Re:Right to Information Vs Right to Privacy
Salaam za Heshima nyingi Kwako na Wadau wote. Wadau kuna hili suala la blogging pamoja na networking sites ambapo mtu anapiga picha kisha kuziweka kwenye blog yake ambayo wewe huijui wala huambiwi kuwa hiyo picha itaning'inizwa mtandaoni.
Ama mtu yuko club (ama kwenye masherehe) hachezi mziki ila kazi kupiga picha kisha kuzining'iza kwenye SuraKitabu kama picha zake za ukutani wakati sura yake haipo kwenye hata picha moja. Naomba kujua kama ninahaki ya picha zangu kutowekwa mtandaoni bila ruhusa yangu.
Mdau Mkereketwa wa blog ya Jamii.
Nadhani ni utaratibu wetu
kuweka majina na email kapuni.
Mdau Mimi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2010

    Ukiwa kwenye public place yeyote mtu yeyote anaweza kukupiga picha ila iwapo upo kwenye private place hamna mtu mwenye ruhusa ya kukupiga picha bila ridhaa yako. Ni ustaarabu kuomba ruhusa kupiga au kutumia picha ya mtu yeyote.

    Mfano: Iwapo mpo kwenye ibada na picha ikapigwa na watu mkawa wengi.... hii picha inaonyesha kwa ujumla watu wapo wanaabudu. Ila iwapo ukapigwa picha peke yako na upo ibadani na bila ridhaa yako picha ikatumiwa kwa namna ambayo haiendani na mazingira ya picha, si ustaarabu na una haki ya kumshitaki mpiga picha. [nchi za watu sijui TZ]

    Kwa ufupi privacy is very expensive, mdau itakubidi uende kwenye exclusive clubs ambazo hairuhusiwi kupiga picha na kuna hefty fines kupiga picha [kila club member anafahamu hilo] na kingine unachoweza kufanya ni usitembelee public places au ukiona wapigwa picha kataa.

    Pole sana.
    * Mimi si mwanasheria ila napenda kupiga picha. Na huwa nazingatia nilichoandika hapo juu. Ni kawaida mtu akisema hapana {kwenye public places} huwa ninaheshimu uhuru wao na a thumb up I'll go ahead and take the picture.

    ReplyDelete
  2. kama hio picha imepigwa hadharani, una haki ya kumchukulia hatua za kisheria mpiga/mbandikaji wa picha hio, ingawapo yeye huitumia picha yako kwa manufaa ya kibiashara, kwa nia isiyo halali ama kwa nia ya kuiadhiri ama kuidhalilisha nafsi yako.

    Vinginevyo, una haki ya kumuomba mpiga/mbandikaji wa picha hio aishushe, watu wasiione. Ila yeye hana wajibu wa kutimiza ombi lako.


    Natumai nimesaidia kujibu swali lako.

    Chiziness

    ReplyDelete
  3. Mtoto wa CoastJuly 02, 2010

    Swali lako zuri ila linazua pia maswali mengine maana pia inategemea na utofauti katika hali au mazingira mfano:

    1. Je wewe ni 'public figure' au la?

    2. Hiyo blogu / sura- kitabu na au tovuti inamilikiwa na nani?

    3. Mlikuwa katika shughuli ya aina gani binafsi, kijamii, sikukuu ya kitaifa n.k

    4. Je, picha yako imewasilishwaje. Yaani je kuna dalili za kudhalilishwa au kukuonyesha kwa umma hakika usivyo? Yaani hapa tunaangalia sababu au kusudio la kuweka picha.

    A search for an optimal balance b/w right to information Vs right to privacy is in a Pandora box!

    Hii ni sawa pia na kutafuta uwiano kati ya SECURITY Vs PRIVACY katika suala zima la usajili wa lazima wa namba za simu na majina yake.

    ReplyDelete
  4. Mwaushe OhiwaJuly 02, 2010

    Ndugu kuhusu suala lako ni kweli unahaki ya faragha (privacy).

    Kwa kwetu hapa Tanzania privacy right iko katika Ibara ya 16 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.

    Ingawaje haki hiyo ipo kikatiba yapaswa kuwe na sheria maalumu ya Privacy na sheria hiyo kwa bahati mbaya haipo.

    Lakini hata hivyo kuhusu privacy right unaweza tembelea tovuti ya TCRA wao wameainisha haki za watu wanaotumia huduma za mawasiliano. Pia unaweza ripoti tatizo lako kwa TCRA consumer consultative council. Au unaweza ripoti polisi kama huyo mmiliki wa blog unamfahamu na unajua yuko wapi na anwani yake hasa hapa Tanzania.

    Kuhusu mkanganyiko wa haki ya faragha na haki ya kutoa na kupokea habari; ni kweli tatizo hili lipo na linatokana na ukweli kuwa Tanzania hakuna sheria maalum ya inayopambanua haki ya faradha na kuweka mipaka yake na haki zingine kama uhuru wa kutoa maoni au kutoa habari.

    Kuhusu suala la public place, si kweli kuwa kwenye public place kama bar au pub au klabu za usiku ndio mtu apigwe picha bila ridhaa yake. Haki ya faragha haishii chumbani ipo mpaka kwenye public places.

    Pia kuna mkanganyiko wa kuvunjwa kwa haki ya faradha na kudhalilishwa au defamation. Hivi ni vitu viwili tofauti. Na wala si kitu kimoja.

    Tuwe na utamaduni wa kusoma angalau katiba ya Tanzania

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2010

    loya mpiga picha umeongea vizuri ila sijajua kama waifahamu facebook! unaweza kuwa na sababu gani ya kupiga picha wadada walio club in a proper club attire halafu uliepiga picha ukaziweke kwenye facebook yako ilihali hao wadada si marafiki zako huko kwenye facebook ama unakablogu kako kasiko julikana na hao wadada.
    Nadhani kuwa mwanasheria tu haikufanyi wewe kuwa mtaalamu wa suala linaloongelewa hapa. Je ulisoma huko darasani?Tunaweza kuchukua uliyoyasema? Are you authority in Issues of Privacy?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...