Usiku wa kuamkia jana ofisi za Global Publishers zilivamiwa! Mara baada ya uvamizi huo walimteka mlinzi na kumfunga kamba kisha kuondoka naye na kwenda kumtupa maeneo ya kurasini Temeke jijini Dar es Salaam hata hivyo askari huyo yuko chini ya ulinzi anaisaidia polisi.
Inasemekana kulikuwa na makundi mawili ya majambazi waliokadiriwa kufika ishirini, ambapo kundi la kwanza liliondoka na mlinzi huyo ambaye alifungwa plasta mdomoni na kamba mikononi na miguuni, kisha kundi la pili lilivunja mlango na kuingia ndani ya news
room.
room.
Habari zinasema walipoingia ndani ya news room walipekua na kuvunja droo kadhaa na kutupatupa vitu vingi ikionesha kulikuwa kuna kitu au nyaraka fulani waliyokuwa wakitafuta, kwani hakuna hata kompyuta moja iliyoibwa wala kuguswa! Zaidi walichukua TV moja ndogo ya flat screen, iliyokuwa reception kwa sababu wanazozijua wenyewe na kuondoka nayo.
"Ni jambo la kushangaza kwa kweli na kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na usumbufu na hasara ambayo tungeipata kama wangebeba kompyuta", afisa wa chombo hicho cha habari anasema.
"Tumeona ni bora tuwafahamishe wasomaji wetu wapendwa juu ya jambo hili ili muweze kujua kilichotokea siku ya leo ambayo imetufungua macho na masikio na kutufanya tuamue kuchukua hatua madhubuti ya kuimarisha ulinzi na usalama wa kampuni yetu", aliongezea.
Kwa picha na habari zaidi
huyo mtaalam wa fingerprints mbona hajavaa gloves?
ReplyDeletePole sana mithupu,hawana lolote km bao umeshawapiga wakati wewe unatembea wao walikuwa wanatambaa na kujitia siku zinaganda sasa wewe unakimbia wanataka utembee km wao.Kaza buti achana nao na wasipoamka muda huu wataendelea kulala mpk siku ya kiama.
ReplyDeletemh!!hapa ndo uwa najua kuna mafia hii nchi
ReplyDeletepoleni global publisherz
..Duh hao majambazi kiboko... hii habari imenikumbusha sana wale jamaa walioiba mifano ya Kombe la dunia kule Kwa madiba....
ReplyDeleteof coz kupunguza hasira za kukosa hiz nyaraka nadhani wakaamua kuchukua tv.
Hata wana-sisiemu mnavamiwa, safari hii Global lazima mlikuwa na news za kutikisa jamii.
ReplyDeleteMdau
Nairobi.
Ofisi kama hii ya Global inatakiwa iwe ina shift ya wafanyakazi wachache wa usiku, huku kukiwepo pia mlinzi, hiyo ndiyo dawa ya kuzuia 'udaku' kuporwa kirahisi toka ofisi za Global.
ReplyDeleteMaana waliotumwa wakifika reception wataonwa na mlinzi+CCTV na kwa vile kuna staff wachache wa shift ya usiku basi patakuwa pagumu kunyakua habari 'nyeti' toka madroo ya wahariri.
Mdau
MagazetiYaUdaku-Ughaibuni
Watu wana usongo na story za udaku.
ReplyDeleteSasa cha kushangaza baada ya nyie GP kuvamiwa, mbona mnaharibu "crime scene"? Sijui wamewaruhusu kivipi kwa haraka hivyo kuingia ndani ya jengo kabla ya hawa watu wa "forensic" kufanya kazi yao!
ReplyDeleteNa huyo mtu wa "forensic" hana gloves wala magwanda ya plastic ya kutokui "contaminate" crime scene"?!
yaani bado baongo mnafanya mambo kienjeji kabisa, ebu mwamngalie huyo jamaa na kabrashi, na kakopo kadogo kabisa ka majivu!
Ni kichekesho na aibu!
Tizameni CSI Miami, Vegas, New York na zingine muone wenzenu wanavyoishughulikia crime scene, na sio huo ujinga na usanii mnaoufanya!
Mnachukua finger prints wakati hakuna Database ya ku-search hizo prints na kugundua ni nani anaye husika! Jeshi la Polisi lipo nyuma sana na inaonesha kama lipo ktk karne ya 10 hivi! Mnashindwa kuvaa ata gloves! Ni aibu kubwa sana, yaani jeshi linaendeshwa kama Primary School!
ReplyDeleteYani hata CCTV (KAMERA) jamani hamna. Acheni uzamani bwana, wala sio gharama. Hao jamaa mngewapata kiurahisi na kuweza jua kilichowafanya waje hapo na mengine mengi. Usikute wametumwa na mtu au kampuni flani, mngiweza jua hayo nakujua kwanini, kitu ambacho kinawaweka nyie ktk position ya kujua mko ktk mazingira gani na mjipange vipi. Haloo, mnaandika habari nzuuuuri kumbe hamuwezi fikiria vitu kama hivi, kuweni analytical in a bigger picture sio kwenye habari mnazoandika tu. Natamani nitukane, mmeniuzi kabisaaaaaaaaaa
ReplyDeletekumbe ofice yenu yote hiyo inalala usiku ...mnatakiwa muwe na 24 hours shift..hata muigawanye kwa masaa 8 8 ...ndio maana mnasongoa hadithi kutwa kwa vile kazi hamna la kufanya.. weka wafanyakazi wachche kila shift..mkijaga huku hamwendi kutembelea vyombo vya habari muone jinsi wanavyowork work..hawalali wenzenu..
ReplyDeletewaosha vinywa wenzangu mlio changia kutoa madaa zenu mbona mna jazba sana jamani nyie eeh?
ReplyDeletepoeni moto, cool down and cheel out,mnataka kuifananisha Tanzania nchi yetu tukufu na marekani,eti data basse za kuchukulia finger print hatuna,sijui haja vaa gloves sijui nini na nini, sasa mbona katika picha hii haionyeshi huyo jamaa aliye haribu crime scenery?
uzushi mtupu na majungu ndo muwezayo na mdomo kaya, kama mnanaona tuko nyuma hebu saidiyeni nchi yenu mlioko huko majuu mbona hamfanyi hivyo domo kaya mkija katika website hii ya michuzi
kuweni wastarabu kidogo na wekeni heshima huko huko kubaya vacation zenu mnakuja kila leo, mtu kwao na heshima hupewa kwao, huko uzunguni mnadhalilishwa mbona hamsemi kweli
watu wanafanya kazi pesa zote zina ishia renti hata raha ya ulaya hamfaidi mkija nyumbani ndo mnajitia mabrother man na ma sister duu mchwara mchwara kwa kubeba maboksi au kupata makaratasi kwa vijizee vya kizungu na vijanajike na vijanadume vizima haya hamuoni kutembea na mababu zenu kwa karatasi ya kujia nyumbani
wacheni hizo
enzi ni chenu na heshimuni chenu, nchi yenu
hahahaha! wabeba box mnalo? huyo jamaa hapo juu kawapaka. ngoja waamke watakuja na jazba patakuwa hapatoshi!
ReplyDeleteJamaa kawambia ukweli, watu kwa kuwa wako ulaya basi ni dharau tu. Mbona hayo yenu ya ulaya mabaya hamyasemi au mnadhani tuliopo huku hatujui? Watu kila siku Bongo mko nyuma bongo mko nyuma mlio mbele mmeleta mabadiliko gani sasa?
ReplyDeleteMnaowaponda wasioenzi chao ebu niwaulize tuenzi kitu gani hapo? Hako kabrash au majivu? Au Tuenzi jinsi tusivyokua organised? Sio kwamba pesa hamna, pesa ipo ya kununulia hizo gloves, magwanda ya plastic, utepe wa kuonyesha neno police, n.k.
ReplyDeleteAu ulitaka tuseme kwamba aise hawa watu wa forensic wako professional ile mbaya!
Labda ulitaka tushauri mganga aje apiga ramli? Au Vitabu vya dini vije na watu wasomewe dua?
Wabongo bwana?!