliyeanza kupiga kelele si Edwin Mtei akaishia kufukuzwa kazi. badala yake akateuliwa Amiri Jamal ambaye alikuwa anasuasaua kuleta mabadiliko. baadaye aliteuliwa Cleopa Msuya ambaye alisisitiza msimamo uleule aliokuwa nao Mtei. matokeo yake ni kuchukiwa na kufanyiwa kila aina ya fitina na wahafidhina wa CCM. ukweli ni kwamba, Mwinyi aliwaweka karibu wale waliotaka mabadiliko ya kiuchumi, na kuwaondoa wahafidhina wa siasa na sera zilizofeli. mashujaa wa kweli wa harakati za kurekebisha uchumi hawapewi sifa wanayostahili.
ReplyDeleteMzee Ruksa alifanyakazi nzuri sana wakati wa uongozi wake japo alikorofishana na baba wa Taifa JKN kuhusu uongozi wake akidai nchi inaongozwa na mwananmke wakati huo. Mimi naamini, wakipambanishwa leo, Mwinyi, Mkapa na JK, Mwinyi atachukua nchi. Watanzania hawapendi kusikia longolongo ya uchumi unakua!! wakati watu hawana hata thumni mfukoni. Wakati wa Mwinyi maisha yalikuwa tanbarare, watu waliacha kazi za kuajiriwa wakawa wafanyabiashara. watu walikuwa wakipanga cret za bia baa kwa kimo chao, wasijue maisha ni kupanda na kushuka. Kwakweli mzee Ruksa alikuwa safi sana. Mabasi ya mikoani yalianzia kwake, angalau tulianza kutumia usafiri wa mabasi badala ya treni nk. E bwana, ntaongea mengi. Ukiachia kasoro hizo za azimio la arusha sijui, ambalo bado naona lisingetusaidia sana wakati huu maana lilikuwepo miaka mingi hakukuwa na maisha bora. kama noma na iwe noma lakini Mwinyi alikuwa saaaaaaaaaaafiiiiii
ReplyDeleteMDAU WA UNITED KINGDOM NAONA AKILI ZAKO NI FUPI SANA NA MWEUPE WA MASWALA HAYA NA MUELEWA YA MAMBO YA WATU YA MITAANI YA BILA KUYACHABUA KIUNDANI. MWINYI HAKUJIUDHURU KWA HIARI YAKE PALE MAMBO YA MAUAJI YA VIKONGWE YALIPOTOKEA KULE SHINYANGA, ALIOMBWA AACHIE NGAZI, THE SAME KWA LOWASSA HAKUJIUDHURU KWA HIARI YAKE ILE ALIOMBWA AACHIE NGAZI AND THE SAME KWA MSABAHA NA YULE WAZIRI MWINGINE. KWA USTAARABU NA ITIFAKI YA SERIKALI YOYOTE ILE HAIWEZI KUSEMA TUMEMUOMBA FULANI AACHIE NGAZI KWANI KUFANYA HIVYO NI KWENDA KINYUME NA ITIKADI YA COLLECTIVE RESPONSIBILTY KWANI KAMA NI KUJIUDHURU YEYE KAMA WAZIRI PIA ANAWEZA KUDAI NA RAIS NAYE AJIUDHURU KWANI WAKATI MAMBO YANAARIBIKI HAKUYAONA KWANI WAZIRI KACHAGULIWA NA NANI SI YEYE RAIS, KWA MAANA HIYO ALICHAGUWA WAZIRI MBOVU, THE SAME ILIVYOTOKEA KWA MKUU WA MAJESHI YA AMERIKA NA NATO KULE AFAGHANISTAN ALIJIUDHURU MAJUZI TU NA RAIS KUSEMA ANASHUKURU KWA KUJIUDHURU KWAKE KWA SHINGO UPANDE UKWELI ALIMUAMBA AONDOKE BAADA YA INTERVIEW YAKE NA GAZETI LA ROLLING STONE. KUHUSU UKOMBOZI WA AFRICA NAONA HAPO NDO UMEPOTEA KABISA KWA VILE HUELEWI CHOCHOTE JUU YA INTERNATIONAL PILICS/COOPERATION KWA MAANA HIYO BASI KUSINGEKUWA NA HAJA YA KUWA NA UN NA SISI KUWA WANACHAMA TUNAOLIPIA ADA KUBWA KILA MWAKA PESA AMBAZO ZINGETUSAIDIA KATIKA MAENDELEO YETU YA WANANCHI. PIA MWINYI HAKUFUNGUWA BIASHARA OPEN KWA MATAKWA YAKE BALI PRESSURE FROM IMF NA WORLD BANK NA NCHI ZA KIBEPARI NA MASHIRIKA MAKUBWA YA BIASHARA YA KIBEPARI YA NCHI ZA ULAYA MAGHARIBI, HATA HIVYO PROCESS ILIANZA TOKA KWA MZEE NYERERE NI IMF NA WORLD BANK ILIYOSHINIKIZA TANZANIA KUFUNGUWA BIASHARA OPEN KWA KUWEKA MASHARITI MAGUMU KWA MFANO KAMA TANZANIA INGEKATAA ISINGEPEWA MIKOPO NA MISAADA TOKA IMF, WORLD BANK NA NCHI WANACHAMA WA WORLD BANK KAMA UK, CANADA NA U.S.A AMBAO NDO WAFADHILI WAKUBWA WA TANZANIA NA WORLD BANK NA IMF. HATA KWENYE BAJETI YA SERIKALI YEU ASILIMIA KUBWA NI KUTOKA KWA WAKUBWA HAWA. KUHUSU MASHIRIKA YA UMMA HAKUKUWA NA UBAYA WOWOTE WA KUWA NA MASHIRIKA YA UMMA TATIZO LILIKUWA NI WATENDAJI WETU WABOVU WALIYOYAFILISI HAYO MASHIRIKA KWA KUTOZINGATIA MIPAKA YA UONGOZI WAO WENGI WALITUMIA VIBAYA MALI ZA MASHIRIKA HAYO PAMOJA NA PESA WALIZIIBA SANA NA BAADHI YA MAMENEJA WA MASHIRIKA HAYO NA NDUGU ZAO NDIO MATAJIRI WAKUBWA LEO HII. CHINA UNAYOIONA LEO UNACHANJA MBUGA KUELEKEA KUWA NUMBER ONE WORLD ECONOMY IN THE WORLD MSINGI WAKE MKUBWA NI MASHIRIKA YA UMMA, ANYWAY THIS IS ANOTHER TOPIC NISIKUCHANGANYE SANA. NIMEKUPA UWAZI KIDOGO KWA LEO TU NAOMBA NIISHIE HAPA
ReplyDelete