Ankal
Mambo ni aje. Naona watani wajadi wametunanihii kwenye libeneke la Google transalation. Ukiandika "Natoka Tanzania" ina translate "I am from Kenya"....
Angalia link hapa chini.
http://translate.google.com/?hl=en&tab=wT#swenNatoka%20tanzania
Naomba uitundike ile watu waliobobea mambo ya teknohama wawaandikie Google walirekebishe
hili tatizo.
Mambo ni aje. Naona watani wajadi wametunanihii kwenye libeneke la Google transalation. Ukiandika "Natoka Tanzania" ina translate "I am from Kenya"....
Angalia link hapa chini.
http://translate.google.com/?hl=en&tab=wT#swenNatoka%20tanzania
Naomba uitundike ile watu waliobobea mambo ya teknohama wawaandikie Google walirekebishe
hili tatizo.
PS: Pole na macho kucheza winga.....
Mdau Japani
Hakuna tatizo, wewe ndio mwenye matatizo, nimejaribu haina matatizo japo kuwa inatafsri mbovu
ReplyDeleteim so sorry for the language this is bullshit it will never happen on google i work for them and what i can say that guy a is Kenyan and talking crap
ReplyDeleteMwenye kutuma hii post ndiye mwenye shida. Google haina shida. Anataka watu warudie yale ya Paulo Kamau. Nahisi ni Mtanzania anayetaka chokochoko na Wakenya... Wadau tujihadhari na watu wakuleta uchochezi...
ReplyDeleteKaka hiyo google translate ya wapi?? Mbona sioni hayo matatizo unayosema! labda ulichemka mwenyewe
ReplyDeletemdau ni kweli kabisa. Hii ni aibu tupu.google wajirekebishe
ReplyDeleteMalisaBG
Ankal, post nyingine za watu kama hawa zinatupotezea tuu stimu zetu! Achana nazo, hajui alilokua anataka kuandika.
ReplyDeleteSi hiyo tu. Yaani sentensi yoyote unaweka yenye "TANZANIA", translator inasema "KENYA". Huu ni uhuni mkubwa. Kama wamefikia kiwango hiki wanaweza hata kuua. To hell with EAC. Nyang'au ni nyang'au tu.
ReplyDeleteHuyu Mdau hana chochote ni chokochoko tu.. kwa hiyo GOOGLE NI YA WAKENYA??? Makubwa...
ReplyDeleteWewe umetumiwa link unafungua na unachopata unaamini? Huwezi kujiuliza huyu jamaa kinachochea fikra hasi zake ni nini kama siyo chuki binafsi na Wakenya tena kwa pamoja?
Huyu aliyetuma hii link anayake na wakuulizwa siyo Google ni yeye mwenyewe. Uzushi mtupu!
Aliyetuma Post kachanganyikiwa check hii link ya google ya Kenya:
ReplyDeletehttp://translate.google.co.ke/#auto|en|Natoka%20Tanzania
Enter text: Natoka Tanzania
Swahili to English translation:
I come from Tanzania
Kwa hiyo aliyetuma post yeye iko tatizo kwenye kichwa yake.
Google iko tafsiri maneno na sio majina.Kwa hiyo ,kama iko yeye fanya sisi au Google jinga,yeye ndio jinga.
From Nairobi.
Kwanza siku zote tafsiri ya lugha inafanywa kwenye maneno na sio majina ya sehemu au mtu.
ReplyDeleteUkishagundua hilo wala huumizi kichwa.Huyo aliyetuma post kichwa chake kina matatizo na inabidi akapimwe akili ili kujua kama iko sawa.
SASA NYIE MNABISHA NINI WAKATI HATA HAMJAJARIBU....MIMI NIMEJARIBU NA NIKAONA NI UKWELI, KWA MFANO UKIANDIKA TANZANIA YETU - GOOGLE INATRANSALTE KUWA OUR KENYA, PENDA TANZANIA - TRANSLATES TO LOVE KENYA.........MSIWE WABISHI BILA SABABU YA MAANA
ReplyDeleteMimi nimeandika "tanzania kesho" inaleta "kenya tomorrow".
ReplyDeleteNI hayo tu.Ila kwa uganda hakuna tatizo.mimi najiuliza hawa watu wanatutakia nini sisi.Na ningependa hata hiyo EAST AFRICA isiwepo..nasema hivi kwa uchungu mkubwa.HAWA SIO MARAFIKI KABISA.NI SAWA NA URAFIKI WA PAKA NA PANYA.
Haohao wanaotuhujumu sis Watanzania ndio wanao-post hapa kuwa hakuna tatizo. Nyang'au wakubwa nyie. Uzuru ni kwamba ukitafsiri kutoka English kwenda Swahili unapata tafsiri sahihi. Watalii wanahitaji kutafsiri kutoka English kwenda Swahili. Nyang'au ni nyang'au tu.
ReplyDeletekuna vitu viwili.
ReplyDelete1- google translater
2- google translate
ukitumia translater ambayo ni namba 1 inatoa tafsiri sahihi
na ukitumia namba 2 inatoa tafsiri isiyo sahihi hii ni link:
http://translate.google.com/?hl=en&tab=wT#sw|en|tanzania%20yetu
watu wengine wanakurupuka na kuanza kuandika comment bila hta kujaribu, ni kweli kabisa anachosema mdau,ukiandika Tanzania inatafsiri kenya, jaribu nipo tanzani-am in kenya,karibu tanzania- about kenya!!!ambaye hajapata hizi tafsiri hajui kutumia google translator
ReplyDeletemdau
Birmingham
Mimi nimejaribu sasa hivi 19.36 Uk time, nimeandika "natoka Tanzania" inasema "departed from Kenya". Haya Tanzania iwe Kenya jamani?
ReplyDeleteHah jana nilijaribisha ninatoka Tanzania ikaleta the correct meaning..wala sikuweka comment yeyote nilizania kijana analeta longo long tu hapa...Leo nimeweka Tanzania yetu ikasema Our Kenya ...lol....heeeeee ....Love thy neighbor!!!!!
ReplyDeleteJamani kuna tatizo hapa huyo jamaa hajachanganyikiwa, jaribu kutumia capital letter wakati unaandika neno la kwanza pia wakati unaandika Tanzania inakuja vizuri. ukitumia herufi ndogo kote inaleta Kenya!! Ila kwa google lazima warekebishe hii haipendezi hata kidogo.
ReplyDeleteMnajua sio mnakurupuka tu HAPA kuna tatizo Google wanapaswa kujua hili na kurekebisha. Link ni http://translate.google.com/ ukiandika - natoka tanzania unapata - departed from Kenya na ukiandika Natoka Tanzania unapata - I come from Tanzania. HAPA utofauti wake uko kwenye herufi ya kwanza katika kila neno. Kuna uwezekano mkubwa kuna jamaa katumia Contribute a better translation Link kufanya upumbavu wake kuwapotosha watu na lugha yake mbaya, hii ni mbaya sana GOOGLE WANAPASHWA KUJUA NA KUREKEBISHA
ReplyDelete