Habari Kaka michuzi,
Naomba ushauri na ujuzi toka kwa wadau.kaka michuzi mimi nimeagiza toka japan.document zote za japan zinaonyesha gari ni ya mwaka 2001.lakini lilipofika bandarini darnaambiwa wadau(customs) wameikagua na kusema ni ya mwaka 2000.nilipouliza kigezonikaambiwa na agent wangu kuwa wameangalia mkanda(seat belt).
Je kaka michuzi nisaidienikujua ukweli,ni kigezo gani kinachoonyesha mwaka wa gari? je uko japan walivyoikagua walitumiakigezo gani?gari bado ipo bandarini natakiwa kulipia uchakavu.2.gari hilo nimeagiza kwa njia ya mtandao,na nina ushahidi wote kuanzia e-mail,invoice na copyya TT ya benki niliyotumia hela Japan.
Je kaka michuzi na wadau ni ushaidi gani tena unaoitajika?au wao TRA wanatumia kigezo gani kuniambia sijanunua bei hiyo?kama hawaamini kwaniniwasiwasiliane adress iliyopo kwenye document?naomba msaada kaka angu hasa kutoka kwawadau wa TRA na wadau wengine wote wazoefu wa haya mambo.wako mdau.F CN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2010

    Kaka pole,Mwaka unaoonekana hapo kwenye invoice yako ni year of first registation TRA wanaangalia year of Manufacture ambao unaandikwa kwenye seart bealt. Inawezekana year of firt regist ikafanana na yr of manuf. au zikatofautiana.Zinapo tofautiana ndo problems zinatokea

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2010

    Tatizo nchi yetu kila kona watu wasio kuwa na elimu ndio wamepewa nafasi ya kufanya maamuzi.

    sasa hawajui kwamba mikanda inaweza kutengenezwa wakati wowote tu na ikatumika kwenye gari la mwaka wowote.wametumia kigezo kipi kusema kwamba mikanda iliotengenezwa 2000,1999.... sio safe kama ya 2001.


    sheria za ajabu ajabu nyingi na ndiomaana nchi imeganda tu pale pale.baada kuweka inspection za maana kwa gari ya mwaka wowote ule wao wanaona kwamba gari ya mwaka 2005 au 2009 haitakuwa na matatizo kama ya 1999.wakati gari yoyote hile inweza kuwa salama kuwa barabarani kutokana na matatizo tofauti.gari 1999 inaweza kuwa salama zaidi kama ilikuwa inatuzwa vizuri na kufanyiwa matengenezo kuliko ya mwaka 2005 ambayo ilikuwa haituzwi na kufanyiwa matengezo.tatizo sio mwaka,tatizo ni je gari imekaguliwa kila kitu na kuhahakishwa ni salama kuwa barabarani?


    pole sana mdau ndio nchi yetu inayoongozwa na wajinga kupitia njia za rushwa. wewe sio wa kwanza kupata hio shida.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2010

    Kaangalie kama gari lako ni la mwaka 2000 kwenye mkanda. Kama ni hivyo itabidi tu ulipie uchakavu hakuna jinsi. Kuhusu kuongeza pesa ni kwamba TRA wana kamtindo ka ku-uplift (kuongeza) bei ya gari kulingana na wao wanavyopenda. Hapa ndo wanapoudhi. Kwani mtindo wao wa kuona kama mytu akinunua gari ni luxury, wakati mtu unataka kujikomboa kiuchumi kwa kuwezeshwa kwenda popote upendapo kwa haraka. kama wamekuongezea pesa na wewe unadocument zote HALALI kutoka huko uliko nunulia, waweza kukata rufaa ili upunguziwe bei kwa kuonesha TT na Invoice ulizoagizia gari kwa Kamishna wa TRA. Ila uwe mwangalifu unaweza ukaliacha gari lako muda mrefu bandarini na ukaanza kudaiwa storage charge. Utalia zaidi. nadhani nimekusaidia kwa kiasi fulani. Nawasilisha

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2010

    kitu cha muhumi ni kuchukua vile vitabu vya TRA kusoma mambo ya kodi na sheria zake ni bure kila mtu anapaswa kwenda kuchukua, ili sidanganywe na TRA.vitabu hivyo vina mwongozo.
    kumbuka usipojua sheria ndio watakupiga changa la macho wale wafanyakazi, lakini wakishtuka wewe unajua sheria, na ukawauliza ni kifungu kipi kimetumika utawakamata vizuri ni hayo tu kwa wale waagizaji wa magari na vitu vingine.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2010

    Nchi zilizoendelea gari hukaguliwa bila kujali mwaka iliyotengenezwa. Ikipass test inapewa registration.
    Hawa TRA wanaona bora uimport gari la mwaka 2010 lililokua writen off kuliko la mwaka 98 lililo fit.
    Kama gari imetengenezwa mwaka2000 mwezi wa 12 na ikaanza kutumika March 2001 nini tatizo?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2010

    NAKUMBUKA WAKATI SUMAYE AKIWA WAZIRI MKUU ALIAGIZA MAGARI YOTE YA ABIRIA YAFUNGE SEAT BELT SASA INA MAANA KILA MTU ALIKUWA ANAENDA MADUKANI KUCHAGUA MKANDA UNAONDANA NA MWAKA GARI LILIPOTENGENEZWA? AU LABDA HATA MIMI SIJAWAELEWA VEMA WADAU WALICHANGIA MADA HII.HAKUNA KIGEZO KINGINE KINACHOAMINIKA ZAIDI YA MKANDA?

    KUHUSU BEI YA GARI, NDUGU YANGU NAKUSHAURI TU ONGEA NA HAO JAMAA WA TRA KIUSHIKAJI WAKUPUNGUZIE HICHO WALICHOONGEZA THEN ULIPE FASTA MAANA HATA KAMA SHERIA UNAZIJUA WATAKUPIGA CHENGA NA KUKUPOTEZEA MUDA HADI UNAKUJA KULAMBWA KWENYE STORAGE CHARGE. HAKUNA SHERIA INAYOMTIA HATIANI TRA KWA KUCHELEWESHA MZIGO WA MTEJA BANDARINI. HILO NALO ULIJUE.

    HALAFU PILI, TRA NAO WANA "STANDARD COSTS" ZA AINA TOFAUTI TOFAUTI ZA MAGARI BILA KUJALI INVOICE YAKO ULIYONUNULIA. HAPA NDIPO ULIPO MRADI WA VIGOGO WA TRA KWANI KILA ANAWEKWA KUKAA KATIKA DAWATI HILI LA KU-UPLIFT, JIONI ANAAMBIWA AWASILISHE HESABU YA MGAWO WAO (MABOSI WAKE) NA WA SERIKALI

    TATU NA MWISHO, HUU NI MKAKATI WA MAKUSUDI NA WA SIRI WA KU-DISCOURAGE IMPORTATION OF PRIVATE CARS ILI KUPUNGUZA FOLENI MIJINI

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2010

    hizi vitabu hazipo TRA ,hazipo government printers wala hakuna kwenye site yao.

    waki angalia gearbox wange ku maliza.
    waki angalia alternata sijui wata semaje.pole sana

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2010

    TRA HAWAKATAZI WEWE KUINGIZA GARI YA MWAKA WOWOTE ULE. ILA HAPO WANACHOTAKA WAO NI KUKULIPISHA KODI KUBWA KWA MAANA GARI YOYOTE ILIYO NA MIAKA KUMI NA KUENDELEA UNALIPA KODI KUBWA. SASA WAO WANATAKA KUKUBANA HAPO ULIPE KODI KUBWA NA KWA KUFANYA HIVYO PIA WANATAKA RUSHWA TOKA KWAKO WANAJUWA UTAONGEA NAO WAKIKUPACHIKA KODI KUBWA HUO NDO MTINDO WAO NA WAKUU WAO WANAJUWA HIVYO LAKINI HAWACHUKUWI HATUWA YA KUWAKEMEA WATENDAJI WAO. KUHUSU MKANA NI KWAMBA SI KIGEZO CHA KUJUWA GARI ILITENGENEZWA LINI HUO NI UPOTOVU KABISA. HIVI WANAJUWA KUWA GARI HUWA LOTE HALITENGENEZWI KIWANDA KIMOJA! MIKANDA INATENGENEZWA NA KIWANDA KINGINE KABISA KWA MFANO KAMA NI TOYOTA HUWA WANANUNUWA MIKANDA TOKA KAMPUNI INGINE KABISA NA UKO UWEZEKANO WA KUNUNUWA MIKANDA YA GARI YA MWAKA HUU KWA MIKANDA YA MIAKA MITANO ILIYOPITA CHA KUANGALIA NA CHA MSINGI NI LOG BOOK YA GARI NDIYO INAONYESHA YEAR OF MAKE, TRA WAACHE HUU MCHEZO LAZIMA WAANDE NA WAKATI WANAWEZA HATA KUTUMA WATAALAMU WAO WAKAENDA JAPAN NI KUJIFUNZA MAMBO YANAENDAJI JUU YAMAGARI, MAGARI HUWA YAUNGANIASHWA PARTS FROM VIWANDA MBALI MBALI SI KIMOJA. HII KITU INATAKIWA IPIGIWE KELELE NA SERIKALI IJUWE NINI KINAENDELEA. KUNA HAJA GANI YA KUKADIRIA BEI WAKATI MTU MAKARATASI ANAYO NA KWA NINI IWE KWENYE MAGARI TU NA SI KWENYE BIDHAA ZINGINE? SIJAWAHI NIKASIKIA MTU KAAGIZA TV IKAFIKA TRA WAKAKADIRIA BEI, KWA NINI IWE GARI TU?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2010

    Mimi sijui hizo gari za Japan zinakuwa zinaandikwaje kwenye mikanda lakini hapa US kama gari imetengenezwa after June ya mwaka wowote wanahesabu hiyo gari ni ya following year mfano kama manuf. date ni 6/2000 hiyo gari inakuwa model ya 2001. Jaribu kuangalia na ikiwezekana tafuta vitabu vya TRA ili uone wanasemaje kuhusu hilo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 21, 2010

    Kila nchi na sheria yake

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 21, 2010

    Ndugu Pole kwa Matatizo hapa hamna cha Ushahidi Kaka hata kama Umeagiza kwenye Mtandao Japan pia Wajapani Ujue Ni Waongo si Kwamba wako Straight sana.
    Na Ukizingatia wewe ndye uliyetaka Gari La Mwaka 2001 lazima wangekuliza Kwa Stail hiyo.
    Pia Nadhani hukupata Agent aliye kuwa Makini
    Kuna jamaa wanaitwa
    www.dolphincargo.com hope wako makini sana koz waliwahi kunishauri wakati naagiza Gari.Kwa upande wa Bei Serikali yetu Haina mfumo Mzuri wa Kutoza Kodi just why mmnaweza kuwa watu 5 mmeagiza the Same Car but ushuru ukawa umetofautiana

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 21, 2010

    KWANI NINI MUHIMU UCHAKAVU AU UBORA?HUKU KWETU KWA NINI HATUNA YALE MAABARA YA KUKAGUA UBORA WA GARI KABLA HAYAJAINGIA BARABARANI?MIMI NINGEWASHAURI WAANGALIE KWENYE BODY KUNA ILE "STICKER" YA SILVER INAYOELEZA GARI IMEUNDWA LINI NA WAPI?SIO KUANGALIA MIKANDA,MAKOCHI NA VITAKA TAKA VINGINE VYA NDANI YA GARI HIVYO HUTENGENEZWA VIWANDA TOFAUTI MAKAMPUNI MENGINE YA MAGARI HUTENGENEZESHA VIFAA HIVYO NCHI TOFAUTI INATEGEMEA NA WAPI WAMEPATA BEI NAFUU,HATA UTENGENEZAJI WA NDEGE UKO HIVYO SASA IKIWA KAZI YENU NI KUSOMA LEBO ZA VITI, MIKANDA,USUKANI,MATAIRI,UPEPO UMEJAZWA WAPI NA RANGI IMEAGIZWA WAPI ITAKUWA KAZI NA HIYO GARI HUENDA MKAGUNDUA IMEUNDWA KWA MIAKA NANE KABLA HAIJATEMBEA HILO NALO MUWE TAYARI KULIJIBU MKIFIKA KUJIULIZA.
    HAO WEZI TU HAPO WANATAKA KUTAFUTA JINSI YA KUPATA HELA ZA KUNYWEA BIA SIO KUWA HAWAJUI HIYO GARI YAKO IMETENGENEZWA LINI.
    HUO MKANDA NDIO GIA YAO YA SIKU ZOTE WANAJUA INATATASHA KWA ASIE JUA AU MGENI NA MJI.
    MDAU.
    CANADA.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 21, 2010

    jamani tuwe wakeli kidogo. hakuna uhusiano wowote wa mikanda ya gari na umri wake. mimi naishi huku ulaya. magari yangu yote yana mikanda inayoonyesha mipya kuliko gari lenyewe. gari ni la 1993 na mikanda 1995. na gari nyingine ni ya mwaka 1998 na mikanda inaonyesha 1999. wakati huo huo rafiki yangu mikanda yake haifanani mmoja ni wa 1995 na mwingine 1997.

    TRA wanalazimisha pesa na wanataka kutumia kila liwezekanalo kufanikisha wanachotaka. ukiangalia chesis namba unaweza kujua gari lote. ni kuacha uvivu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 21, 2010

    Sasa document za gari zingekuwa zinaonyesha mwaka 1999 na mkanda mwaka 2001 ingekuwaje? Wangesema gari ni la mwaka gani?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 21, 2010

    Ndugu pole sana, mimi nakubaliana na sheria za TRA lakini utendaji wao ndio tatizo, kwa kesi yako maadamu gari ilishafika bandarini jua unakimbizana na muda, washakushika pabaya kwani ukichelewa utaanza kulipishwa storage ukizidi kuchelewa usishangae kukuta gari yako ina LOT number, lipa tu uchakavu, japo kitu kingine kinachonishangaza hapo ni kwanini ulipie uchakavu gari ya mwaka 2000 wakati halijazidi miaka kumi, maana nielewavyo mimi uchakavu huanza kutumika mwa gari la zaidi ya miaka kumi kwa maana kama ni c.c chini ya 2000 basi ushuru utakua ni(0.25+0.20+0.18)X CIF price. Hivyo utapata gharama halisi ya gari yako hadi inapotoka bandarini ukijumlisha kodi(0.25+0.20+0.18)xCIF na CIF price ie
    (( CIF price)+(0.25+0.20+0.18)xCIF))
    huku uhuru wa Bidhaa au uchakavu huo! ukiwa ni 20%, Forodha 25% VAT 18%. Sasa maadamu ihakua hivyo ndugu sauti yako ishafunikwa na mtungi. Bora Kenya wao wameamua moja tu hakuna kuingiza gari iliyozidi miaka 8!.
    Ushauri wa bure kwa wadau waagiza magari chukueni Profoma Invoice mapema ili mkadiliwe kodi mtakazolipa ili angalau kupunguza usumbufu na kujipa muda wa kujiandaa kwa kukadilia gharama za kununua gari hadi Tanzania na makadilio ya Kodi utakayo lipa ili ujue utatenga kiasi gani na uweke kiasi gani cha dharula.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 22, 2010

    wewe nfio mara yako ya kwanza kuingiza gari? hiyo ina maana kata kitu kidogo, nilileta benz ya mwaka 1995 nikakata ikaandikwa ni ya 2004. Acha mkno wa birika kaka utalikimbia gari

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 22, 2010

    The year of a car is determined by the body and not any parts of the car look on the door jam there is all information of the make, model and the year of the car also. Under the windshield there is the vin number of the car which determine the the year, model and the make here in the united state they have just a scanner which scan your bar code on the door jam and it will tell every thing about the car if not then the vin number will be used to do that
    TRA need to implement this system to determine the year and the model, make of the car the scanner is universal it can be used in any country and this will eliminate while lot of corruption and inconvenience the customer endure
    Also something need to be note here about the car manufacturing. Proccess the car maker buy a lot of parts from a third part company including the engine and the seat belt do there is good chance that the belt might be old than the car it self hence the start to make parts and then the body it self that's goes for the engine and the lights and so on only very few manufacture does their own engine for example BMW and Benz but the rest especially Toyota do buy from third part company
    Please michizi forward this to the minster who is responsible for TRA so he can do his own research and help this poor Tanzania to overcome this ignorance of not knowing what they are charging for
    The said scanner don't even cost $ 5000 each

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 22, 2010

    BONGO BWANA, KILA MTU ANAAMUA CHAKE. KWANINI WASIANGALIE MWAKA KWENYE BETRI YA GARI BASI AU KWENYE MATAIRI YA GARI........? MWAKA WA REG. INAMAANA NI WAKATI LIMEANZA KUTUMIKA MUDA HUO NA HATA KAMA UCHAKAVU WAKE UTAANZIA KUHESABIA HAPO. SASA UNATAKA KUSEMA GARI LINAWEZA KUCHAKAA LIKIWA LIMEKAA SHOWROOM JIPYA?? NDO MAANA NASEMAGA KUNA WATENDAJI HUKO WAHUSIKA HAWATUMII AKILI.
    KWELI BOGNO TAMBARARE! NA UKITOA HONGO TU MAMBO YOTE HAYO HAYATAFUATILIWA TENA.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 22, 2010

    huyo afisa wa TRA aliyefanya physical inspection na kuona mkanda umeandikwa year2000,alikua anajenga mazingira ya rushwa ili umpoze.Hakuna nchi inayotumia mkanda kama kielelezo cha mwaka wa gari.

    Kuna nchi zipo very strick katika mwaka wa gari,mfano Kenya na Mauritus,hawa wote huwa waanangalia first registration(month ,year)iliyoandikwa kwenye export certificate kwa magari yote yanayotoka Japan,hakuna mtu wa kuangalia mkanda wa gari.Huo ni wizi na elimu duni kwa watu wa TRA na hata clearing agents.

    Mnashindwa kukusanya kodi kutoka kwa hawa wahindi wakwepaji kodi,mnang'ang'ani used vehicles.Hii nchi bure kabisa.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 22, 2010

    pole sana..ata mie yalinikuta hiyo ya ku uplift..sasa basi niliongea na agent wangu vizuri nikampa kidogo dogo nae akaenda kuwapa TRA wakashusha bei ikawa kama ninachotakiwa kulipa..hawakua na muda na TT wala nini wakidai labda nililipia TT that amount thn nyingine nikaenda lipia hukohuko japan au kumtuma mtu..good enough nilianza kushuhurikia ushuru before gari alijafika by the time limefika nilikua nishampa hela agent akaenda klumalizana nao kama elfu 50 ivi mana niliona documents zote wanayosema gari limekua uplifted..hakuna chakufanya ndugu..
    hakikisha gari unatoa kwa muda unaotakiwa na hongo ikishindikana toa gari lako wanavyotaka wao once lipo nje ndowashtaki mana ni haki yako..nawakuelezee kwanini wamefanya walichofanya ila kikubwa soma kwanza vigezo vyao na kanuni na rules zote ndousimame kujitetea...hata wao wanaogopa wakiona mtu anajua sheria..ila toa gari kwana

    ReplyDelete
  21. Habari zenu, naomba kumsaidia huyu bwana utaratibu wa kukagua gari upo pale sehemu wanaiita WHRAF kule bandarini, na kitu wanachokagua ni kujua kama kile ulichoagiza na kilichoandikwa kwenye makaratasi yako ni sahihi, sio kwa magari tu ni kitu chochote kile ambacho unakiingiza nchini kinapaswa kukaguliwa na maofisa wa forodha, sasa kwa kesi hii wale watu wa TRA wanachokagua kwenye gari hasa ni mwaka husika, CC za gari na chasis number na model pia type ya gari, sasa kwa kesi ya mwaka kuwa tofauti hata kama ungekuwa umeagiza gari ya mwaka 2001 na ikasomeka 2003 bado ungetakiwa ukabadili TANSAD yako isomeke mwaka husika, ila kwa vile ya kwako imesomeka mwaka wa chini ya ule ulionunulia na ukapatwa na uchakavu hapa HUNA BUDI KULIPIA DUMPING FEES ambayo ni 25% ya CIF, sasa narudi kweny swala kwa nini makaratasi yameandikwa mwaka 2001 na ukaguzi umeonesha 2000, ukiangalia sana wajapani wanachoangalia jamani ni mwaka wa kusajiliwa ilo gari lako kule japan ambapo inawezekana gari ilisajiliwa miaka miwili baada ya kutengenezwa na huku TRA wanaangalia mwaka wa gari lilipotngenezwa ambao sasa ni huo 2000 ambao huwa wanaandika kwenye mikanda yote ya magari yenu, tafadhali ndugu angalia kwenye kitu kinaitwa JAAI au EAA aambayo utakuwa nayo kwenye moja ya documents zako utaona wmaendaika YEAR OF FIRST REGISTRATION ni mwaka gani utaona ni 2001, sasa angalia kwenye mkanda w3ako wameandika YEAR OF MANUFACTURE ni 2000 nadhani hapa umeniapat sasa, muda wa kusajiliwa gari sio muda wa kutengenezwa gari, kwa hiyo MDAU HAPA INABIDI ULIPIE TU HARAKA kukwepa storage na gharama za bandari,

    Angalizo siku ingine ukiagiza gari waambie wakupe mwaka wa kutengeneza gari kwa uhakika kukwepa ishu kama hizi au wasiliana na wataalamu wa hizi mambo wakupe ushauri.

    ASANTENI

    MDAU - MANGI SHIRIMA

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 22, 2010

    Weka chassis number kwenye hii website http://www.sbtjapan.com/chassischeck.aspx hapo utapata mwaka gari lilipo tengenezwa wapelekee TRA hiyo website vilevile wanaweza ku verify kwa magari mengine pia jamani hizi tools zote zipo online isipokua hawa watu wa TRA wanajifanya wanawatu wa IT kumbe ni mambumbu watoto wa vigogo waliofeli masomo akili zimelala. Ndo maana nimeshasema sitaki kazi serikalini maana akili yangu atalemaa.
    Mdau Bongo Forever ( Sitaki kazi serikalini nitakua mbumbumbu)

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 22, 2010

    Pole sana bro hapa bongo uswahili mwingi sana bandari ya bongo mpaka ujuane na kiongozi flani ndio mambo yako yataenda fasta then mi napenda kukushauri elimu ya tz ipo chini sana hata kama viongozi wa pale bandarini ni wasomi wa masters or degree still upeo wao bado mdogo next time ukitaka kuagiza gari pitia bandari ya mombasa wale jamaa wapo kisomi zaidi gari haichelewi wako fasta utafurahi mwenyewe wa tz wengi walioshtukia hili wanashusha mizigo magari yao mombasa mdau kutoka Arusha pamoja sana

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 22, 2010

    pole mdau, hakuna uhalali wa ku-uplift, nirushwa tu. Bahati mbaya sana system zetu (ikiwamo TRA) rushwa ndio inazingatiwa zaidi. TRA wanajua vizuri sana kwamba mwaka ulioandikwa kwenye mkanda ni mwaka ambao mkanda huo ulitengenezwe na si mwaka ambao gari ilitengenezwa, lakini wanajifanya hawajui kwasababu inawasaidia kula rushwa. kuna wakati kampuni ya kuuza magari ya autorec walilifafanua hili na wakawa na kama walsha fulana kuelezea hili kwa TRA wakisaidiwa na maelezo ya wataalamu kutoka kwa baadhi ya manufacturers, lakini hawataki kuelewa kwa sababu watakosa rushwa. kuhusu kupata msaada kutoka kwa wakala wa mizigo (clearing agent), itakuwa vigumu sababu wakala wengi hawajui wako pale kumtetea nani, mteja wake au TRA? wakala wengine wanashirikiana na baadhi ya maofisa wa TRA ili kumtoa mteja pesa zaidi, ma-agent wengi tena wengi sana wanajua kuwa kazi yao ni kutoa gari/mzigo bandarini tu, kuhusu kwamba yeye ni kiungo kati ya mteja na TRA ili kutoa picha halisi ya wateja wasivyoridhishwa na TRA kwa TRA hilo hawalijui na wanaona haliwahusu! Kwa masikitiko makubwa nakushauri wahonge utoe gari yako mapema na kwa bei nafuu, Kwani nina uhakika hata huyo agent wako hakutetei kwa nguvu inayostahili.
    The brain

    ReplyDelete
  25. saidi linoJuly 22, 2010

    MZEE UMEAGIZA GARI TOKA JAPAN KWA PESA NYINGI SASA UNASHINDWA TOA RUSHWA JAPO YA LAKI TATU TU? UTAPOTEZA GARI LAKO SASA HIVI WATAANZA KUKUPIGA STORAGE, HATA KAMA GARI YA MWAKA 2010 LAKINI BILA RUSHWA GARI HAITOKI BANDARINI TENA BAHATI YAKO SANA HAWAJAKAMBIA NI LA MWAKA 1995.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 22, 2010

    wadau mimi binafis nashukuru kwa mchango wenu katika tatizo lililo mkuta mwenzetu.Lakini mimi bado nipo gizani hapa kwamba kuna mchangiaji amesema uchavu utakatwa kwa 25% ya CIFsasa swali langu inamaana hata gari la mwaka 1995 litakatwa gharama sawa za uchakavu na gari la mwaka 2000?.mfano gari nililo agiza la mwaka 2000 lenye CC 1,300 na ghara za CIF ni dolla 3260 itanigharimu kiasi gani hadi kutoa bandarini naomba kufahamu kwa msaada wenu asante.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 22, 2010

    wewe bwana Mangi Shirima unaonekana ni mmojawapo wa TRA mnaowadanganya watu. issue hapa ni kama kweli mkanda unaonyesha mwaka wa gari kutengenezwa au mkanda kutengezwa. wewe unatetea TRA.

    tumshauri vizuri huyu jamaa. kaka angalia hiyo site uliyopewa na kama vipi juana nao vinginevyo kama hawapo sawa lipa halafu nenda kwenye haki.

    HATA HIVYO WATANZANIA VICHWA NGUMU. HIYO BANDARI WEZI KUPINDUKIA. MIMI WALIIBA KILA KITU KWENYE GARI, TRA RUSHWA, BANDARI WACHELEWESHAJI WA MIZIGO, BADO MNAENDELEA KUITUMIA HIYO BANDARI PAMOJA NA KUSHAULIWA KUTUMIA MOMBASA AMBAYO NI EFFICIENT. SHAURI YENU.

    MSILALAMIKE TENA.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 22, 2010

    No hassle tumia Mombasa pitia Namanga au Holili, no hassle ukirudi TZ shukia Nairobi or Kilimanjaro,life goes on. Dareslaam kumejaa wezi tu kuanzi posta, na kwingineko.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 22, 2010

    Pole sana.
    TRA ni wasumbufu sana. Wafanyakazi wa pale hawajui kutumia elimu waliyonayo kufikiria vizuri, utafikiri hawajaenda hata shule ya msingi.

    Nimemaliza kuangalia kwenye gari yangu sasa hivi.
    Tofauti ya mwaka wa gari na mwaka wa seat belt.

    Ni gari ya kijapan (Toyota) imekuwa registered mara ya kwanza mwaka Nov 2000.

    Mikanda miwili ya viti vya mbele imeandikwa hivi:
    Seat belt for automobiles
    Mfd. by Tokai Rika Co. Ltd for Toyota motor corporation in Dec 1999.

    Mikanda mitatu ya viti vya nyuma imeandikwa hivi:
    Seat belt for automobiles
    Mfd. by Takata Corporation for Toyota motor corporation in March 1997.

    Kwa hiyo mikanda ya viti haitengenezwi na kampuni ya Toyota yenyewe bali inatengenezwa na makampuni mengine kabisa kwa ajili ya magari ya Toyota.

    Hivyo ni uhaini mkubwa kusema kuwa mwaka ulioandikwa kwenye mkanda ndiyo mwaka wa gari kutengenezwa.
    Hii ni njia tu ya kutaka rushwa full stop.

    Gari inaanza kutumika tokea upya wake toka pale tu inapokuwa registered kwa mara ya kwanza na kuingizwa barabarani.

    TRA tumeni watu wenu waende Japan wakapewe shule ya tofauti kati ya mkanda wa gari na gari yenyewe siyo kungangania ujinga.

    Hiyo yote inakuwa nikusumbua wateja tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...