

Haya DJs walikuwa, na bado ni watu muhimu katika shughuli za muziki Tanzania. Labda nikupe maelezo mafupi. Baada ya Biribi Discotheque kupumzika, akazuka kijana huyu, kwanza kwenye parties maeneo ya Upanga, na baadaye kuwa DJ maarufu aliyejulikana kama Dj Emperor, akiburudisha sana pale Motel Agip na kisha kuhamia ghorofa ya saba New Africa Hotel. Alifanya mambo makubwa Arusha pia. Wapenzi wa disco mnamkumbuka? na disko lake liliitwaje? Anauliza mwanamuziki nguli na mwana libeneke aliye juu katika tasnia ya muziki John Kitime a.k.a JFK. Kwa haya na mengi mengine katika muziki wa bolingo hebu mtembelee BOFYA HAPA
Huyo ni Big JOE Joseph kusaga enzi zake alipokuwa Dj na DISCO lake la mawingu ambalo baadae lilijigeuza na kuwa redio pendwa kwa sasa hapa bongo ikiitwa mawingu redio,mkidhungu unaweza kuiita REDIO CLOUDS a.k.a. REDIO YA WATU,na big JOE kwa sasa si DJ tena bali ni mkurugenzi wa REDIO hiyo pendwa.Hongera bwana JOE a.k.a. Big Boss,toka u dj mpaka ukurugenzi mzee pana hatua
ReplyDelete