Wadau wa Rio Blanco Internet and Video Libray ya Mwananyamala Komakoma wakiwa katika uzi wa Globu ya Jamii leo mbapo huduma za mtandao nyingi aidha ziko slow ama hazipo hewani kabisa kutoka na na kwikiw ya mkongo wa Seacom toka jana. Globu ya Jamii inatumia Vodacom Internet Serevices hivyo hamna kwikwi wala nini. Libeneke oye!

SEACOM SERVICE DOWN; SEACOM actively seeking options to restore service

At 09:19 GMT, 5 July 2010, SEACOM experienced a submarine failure resulting in service downtime between Mumbai and Mombasa. Current investigations indicate that a repeater has failed on segment 9 of the SEACOM cable, which is offshore to the north of Mombasa. This unexpected failure affects traffic towards both India and Europe. Traffic within Africa is not affected.

SEACOM has initiated emergency repair procedures to replace the repeater. Once mobilised, the repair ship is deployed to the location of the fault to pick up the cable. The cable is then brought on board to undergo the repair – the faulty element is replaced with a new repeater - before being put back in the water.

Whilst the repair process itself will only take a few hours, the overall process may last a minimum of 6-8 days. The actual duration is unpredictable due to external factors such as transit time of the ship, weather conditions and time to locate the cable. For this reason, the estimated duration of this repair remains uncertain.

SEACOM, in co-operation with individual clients, is actively seeking alternatives to restore service whilst the repairs are undertaken.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2010

    Mimi nilidhani internet network ni kama barabara ya usafiri wa basi toka DSM kwenda Mwanza kupitia Kilosa na Dodoma. Ikitokea mafuriko Kilosa, basi usafiri utakuwa kupitia Korogwe, Arusha, Namanga, Kenya halafu tunarusi Musoma mpaka tunaingia Mwanza.

    Hii internet network gani isiyokuwa na alternative?!?

    Mdau
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2010

    SI MLITUAMBIA MAMBO YATAKUWA BOMBA BYEEEE, KELELE NYINGII NA HUO NI MWANZO TU NA NGOMA IKO MPYA MMAAAA JE IKISZEEKA? SI ITAKUWA PATASHIKA NGUO MKONONI!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2010

    this will happen frequently nd we have to bear it because we have nothing like backup system.we always have somebody controlling our lives.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2010

    Ubungo Darajani himaya ya vibaka

    Nalo eneo la Ubungo Darajani linatajwa kushamiri vitendo vya uhalifu hasa wa kupora watu.

    Inadaiwa kuwa genge la vijana zaidi ya 20 linalofanya uhalifu limepiga kambi katika eneo hilo kiasi ya kuhatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo na wasafiri wanaotumia barabara ya Mandela.

    Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kibangu, Kata ya Makuburi, Desdery Ishengoma, alithibitisha kukithiri kwa vitendo hivyo na kueleza kuwa vinachangiwa na biashara ndogondogo zinazofanywa kando kando mwa barabara ya Mandela, eneo la Darajani.

    Alisema tayari ofisi yake imeandika barua kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na kupendekeza kuwa eneo hilo lifanywe bustani za miti na maua badala ya biashara ndogondogo.

    Alisema mbali ya pendekezo hilo, ofisi yake imetengeneza mpango wa kuweka sungusungu katika eneo hilo na kwamba kwa sasa vijana watakaoshiriki kazi hiyo wameanza mazoezi.

    “Kwa kweli hapa darajani hali ni mbaya sana, watu wanaumizwa na kuporwa kila saa na kila siku...sisi tumeshaliona tatizo hilo na kama nilivyokueleza, tumeanza kuchukua hatua,” alisema Ishengoma.

    Alisema kwa siku wamekuwa wakipokea malalamiko zaidi ya matano kutoka kwa watu mbalimbali wanaojeruhiwa na kundi hilo la uhalifu.

    “Lakini naamini hao ni wale wachache wanaoamua kuja kwetu, matukio ni mengi sana kutokana na hatari iliyopo,” alisema.

    Wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kikundi cha vijana hao kimekuwa kikifanya uhalifu na kukimbilia chini ya daraja.

    Alfred Mushi, mkazi wa eneo hilo alisema vibaka kwenye eneo hilo wamekithiri huku polisi wakifumbia macho matukio ya uporaji na kuwaacha vibaka wakitamba.

    “Si unaona kituo cha polisi kipo jirani tu, lakini hapa vibaka wanatamba utafikiri hamna vyombo vya dola...ukienda polisi unaulizwa una gari? au wanakuambia hawawezi kutoka kwa sababu hakuna askari wa kubaki kituoni,” alisema Mushi.

    Alisema wakati mwingine askari wamekuwa wakiandika maelezo na kuahidi kufuatilia tukio, lakini hawafanyi hivyo na ndio maana vibaka wanatamba katika eneo hilo.

    Alisema: “Hali hiyo imekuwa ikichochea hasira za wananchi, ndio maana wakifanikiwa kukamata mhalifu wanamchoma moto kwa kuwa polisi wakimkamata kibaka asubuhi, mchana unamkuta mtaani.”

    Mwananchi mwingine, Abdalah Jumaa, aliwalaumu askari wa vituo vidogo kuwa na kasumba ya kupuuza malalamiko ya wananchi.

    “Ukiongea na Kova (Suleiman Kova, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam) anakujibu vizuri kuliko hawa askari wadogo, yaani ukiwa na tatizo huwezi kuhudumiwa bila kuwasiliana na Kamanda Kova ili awaagize watu wake katika vituo husika...sijui kwa nini hawa askari wako hivyo,” alisema.

    Polisi wa Kituo kidogo cha Ubungo Kibangu ambao hawakupenda kutaja majina yao, walisema wakati mwingine wananchi wamekuwa wakikuza matukio ikilinganishwa na hali halisi.

    “Kama wananchi wanasema hapo Darajani kunatisha, mbona hawaleti malalamiko yao hapa? Ni kweli pale kuna vibaka, lakini sio tatizo kubwa kama ulivyoelezwa na hao unaosema ni wananchi,” alisema askari mmoja.

    Baada ya kueleza hayo, askari wa kituo hicho walimtaka mwandishi wa habari hizi kuwasiliana na Kamanda wa Kanda Maalum kwa ufafanuzi zaidi kwa maelezo kwamba wao sio wasemaji wa jeshi la polisi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2010

    Hayo ndo mambo,kila ki2 kwetu sawa maana Tz ndo jalala la kitu au niseme ni sehemu ya majaribio kujua kitu fulani kina madhala au la ndo kisambazwe kwingine.
    Hongereni mliotia sahihi ktk mkataba huo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...