Kaka Michuzi mzee wa libeneke,
Tunakushukuru sana kwa kuendeleza libeneke la kuunganisha wadau wote duniani. Naomba uniwekee swali langu kwenye globu yetu ya jamii.
Naomba kuuliza swali kizushi: Katika kombe la dunia linaloendelea Kusini mwa Africa, bahati mbaya timu zetu za Africa hazikufanya kama wengi tulivyotegemea hasa baada ya Ghana kutolewa jana.
Nimeongea na wadau kibao, kila mtu na sababu zake: mara siasa, mara hatujui mpira, ohh hali ya hewa, ohh wachezaji hawana uchungu na nchi zao, na kadhalika. Ila wakati huo nikaona siwezi kuzilaumu nchi sita zilizoenda wakati nchi yangu Tanzania haijawahi hata kufika kombe la dunia...
Bila kiswahili kirefu, nependa wadau wanisadie: Kwavile mashindano ya kombe la dunia yatakuwepo mengi tu huko mbeleni, Tanzania tufanye nini ili tushiriki hata miaka nane ijayo???
Brother nitashukuru msaada wako
Mdau J Makwanga
Tunakushukuru sana kwa kuendeleza libeneke la kuunganisha wadau wote duniani. Naomba uniwekee swali langu kwenye globu yetu ya jamii.
Naomba kuuliza swali kizushi: Katika kombe la dunia linaloendelea Kusini mwa Africa, bahati mbaya timu zetu za Africa hazikufanya kama wengi tulivyotegemea hasa baada ya Ghana kutolewa jana.
Nimeongea na wadau kibao, kila mtu na sababu zake: mara siasa, mara hatujui mpira, ohh hali ya hewa, ohh wachezaji hawana uchungu na nchi zao, na kadhalika. Ila wakati huo nikaona siwezi kuzilaumu nchi sita zilizoenda wakati nchi yangu Tanzania haijawahi hata kufika kombe la dunia...
Bila kiswahili kirefu, nependa wadau wanisadie: Kwavile mashindano ya kombe la dunia yatakuwepo mengi tu huko mbeleni, Tanzania tufanye nini ili tushiriki hata miaka nane ijayo???
Brother nitashukuru msaada wako
Mdau J Makwanga
Kweli swali la kizushi.
ReplyDeleteMaximo aliwaanzishia cha kufanya mkampiga majungu weee! Andaeni chipukizi wa kutupeleka huko. Alipokuwa anawaandaa kina Kigi Makasi na Tegete mkasema anawapeleka watalii kambini. Kubalini ukweli kwamba hamwezi kutoka kwenye mpira wa tia maji tia maji na kutwaa ubingwa wa Afrika katika miaka miwili au minne.
Katika timu za Afrika Ghana ndio walikuwa na wachezaji chipukizi na ndio waliofanya vizuri zaidi. Habari ndio hiyo!
Swali zuri Mdau,
ReplyDeleteTanzania tunahitaji kila mchezaji awe na Mganga wake wa Kienyeji. Kwa utaratibu wa sasa, Timu nzima inakuwa na Waganga kama 3 ambao wanashughulikia wachezaji 23.
Ni dhahiri kuwa hawa Waganga wanashindwa kujua mahitaji ya kila mchezaji kikamili, hivyo kuweka kila mchezaji kuwa na mganga wake itaboresha sana mahusiano baina yao.
Ukiondoa hilo, mbinu hii pia itaongeza ajira kwa waganga wa kienyeji wengi ambao wamejaa nchi nzima.
Naomba kuwakilisha.
Mdau.
Mimi kwa upande wangu kama mtu ninayeishi kwasasa huku ulaya,,naona vitu vinavyosababisha timu zetu kutosonga mbele nivingi,,huku ulaya kuna shule za mpila,,tena hata timu za watoto zinalipa mshahala,,halafu timu za taifa unakuta ziko kama tano yani 1....mpaka 5 kutofautiana na umli,ndio maana mchezaji mzuli huku ulaya anaonekana tangu utotoni kabisaaa,,akija kufika juu ndo inatokea kuwa wachezaji wazuli.Kitu kingine wachezaji wanaheshimiwa kila sehemu na wanafurahishwa kwakila kitu ili kupenda kazi yake zaidi,na mchezaji wahuku nivigumu kuwa na mambo mengine tofauti na soccer,nimambo meengi tu tofauti na huko kwetu,,Sasa nikiludi huko kwetu majuzi nilisikia eti mchezaji mzuli hapo bongo hawezi kupewa hata laki nane kwamwezi kipindi kunawafanyakazi hapo wanapata mshahala zaidi hata milioni kwamwezi,,na ukumbuke kuwa huku ulaya penyewe wachezaji wanapewa mshahala yao kila wiki sio mwezi!Halafu majuzi nilisikia eti timu ya taifa ya Burundi ilisafili na gali na chenyewe kibovu kwenda kucheza Uganda mpaka kikahalibikia njiani mpaka wakachelewa hata mda wakupumzika,,bado mazoezi,,hapo utasubili ushindi kweli?mchoko wa hicho ki hiace wenyewe hoyi.Halafu hasa hizo nchi zetu amabazo hazijawahi kudhubutu hata kukanyaga kombe la dunia hawathamini maisha ya timu,,Ushahuli;Anzisheni makundi yamichezo kuanzi shule zamsingi mpaka mpate timu angalau hata 3 za taifa hapo mtachambua kutokea shule za msingi,,Nahapo mtenge hela za kazi hiyo yani mishahala na vingine,,pia ongezeni mishahala yawachezaji selikali iwaheshimu kama wengine,ni hayo ngoja niwapishe wengine.Mdau wa Marseille.
ReplyDeleteIli Tanzania iweze kushiriki kombe la Dunia ,miaka nane ijayo kuna mambo yakufanya mengi lakini haya yafuatayo ni lazima:
ReplyDelete1. Tuwekeze katika academy, ikiwa ni pamoja na kila club kuwa na academy yake.
2. Tufanye ligi yetu iwe ngumu, ikiwa ni pamoja na kuondoa kupanga matokeo,ushirikina na kuwa na marefa wa aminifu.
3. Tuipe Taifa stars,mechi nyingi za kirafiki za kitaifa...hasa nje ya nchi--ili iwe imara na wachezaji wetu waonekane na kupata nafasi kucheza katika vilabu imara Ulaya..ili waweze kuisaidia Stars
4. Wachezaji wabadilike, wawe na ari ya ndinga,heshima na wajitume zaidi
5.Tufanye link na timu kubwa duniani,ili tuwapeleke makocha wetu kujifunza huko na timu zetu,zinolewe na makocha wazawa wenye ujuzi na wanaolipwa vema kama tunavyolipa wageni. Tuanze kuwaamini Watanzania wenzetu.
Nafikiri wadau watachangia zaidi,lakini haya na mengine kutoka kwa wadau yanaweza kuwa chachu.
Kampuni
Norway
Makwaga ndugu yangu,
ReplyDeleteTuna safari ndefu sana kama tunautaka kucheza jabulani la ukweli......Nadhani mpaka sasa hatuna uongozi wenye maono na nia ya dhati katika chama chetu cha mpira.
Hakuna mipango endelevu ya kujenga mihimili mikuu ya mpira (waalimu, waamuzi, Viongozi wenye uwezo ktk sector zote za Jabulani, vilabu, mifumo ya utawala na miundo na kalenda za michuano mbali mbali).
In brief we don't have profession, Skilled, committed and people with integrity to run our Jabulani system
Naomba ufahamu kuwa TFF hawapo pale kwa ajili ya kuratibu mambo hayo hapo juu, wote wa nia zingine kama pesa, kuua jabulani kwa kuzijengea mazingira ya upendeleo Kijani na nyekundu n.k.
Maximo anaondoka wengi umesikia wakimlaumu sana, lkn nakwambia kweli amefanya kazi yake kwa mafanikio sana hasa ktk kujaribu kuingiza timu yetu ktk muundo wa undeshaji jabulani wa kisasa...matokeo mazuri yanaazia mbali sana. 90% wachezaji tulio na leo Maximo amewainua toka chini sana k.m. tegete, Nurdin Bakari, Makasi, Bony, Nizar, Joseph, Maftah, Kazimoto lkn sio hao tu. Nijuavyo mimi National team inatengenezwa na vilabu bora vingi na league yenye maadili, taaluma na ushindani sana kutoka 99% mikoa ya Tz kwa ujumla..hii inampa mwalimu wa timu ya taifa uigo mpana wa kuchagua wachezaji wazuri.
Kikwete, NMB, Serengeti na wapenzi wa jabulani wa Tz hawataweza kuonja raha ya jabulani mpaka mihimili mikuu ya jabulani la kileo itakaposimama sawasawa na itakapofanya kazi kwa ufanisi.
Ee Mungu mwingi wa rehema, mjaalie rais wetu JK maono ya kuwawajibisha wahusika wakuu wa matatizo na hujuma za jabulani hapa Tz...sisi waTz tuna vijana wengi wanaoweza kuwa vinara kama Gyan, Folan, David Villa na Mesut Ozil. Amin
wengine hatuna starehe zaidi ya kuangalia jabulani lkn haitoshi kuangalia timu za wenzetu tu..sisi pia tunaipenda nchi hii na jitihada zake za kujikomboa ikiwa ni pamoja na sector ya jabulani.
By PM
Good topic, mi naona clubs zetu za hapa nchini ziwe na football academies kwa ajili ya vijana wadogo, badala ya kuchukua wachezaji kutoka kenya, congo, rwanda, na nigeria...tukiwa na wachezaji wa hapa wadogo kwenye club zetu tutafanikiwa...
ReplyDeleteJibu ni kuwekeza ktk soka, kuanzia miundo mbinu hadi uongozi. Lazima kuanzia kwa watoto wadogo na tusiingize siasa katika soka kama ilivyo sasa.
ReplyDeleteMiaka 8 ijayo bado tutakuwa watazamaji kama ilivyo sasa...
ReplyDeleteLakufanya ni kuwapoteza wote waliokuwepo katika safu ya Michezo haswa viongozi.Kisha kuweka watu wenyenia na Upendo kwa manufaa ya nchi.
ReplyDeletePia vipaji visichukuliwe kwa kufahamiana.Kwani wanaofahamika wengi hawanavipaji bali wanafahamika tu.
Tanzania inabidi tuanze kujiimarisha kwanza katika mashindano ya Zone(Challenge cup ya Afrika mashariki).Baada ya hapo ndipo tupignie kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika.Tukishaweza kushiriki Afrcan Cup of Nations ndipo sasa wazo la World Cup liingie akilini.
ReplyDeleteNinavyoona tukijipanga sawasawa tunaweza kushiriki African Cup of Nations mwaka 2014.Then we can try to enter into the World Cup in 2022.
inabidi serikali ianzishe academy football kama nchi ya ivorycoast na west africa nyingine wanashule za bording za mpira wanawachukua vijana mitaani kuanzia age 8 na kuendelea kuwapeleka kwenye hiyo shule football ni 60% na masomo ni 40% kwahiyo wanakazania mpira zaidi kuliko masomo.na ikifika wakati wa rikizo kama unata kurudi kwenu au unataka kubaki shule ni uamuzi wa mwanafunzi. na shule inakuwa na kila kitu kinachousu michezo kuanzia uwanja mzuri sehemu ya mazoezi na madaktari.wanachukua makocha toka nje kuwafundisha hawo watoto jinsi ya kupass football,technics,na kila kitu ndio maana ivorycoast ni wazuri sana.aslimia 85%ya wachezaji wametoka kwenye hiyo academy, wanapelewa kwenye team za ulaya kwa majaribio wakiwa na miaka kuanzia 16 kwa majaribio kama team za ulaya zimempenda mchezaji wanailipa hiyo academy kiasi fulani cha pesa kuanzia pound500,000.ndio maana wachezaji kama kolo toure arsenal walimchukua kwa pesa ndogo toka hiyo academy. yaya toure naye alichukuliwa na monaco kwa psa ndog.salomon kalou alichukuliwa na fayanood kwa pesa ndogo na wengine wengi tu. bila serikali kujenga football acedemy hakuna kitakachosaidia mpira hapo tanzania ni mimi mdau wa texas
ReplyDeletewewe una ndoto, yaani sisi tunapenda sana ku simplify mambo. Hivi unafikiri miaka nane tunaweza kweli kuwa kwenye kombe la dunia?
ReplyDeleteHakuna hata program moja ya kukuza vipaji Tanzania. Hii ni project ya miaka 20-25 kama kweli tunataka kuwa kwenye kombe la dunia.
Inabidi tuanza kuangalia mambo kwa mapana na marefu. Wewe unataka kukata short cut tu tuingie kombe la dunia miaka nane ijayo halafu itakuweje huko? Tupigwe 8-0 kwenye mechi zote?
Kama ni kuingia kombe la dunia ni kuingia kwa nia ya kushinda kombe la dunia hiyo ndio iwe nia. Nafikiri nchi nyingi kama sio zote za africa nia ni kuingia (qualify) kucheza kombe la dunia lakini Hatuna mikakati ya kushinda kombe la dunia.
Ukiangalia nchi zinazoshinda mikakati imeandaliwa miaka mingi. Angalia kwa mfano nchi kama Germany mwaka huu, imeandaliwa miaka mingi kuna shule kule Ujerumani ya kuwekeza kwenye vipaji vya timu ya taifa. Matokeo yake tunaona sasa, wanagawa dozi za 4-1, 4-0 mwaka huu. Mipango ni muhimu jamani hatuwezi kushinda tu kienyeji.
mdau swali lako zuri tu na halitokosa jibu. jibu mojawapo ni kuwa WACHEZAJI WAACHE NGONO TU NA TIMU IPATE VIONGOZI WASAFI BASI ITAFIKA. TUSIWEKE KULA MATUMBO YETU TUYARUDISHE NYUMBA BAADA YAKUYATANGULIZA......
ReplyDeleteJibu la kizushi;Sisi tuite wageni waje watuchezee mpira katika timu yetu ya Taifa wakati wenyewe tunaangalia tu kama kawaida yetu.Ndo iliyobaki.
ReplyDeleteJawabu tanzania nayo ijitowe katika mashindano yote ya kitaifa kwa miaka miwili kama wanigeria. Miaka hiyo miwili itumike kuinua kiwango cha walimu na wachezaji pamoja na viwanja vya klabu mbali mbali mjini na vijiji pamoja na kutafuta wachezaji bora mashuleni.
ReplyDeleteHivi Makwanga ndugu yangu umeangalia ligi za Tanzania mara ya mwisho lini? Ungeangalia mpira tunaocheza wala usingepoteza hata muda wako kuulia swali lako.
ReplyDeleteUnless kombe la dunia linauzwa, then najua tutauza mpaka nchi ili linunuliwe.
Ila as long as mpira unaendelea kudunda na watu watu weupe wanaendelea kusimamia utaratibu wake; na sisi wabongo tunandelea kucheza na maisha wala sitegemei kuiona TZ kombe la dunia hata miaka 30 ijayo.... With confidence I can bet on this
Mpira ni pesa...Bongo badala ya pesa kutumika kuendeleleza vijana wadogo ili kujenga timu bora ETI NAO WANAJIFANYA KUNUNUA WACHEZAJI TOKA KENYA,NIGERIA, RWANDA AU BURUNDI!!!YAANI KIAKILI BONGO NI ZERO.LINI TUTATHAMINI VYA KWETU NA WATU WETU....HIVI UFAHARI NI KUWA NA WACHEZAJI WA NJE KWELI....HOVYOOOO.Wenzenu England wanaaaaaajuuuuuuuuuta.
ReplyDeleteMdau wa London.
Tanzania inabidi igombanie kuHOST wORLd CUP 2022 hapo ndio itakuwa njia rahisi na sisi kushiriki vinginevyo itakuwa ndoto.
ReplyDeleteKuna mjadala wa hili swala nilikuwa naufuatilia http://bongoline.com/forums/Sports--Entertainment/228-Are-East-Africans-football-flops.html
ReplyDeleteWadau walikuwa wanajadili documentary ya BBC titled "ARE EAST AFRICAN FOOTBAL FLOPS?" Interesting
Huu ni mjadala Mzuri na ninapenda kuchangia yangu machache.Tanzania Kuingia fainali za kombe la dunia miaka 8 hijayo,mambo haya yanatakiwa kufanywa.
ReplyDelete1.Tafuta kocha mzuri na kumpa lengo kuwa ndani ya miaka 8 tunaingia fainali hizo.
2.Kuanzishwe academy,na wachezaji watakao chaguliwa wacheze pamoja/kukaapamoja kwa muda mrefu kama team,ili kujuana kimchezo na tactical pia.
3.Mechi nyingi za kirafiki na inchi za mabara yote.
4.Tuanze kuwatafutia wachezaji wetu kazi za mpira,hata kama ni Japan.Ni muhimu kwa inchi kwenda mbali,sio kuishia kwenye group stage.
5.Hili ni upende usipende.Uwekezaji kwenye ligi ya nyumbani,wachezaji,teams na mchezo wenyewe.
Ndiyo hayo tu.Unahitaji yote 5 kwa pamoja.
Tu-import wachezaji toka nje ya nchi. Angalia Ujerumani, kuna wachezaji kibao wasio wazawa wa Ujerumani. Ufaransa, Ureno, Uholanzi, Marekani, wote wanatumia wachezaji immigrants katika kufanikisha juhudi zao za soka kitaifa. Hapa bongo wachezaji wetu walio wengi hawana lishe wala vipaji vya kulipepeta kabumbu. Tuende kenya, Zambia, Rwanda na hat aUlaya ya mashariki na kuleta vijana wadogo wa umri wa miaka 16 na zaidi ili miaka mine ijayo TZ nas tuonekane kule Brazil.
ReplyDelete