Wachezaji wa timu ya Polisi Mbeya wakijifua kabla ya mchezo wao dhidi ya JKT Mbweni katika mchezo wa Klabu Bingwa wa Taifa wa Netiboli kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe jijini Dar
Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya Sifa Queen akimiriki mpira huku akizongwa na mlinzi wa timu ya Tamisemi, Hawa Luwa wakati wa mchezo wa ligi ya daraja la kwanza ya netiboli katika mchezo uliofanyika leo kwenye viwanja vya TCC, Chang’ombe Dar es Salaam ambapo mchezo kati ya timu hizi bado unaendelea hadi mwandishi wa Globu ya Jamii anaondoka uwanjani Tamisemi walikuwa wanaongoza kwa magoli 15-3

Mshambuliaji wa timu ya JKT Mbweni, Nell Anyingisye akimtoka Hilda Mpepo ktika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliofanyika leo kwenye viwanja vya TTC, Chang’ombe, Dar es Salaam.JKT Mbweni imeibuka kidedea kwa kuifunga Polisi Mbeya kwa magoli 47-19.
Mfungaji wa timu ya JKT Mbweni, Mwanaid Hassani akiifungia timu yake moja ya magoli yaliyoipatia ushindi timu yake dhidi ya Polisi Mbeya ambapo JKT iliibuka na ushindi wa magoli 47-19. Kwa matokeo ya leo Polisi Mbeya wanazidi kujiweka katika nafasi mbaya baada ya kupoteza mchezo wa pili ambapo katika mchezo wa jana ilikubali kipigo kutoka kwa maafande wenzao wa Mwanza kwa kufungwa magoli 26-22



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...