Picha na Habari na Woinde Shizza,
Arusha.
Shindano la Miss Tanzania kanda ya kaskazini linatarajiwa kufanyika ijumaa Julai 26, 2010 katika hoteli ya kitalii ya Naura Springs, mjini Arusha katika ukumbi wa hoteli ya kitalii ya Naura Springs.
Warembo kumi na mbili kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga watapanda jukwaani kuwania taji la umalkia wa kanda ya kaskazini, taji linaloshikiliwa nae Susan Emmanuel aliyetwaa taji hilo akiuwakilisha mkoa wa Arusha.
Sambamba na malkia wa kanda ya kaskazini pia watapatikana washindi wengine wawili watakaojipatia tiketi ya kuingia katika kambi ya Miss Tanzania baadae mwezi Agosti.

Mkurugenzi wa Miss Northern Zone Erasto Jones toka kampuni ya Crown International Entertainment inayoandaa shindano hilo amesema maandalizi ya shoo hiyo yanakwenda vizuri na kuwataka wapenzi wa tasnia ya Urembo kujitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kushuhudia burudani ya aina yake usiku huo.
Erasto amevitaja viingilio katika shindano hilo kuwa ni shilingi 30,000/= kwa viti vya VIP na shilingi 20,000 kwa viti vya kawaida na tayari tiketi zimeanza kuuzwa Naura Springs Hotel, Duka nguo la JJ Black, CET Garden pamoja na City Link Pentagon Hotel.
Upande wa burudani wasanii Marlaw, Peter Msechu toka Bss na kundi la wacheza shoo la Hot stone Boys toka Arusha ndio watakaounakshi usiku huo ndani ya Naura Springs Hotel.
Aidha Erasto amesema kuwa kutakuwa na surprise kibao kuanzia kwa wasanii, warembo washiriki pamoja na vitu vingine vipya vitakavyoonekana usiku huo ambavyo vyote ni katika kutia chachandu shindano hilo la aina yake mwaka huu.
Amewataja warembo watakaopanda jukwaani kuwa ni Zahar Suleiman (20), Loveness Mallya (20), Glory Mwanga (19) na Zakhia Twahir (20) toka Arusha, Prisca Mkonyi (19), Yacoba Assenga (23) na Lorraine Premsingh (22) toka Kilimanjaro.
Mkoa wa Manyara utawakilishwa nae Paulina William (19) na Rachel Elia (19) wakati Tanga watawakilishwa nao Zulekha Mrisho (20), Thally Moray (19) na Anna Kiwambo (19).
Wadhamini waliowezesha Miss Northern Zone 2010 ni pamoja na Vodacom, Tanzanite One, Redds Original, Naura Springs Hotel, PSI, Chuo cha Taifa cha Utalii – Kampasi ya Arusha, Sky Print, Clouds Fm na Editions Senzia Fashions.
Wengine ni City Link Hotel, Artful Studio, Supreme Power Fence, Alliance Françoise na Duka la Nguo la JJ Black.
Mara Miss Kinondoni, Ilala, Tanga, sijui na "fotojeniki", Utalii...hizi Misses zimezidi!
ReplyDeleteMwishowe, tutakuwa Miss Makengeza!
Itabidi tuanzishe Miss Michuzi sasa
ReplyDeleteAnkal naungana na wengine kuleta kilio kwamba upunguze headline za mashindano ya ulimbwende, humalizi wiki bila kuona sijui mashindano ya miss so and so! Naelewa pengine wanakulipa ama unawapromoti free lakini wanaonekana kutawala wingi wa habari kwenye Blog ya jamii. Kwa mtu mgeni anaetembelea hapa anapata picha kwamba Bongo tumekazania zaidi katika fasheni shoo na ulimbwende.
ReplyDelete