Mtangazaji wa TBC One Elisha Eliya kama anavyoonekana leo asubuhi
Ankal akiongea na Elisha Eliya walipogongana kwenye viwanja vya maonyesho vya Mwalimu Nyerere ambapo mtangazaji mahiri alitoa shukrani kwa wadau wa TBC One na maoni yao juu ya utendaji kazi wake na wenzake. Pia amesema si kweli kwamba ana suti moja tu kama Mdau wa Mafia alivyodadisi kwenye salamau zake. Elisha kasema TBC One inatoa kasma ya mavazi kwa watangazaji kila mara na kwamba kwake yeye tatizo ni kupenda suti za mistari mistari hivyo kuonekana kama ni hiyo hiyo tu. Ameshukuru wote waliotoa maoni yao na kuahidi kuendeleza libeneke la kuleta mambo moto mtoto kila asubuhi. Kwa habari yake ya awali:
BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2010

    Haya kaka elisha tumekusikia na bora umekiri kuwa una suti moja ingawa hukuweka wazi umezungushazungusha kuwa unapenda suti za mistari. Je? na rangi unapenda rangi moja? jipende kaka elisha ili kazi yako ionekane vyema. pia vaa mashati ya rangi za tofautitofauti jana ulivaa pink na leo pink ndo maana unaonekana umevaa kilekile. Hongera kwa kuwa mtangazaji mahiri ongeza juhudi katika mavazi yako.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2010

    Tunashukuru kama umefurahia kukosolewa huo ndo tunauita uzalendo, Mdau wa mafia inaelekea anakufahamu vyema na anakufatilia mno. Ongeza juhudi ya kubadilisha suti na mashati kaka elisha. Sio usubiri mpaka ukosolewe

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2010

    Hongera sana Elisha, mimi ni mdau mwandamizi wa TBC1. umefanya vema kutoa aufafanuzi, lakini pia jambo kubwa ni kwamba umeweza kufahamu kuwa una wadau wengi wanaofuatilia kazi yako na ya TBC1 kwa ujumla, kwa maoni haya pia nadhani utakuwa umepata mawili matatu ya kujiimarisha zaidi kitaalam na kuimarisha kituo chetu, aaaaaah salamu sana kwa dada Agnes Mbapu, na Jafari Haniu. jamni kulikuwa na mdada hivi namsikia siku hizi anga za kimataifa, Zawadi Machibya. TBC1 hoyeeeeeeee!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2010

    TBC1 inatisha bwana eee, mamaa mwenyewe Suzan Mungy, Gloria Bondo wera weraaaaaaaaaaa, dada wa ukweli asikuambie mtu, ila nimekumiss ile mbaya na pilika hizi za kombe la dunia, hope nitakuona siku si nyingi. Kipindi chenu kipya cha daladala najua kitakuwa moto kama kawaida, tena nawafagilia kwa kuwa na mai martha na Ben kinyaiya, vijana wa mirindimo ya kiafrica, Tirdo Mhando endelea kuleta ubunifu. Ila kweli Gason Msigwa, na Emmanuel Amas si mchezo, wafikirieni mara mbili hawa vijana wanatisha, hata Richard Leo "nikiripoti kutoka picha ya samakii, Richard Leo
    Mwanza.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2010

    Watanzania wakati mwingine wakikosa cha kusema wanafuatilia life style za watu..Mimi sikuona tatizo la suti hata km ni moja..Kwa taarifa ni kuwa wapo watu wana class za nguo anaweza kuwa na suti ya aina moja seti 5 na akaamua kuwa hizi ni za ofisini na nguo zake nyingine zikawa za ocasion zingine sasa mwataka kila nguo ajitundike nayo TBC..Achana na watu Elia walikosa la kusema..BIG Up i also do the same and i look smart always

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 02, 2010

    BOSSI TIDO MHANDO NA SUSANE MUNGI, MLETENI KIJANA GASTON MSIGWA HAPO MAKAO MAKUU ILI TBC IZIDI KUWA JUU ZAIDI, HUYU JAMAA ANAKIPAJI SANA NAKUMBUKA WAKATI WA UCHAGUZI WA MAREKANI NDIO YEYE ALIKUWA ATITUPA TAARIFA YUU YA UCHAGUZI, OMBI LANGU KAMA WADAU WENGINE, TBC MTOENI KIJANA HUYU HUKO SONGEA ILI AJE HAPO MAKAO MAKUU. UNCLE NAOMBA UNIFIKISHIE HUU UJUMBE KWA WAUSIKA ILI IWE KAMA CHANGA MOTO

    ReplyDelete
  7. Watanzania tusionyeshe kufilisika kwetu kimawazo na kimtazamo,Hivi kweli tunaloweza kuliona kwa elisha ni mavazi yake? mie nafikiri Elisha ana zaidi ya hilo...
    Kijana elisha nimesoma nae Seminary, nauelewa umakini wake, nauelewa unadhifu wake, kiutendaji na kimuonekano.
    Hivi wana habari wangapi maarufu duniani tunaowafahamu na huwa wanavaa nguo za aina moja?
    maraisi wangapi huwa wanavaa suti, tai na shati za aina moja? kwanini kwa elisha mfikirie eti anayo moja?
    Hivi wafanyakazi wa BOT wanaovaa shati jeupe kila siku ni kwamba wanalo moja?
    Tuache mtindio wa mawazo watanzania, Tushauri yanayojenga sio yanayobomoa, Kijana mtangazaji wa leo, ndio mtangazaji bora wa kesho kama ataonyeshwa njia iliyo bora na kupewa ushauri ulio bora.
    Endelea kupiga kazi kijana elisha mawazo chanya yachukue, yale hasi yaliyo na lengo la kukuvunja moyo yafanyie tathmini halafu yaache.

    ---LJS 2000---

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 02, 2010

    Watanzania tuna haki ya kukosoa, kwani elisha ni nani hadi uone kuwa akikosolewa watu hawana la kufanya? ndiyo maana ya uhuru wa vyombo vya habari kama inakukera sana kaa tu kimya kuliko utoke nje ya jenda. TBC iko juu na elisha tunamfahamu sana na anajisahau lazima akumbushwe, outing yake ni kwenye kazi yake. TBC inaonekana hadi nje ya nchi sasa kuwa na mtangazaji asiyejipenda ni kuharibu jina la kituo chetu kizuri. ajifunze kuwa smart kama wenzie kina msami. mbona baada ya kukosolewa anabadilisha suri. hata mashati ajifunze kubadilisha. kama hajipendi aachwe kwenye kazi ya kuripoti tu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 02, 2010

    Hapo amejitetea tu, lakini siku ya pili yake asubuhu baada ya lile bandiko, nilimsikia akilalamika kuwa anasuti mbili tu. Hakujua kuwa yuko ON-air.

    KakaJambazi

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 02, 2010

    Asiye na maoni akae kimya siyo atoe maneno ya kashfa. Elisha lililo nzuri lichukue baya liache. mwenyewe unajua zuri na baya kwani kila mmoja atasema anakufahamu vizuri hata wale adui zako.
    kila mwanadamu ana adui wake lazima ulijue hivyo

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 02, 2010

    huyo Elisha ninayemjua mie hastahili hizi sifa , huyu ni mnyanyasaji sana kwa wanawake hana heshima hata kidogo na chupi yake kaishikilia mkononi mda wote. Si kioo cha jamii na akiisoma hii message ataelewa, rudi nyumbani kwa mkeo, mheshimu mkeo, tunza mtoto wako kaka.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 03, 2010

    Watanzania kweli pumba tu. Mnaacha kuangalia anatangaza nini mnakalia ana suit moja sijui nini. Kama ni moja lakini ni safi nyie mnajali nini.

    Ndio maana kuna miwanaume hapa inavalia vizuri tu lakini kwenda shule haitaki.. Kalieni kuangalia nani anavaa nini na wewe unakimbilia mall kununua nguo mpya kesho fashion mpya imeingia na wewe unakilimbilia tena. Shauri yenu mmesahau mnazeeka sasa..

    Smart people will judge you for what you know not how you dress...Kama upstairs kumechangamka na umepanga vitabu vyako vinavyoeleweka...unajua kuoga at least mara moja kwa siku na deodorant kidogo don't worry..Its all good and women like that..

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 03, 2010

    we anony wa Fri Jul 02.08:31:00 ACHA ROHO MBAYA! ROHO YA KWA NN! utaishia hivyo hivyo kwa roho yako mbaya na kufatilia maisha ya watu! hizo ni CHUKI BINAFSI! Hapa Elisha hakuongelewa maisha yake binafsi! Alichoongelewa ni utendaji wake wa kazi, uwe mwelewa! usiwe unakurupuka tu kuchafuwa wenzio! km kashika chupi mkononi we yanakuhusu nn? yaani natamani nikutakane matusi yote yalipo yaliyopo Duniani! km mademu wanajipendekeza kwake afanyeje? kula wote Elisha kumbuka tu kuvaa soksi! Endelea kuulamba kaka yangu, C unajua mademu wa bongo wanavyopenda wanaume wenye majina!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 03, 2010

    ankal naona mazoezi hakuna kolesto hizo baba angalia bado tunakuitaji kuendeleza libeneke. mdau wa texas

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 03, 2010

    Wewe anony uliyeshauri Gason Msigwa ahamishiwe makao makuu, ushindwe na ulegee. Umesikia Songea hakuhitaji mtangazaji mahili? Na sisi wa Songea Mkimhamisha Gason Msigwa tutasusia kuangalia TBC1. Mkoa wa Ruvuma sasa hivi upo juu kwa ajili ya huyu Jamaa na sisi huku tunaheshimu sana TBC sema tatizo TIDO MHANDO hajatuletea ving'amuzi wala mitambo ya FM lakini Msigwa anatusaidia sana, ni tegemeo letu. Tafadhari jamani msimhamishe huyu kijana tutapotea tena huku Songea

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 03, 2010

    Wewe anony uliyeshauri Gason Msigwa ahamishiwe makao makuu, ushindwe na ulegee. Umesikia Songea hakuhitaji mtangazaji mahili? Na sisi wa Songea Mkimhamisha Gason Msigwa tutasusia kuangalia TBC1. Mkoa wa Ruvuma sasa hivi upo juu kwa ajili ya huyu Jamaa na sisi huku tunaheshimu sana TBC sema tatizo TIDO MHANDO hajatuletea ving'amuzi wala mitambo ya FM lakini Msigwa anatusaidia sana, ni tegemeo letu. Tafadhari jamani msimhamishe huyu kijana tutapotea tena huku Songea

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 03, 2010

    we anon hapo juu unajishebedua nini kutetea ujinga mbona alipotajwa kijana mzuri mtanashati hukusema personal life walipomsema vibaya unashika bango eti ale wote wanajipendekeza atakula wewe unaemuona wamaana kwako. malaya mkubwa unaendekeza ufska humu kwenye blog yetu. labda alisha kula wewe sasa unamtaka tena lo ankal usibane hii maana ya ugonile umebana sio poa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...