JK akimkaribisha mgeni wake Rais Luiz Inacio Lula da Silva muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana jioni kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania
Rais wa brazil Luiz Inacio Lula da Silava wa Brazil akikaribishwa kwa maua muda mfupi baada ya kuwaisili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa jijini Dar. Pembeni yake ni mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete.
Rais Wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokea heshima wakati wa gwaride rasmi la makaribisho lililoandaliwa na jeshi la wananchi wa Tanzania katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar
Rais Wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokea heshima wakati wa gwaride rasmi la makaribisho lililoandaliwa na jeshi la wananchi wa Tanzania katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Wananchi wa Tanzania muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana jioni





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2010

    Karibu Lula,
    Karibu mwanamapinduzi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2010

    this man is a real great leader viongozi wa kitanzania wajifunze kwake

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2010

    Hawa jamaa tofauti na soka ila wameendelea kiuchumi.Tushirikiane nao hata watusaidie katika kilimo ili tuendeleze mpango wetu wa kilimo kwanza.

    El presidente Luiz Inacio Lula da Silva, bienvenido a Tanzania

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2010

    JK tunaona juhud zako,umeipa nchi yetu heshima na umaarufu ambao ulipotea kabisa.kipindi cha miaka ya 70 tz iliheshimika umo,watu maarufu duniani waliangalia tz moja ya ngao kuu ya africa,tuliona watu kama,malcolm x,fidel castro,mohamed ali, na wengine wengi,lakini mika ya 80 viongozi wote maarufu waliishia kenya,na tz ilionekana nchi iliyokata tamaa.now tz imeanza kurudisha heshima yake,na viongozi wengi duniani wanaamini ni moja ya nchi zenye democrasia na kupiga hatua kubwa africa.JK hongera baba japo wengi hawakukubali nyumbani,kumbuka nabii halubaliki nyumbani

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 07, 2010

    kweli jamaa mwanamapinduzi,juzi amekataa kusign iran kuwekewa vyikwazo,nafurahi kuona viongozi hawa wamewashtukia wazungu wanatunyonya tu hamna zaidi,Lula ameinyanyua brazil vibaya,na anawawekea kiburi wazungu vibaya,naona mshirika wake mkubwa ni uturky.hawa jamaa ndo wameshtuka waangalia maslahi sio siasa,udini,ukabila kama nchi za africa.ukiangalia brazil ni taifa la kikatoliki,lakini wako bega kwa bega na mturuki ambayo ni taifa lla kiislam.maslahi mbele,ili wananchi waishi maisha mazuri mambo ya dini na rangi baadae.brazo lula

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 07, 2010

    jamaa aliipanga trip hii akijua ataishia south kuona brazil fainal.kweli dunga sucks!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 07, 2010

    TALK ABOUT INVESTMENT FROM BRAZIL TO TANZANIA ILI KUSAIDIA VIJANA NA WATU WOTE KWA UJUMLA MASWALA YA KAZI HASA UPANDE WA KILIMO NA BIO-FUEL, PIA ELIMU KWA VIJANA NA MTU YOYOTE ANAYEPENDA KUSOMA BRAZIL

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 07, 2010

    the most liked president in brazilian history. JK jifunze kwa mwenzio, hakumbatii mafisadi...

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 07, 2010

    huyo mfasiri/mlinzi wa Raisi Lula ni pacha wake maana wamefanana sana. Wadau wa Rio De Janeiro tupasheni.
    Mdau
    Gongo La Mboto

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 07, 2010

    ..hicho ndo kichwa ambacho mataifa makubwa..yamekinyoshea mkono....nchi zote zimedumbukia katika recession....yeye haha...aka...nchi yake inapeta...uliza ni nini siri ?....kilimo...! sio kama wana ardhi nzuuuuuri kupita sisi....wamejaribu kusaidia kwa moyo wakulima na kuwatafutia masoko ya nje....wenzangu na mimi mmhh...wanamind saaaana 10%..na kwenda nje kutoa matongo...wakirudi..bwechee...bwetee...!!

    ReplyDelete
  11. godfatherJuly 07, 2010

    Weusi wa Brazil wanashida kama vile enzi za Apartheid Afrika Kusini! Halafu homeless na wasio na kazi wako wengi mno! Msidanganywe!

    ReplyDelete
  12. Ndoto ya mchana,Sweden.July 07, 2010

    Brazil inatafuta njia ya kutajirika na nchi za kiafrika kama Tanzania ambazo haziko makini.Ni rahisi sana kuchota raslimali Tanzania na kuwa tajiri miaka michache.ukiwa na exposure na ukirudi Tanzania ni rahisi kutengeneza fedha nzuri,njia za kupata fedha kihalali ziko ila mawazo yanakosekana miongoni ya Watanzania.Brazili uchumi unamilikiwa na watu wachache tu na mchawanyiko wa uchumi hauko sawa kabisa.
    Umasikini umetawala kwa Wabrazili weusi ambao wana asili yao toka Afrika enzi za utumwa.Wengi wao wanaishi kwenye vijibada na maghetto yenye hali mbaya kabisa ya Favela,huko kuna hali ya juu ya uharifu na utumiaji wa madawa na umalaya.Weusi wanabaguliwa ktk kila kitu wachache wanapata nafasi ya kusoma vyuo vikuu na kuna ubaguzi.
    Rais wa Brazil ana changamoto nyingi tu nchini kwake kwa hiyo WaTanzania msifikirie atawatoa nje ya dimbwi la umasini.Tamzania tuna karibia kila kitu cha kuifanya nchi kuwa tajiri ila inakosekana mipango,vipaumbele,sera nzuri zinazotekelezeka,elimu ambayo ina reflect mazingira yetu n.k. Inaonekana Tanzania tuko likizo kwenye kufikiria na tumekuwa ombaomba wa kutupwa hadi vitu vidogo vidogo tunategemea mawazo na misaada ya kifedha kutoka nchi zingine.Inasikitisha Tanzania.
    Ndoto ya mchana,Tanzania.

    ReplyDelete
  13. Lula es un ejemplo perfecto especialmente para ese presidente conocido como kikwete! lula adora su país y el otro odia... yaani manake (lula is a perfect example especially for that president known as kikwete! lula loves his country and the other one hates)

    ReplyDelete
  14. lula is a perfect example especially for that president known as kikwete! lula loves his country and the other one hates...
    kwa wenzagu-
    Lula es un ejemplo perfecto especialmente para ese presidente conocido como kikwete! lula adora su país y el otro odia

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 07, 2010

    Kweli, hii trip ilikuwa ni ya South Africa kuangalia fainali. Kibao kimegeuka kwa Brazil.... Karibu utalii Bongo itasaidia kupunguza machungu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 08, 2010

    hana mpango alifikiri alikura mlungura wa Iran akakataa kusaini,yako wapi sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...