Marehemu Hamisi Abdallah George Mmakua
Kamati kuu ya maandalizi ya kusafirisha mwili wa Marehemu Hamisi Abdallah George(Mmakua) aliyefariki mjini Rome, Italy tarehe 18 julai 2010, saa tatu na dakika ishirini na tano usiku (21:25), ikishirikiana na Jumuiya mbalimbali za Watanzania nchini Italy, inapenda kuwafahamisha Watanzania wote mliopo nchini Italy kuwa mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumamosi tarehe 31 Julai 2010 saa sita mchana(12:00) kabla ya kwenda kupumzika kwa amani nchini Tanzania. Mwili utaagwa kwenye Istituto Lazzaro Spallanzati, iliyopo nyuma ya Ospitali ya San Camillo, kwenye mtaa wa Via Folchi 6/a, mjini Roma. Watanzania wote mnaombwa mfike ili tumuombee na tumuage marehemu. Kwa maelezo zaidi tafadhali tembeleeni blog ya Jumuiya ya Watanzania Rome: www.watanzania-roma.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Poleni ndugu zetu wa Rome; na Mungu Ampe Marehemu pumziko jema.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2010

    R.I.P Mmakua!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2010

    Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, poleni wote mlioguswa na msiba huu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2010

    Watu wa Rome/Italia nawapongeza sana jinsi mnavyoshirikiana kikamilifu kwenye misiba. Ingekuwa Marekani au Uingereza, tungeona mabakuli. Kwaheri Mmakua.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2010

    Nawapa pole wafiwa wote,na naomba Mungu amsafirishe salama marehemu na hata afike salama nyumbani na apumzike kwa amani,Mungu amrehemu!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2010

    wewe mdau wa 11.19 am umeisha kaa usa au uk au unaongea tu bila kujua unataka kila mtu aliyefariki atangazwe kwenye blog?jaribu kutumia akili bila kuongea vitu usivyojua.poleni wafiwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...