TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA JAPANI
Kamati ya uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya watanzania wanaoishi Japani inapenda kuuwatangazia wanajumuiya wote kuwa UCHAGUZI wa VIONGOZI wapya wa Jumuiya utafanyika JUMAPILI, TAREHE 01/ 08 / 2010 katika ukumbi wa ODASAGA PLAZA-Odakyu Sagamihara Station kuanzia SAA 11.45 jioni. Tume inawakaribisha wale wote wenye SIFA na wanaopenda kuongoza Jumuiya yetu kwa kipindi cha MIAKA MIWILI ijayo kujitokeza.

Sifa za mgombea:
1. Awe na umri usiopungua miaka 18.
2. Awe mkazi, wenye anuani na namba ya simu
3. Awe mwanachama HAI na amelipa ada ya uanachama hadi mwezi wa 8, 2010.
4. Alipie ADA ya kuomba kugombea
a. Nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya Yen 5000/-
b. Nafasi zingine Yen 3000/-

Nafasi zilizo wazi:
1. Mwenyekiti
2. Makamu Mwenyekit
3. Katibu Mkuu
4. katibu Mkuu Msaidizi
5. Mweka Hazina
6. Makamu wa Mweka Hazina

Kamati inawaomba wale wote wenye sifa na wanaopenda kugombea nafasi hizo wawasiliane na wana kamati wafuatao:
1. Mwenyekiti kamati ya uchaguzi Bw Amani Paul: 080-4200-0684
2. Katibu wa kamati ya uchaguzi Dr. Kamugusha Kazaura: 090-8581-9202
3. Wajumbe wa kamati ya uchaguzi:
i. Mama Mariam Nyangasi: 080-3413-4942
ii. Bi Upendo Mwimbage: 080-1326-9700
iii. Mr Amarilo Kilinda: 080-3721-1868
iv. Mr James Ngereza – 090-9845 9699
Ahsanteni.
Paul Amani, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2010

    Haya ndiyo mambo tunayotaka kusikia kuunganisha watanzania,sio wale walioshindwa maisha sasa wanafungua matawi ya CCM kwenye nchi za watu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...