Mh. Emmanuel Ole Naiko akitoa shukurani baada ya kuchaguliwa bila kupingwa kuwa Makamu wa Rais wa shirikisho la Taasisi za Uwekezaji duniani huko Buenos Aires Argentina.
Mh. Emmanuel Ole Naiko akiwa na Raisi wa Taasisi hiyo kubwa duniani
kwa Upande wa Uwekezaji aliyechaguliwa kwa mara ya pili bwana Allessandro
Texeira kutoka Brazil. Picha na habari na Pendo Gondwe

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini, bwana Emmanuel Ole Naiko, kwa mara nyingine tena amechaguliwa bila kupingwa katika nafasi ya Umakamu wa Rais wa Shirikisho la Taasisi za Uwekezaji duniani (World Association of Investment Promotion Agencies (WAIPA) lenye makao yake Makuu nchini Geneva Uswisi.

Uchaguzi huo ambao ulifanyika hapo jana mjini Buenos Aires Argentina ulishirikisha wanachama wa WAIPA kutoka Taasisisi za Uwekezaji zipatazo 250 kutoka nchi zaidi ya 150 duniani kote.
WAIPA ndio shirikisho kubwa kabisa duniani linalosimamia taasisi za Uwekezaji duniani na lilianzishwa na Umoja wa Mataifa chini ya Usimamizi wa UNCTAD huko Geneva likiwa na mamlaka ya kusimamia na kupanga mikakati na mbinu zitakazoongeza na kuboresha Uwekezaji na Mazingira ya Uwekezaji duniani.

WAIPA pia ilianzishwa kwa lengo la kusaidia na kutoa Ushauri kwa taasisi za Uwekezaji duniani ili ziweze kuzishauri serikali zao kuhusiana na kuundwa na kutengeneza sera na mikakati mizuri ya kuweza kuvutia wawekezaji.

Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo pia ulimchagua tena bila kupingwa Alessandro Teixeira kutoka Brazil kuwa Rais wake ili aweze kuongoza WAIPA tena kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. I personally congratulate the guy for being elected without no opposition to lead a such important entity in the world,let your election be an impetus to bring many modern investments particularly best roads...we need highways to ease congestion especially in Dar es salaam and high tech industries and all other types of industries you can name to hire our graduates.We can if we plan good and stick on the plan.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2010

    Thanks Michuzi for this.

    The story tells us the winning, but does not tell us if Ole Naiko deserves that. We all know he has been there for the past term.

    WHAT DID HE DO!? HOW DID HE USE THAT OPPORTUNITY FOR TANZANIAS' DEVELOPMENT?!

    TUNATAKA KUJUA ALITUMIA NAFASI HIYO (KIPINDI KILICHOPITA) KUIFANYIA NINI NCHIYETU NA SI KWA JINA TU KUWA MAKAMU ANATOKA TANZANIA. LAH SIVYO TUSICHEKELEE YASIYOTUFAA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...