Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Zanzibar, Stewart Hall, kutoka Uingereza akisaini mkataba wa miaka mitano wa kuifundisha timu hiyo katika hafla iliyofanyika kisiwani. kushoto kwake ni Rais wa Shirikisho la Soka la Zanaibar (ZFA) Ali Ferej Tamim
Rais wa ZFA Ali Ferej Tamim akisaini mkataba huo
Ali Ferej Tamim akipeana mikono na kocha
Stewart Hall baada ya kutia saini mkataba
Kocha Stewart Hall akizungumza baada ya kutia saini mkataba wake.
Habari zaidi za kocha huyu:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2010

    Tanzania ina makocha wazuri tu ambao wanaweza kufundisha vizuri na kuiwezesha timu kuingia world cup. Sio hao wazungu wachovu kutoka Little Wallop na kujifanya wanajua soka. Mtajiju!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2010

    Ni hatua nzuri ya kuleta mapinduzi ya soka la Zanzibar, lakini kumpa kocha mkataba wa miaka mitano ni mingi mno! angepewa angalau miaka miwili kwanza halafu atazamwe, akifanya vizuri aongezwe polepole, lakini miaka mitano ni mingi mno na lolote laweza kutokea kabla. Kuna hatari mkamchoka huyo bwana ndani ya miaka miwili

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2010

    EBOOO JACKY PEMBA KAIBUKIA KISIWANI ZENJI???BIG UP KAKA KWA KUSAIDIA SOKA LETU NAJUA U GOT THE POTENTIAL TO MAKE OUR SOCCER GROW...PAMOJA SANA MDAU

    MDAU MAC T, PPF TOWER

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2010

    Wewe unayesema kuna makocha wazalendo huna kumbukumbu hata kidogo au baba yako ni kocha wa kizalendo! Makocha wa kizalendo tupo nao miaka zaidi ya 40, toka nchi hizi zinapata uhuru wamezipeleka mara ngapi timu zetu kwenye fainali za kombe la dunia? Ili upate maendeleo ya aina yoyote lazima uujue uimara wako na mapungufu yako. Kwenye mapungufu omba usaidizi wa mtu mwingine.
    Mataifa mengi tu hata yale yaliyoendelea yanatumia makocha wa kigeni, Togo walipelekwa world cup finals na Mnigeria, Gabon wanacheza mpira mzuri sana wanakocha wa kigeni, Tanzania imefikia kiwango cha uchezaji huu kwa kutumia mgeni. Leo hii unataka kutuambia makocha wazawa ndiyo wanaoweza kuipeleka timu kombe la dunia!!! kwako wewe kombe la dunia limeanza mwaka huu!!
    Kwangu mimi nitapingana na mtu yeye atakayeniambia makocha wakizalendo ni bora zaidi kuliko wa kigeni. Lakini naweza kukubali ubora wa mzalendo kwa taaluma lakini siyo kwa 'implementation' kwa sababu katika 'implementation' makocha hawa huchanganya na mambo ya 'kiswahili' ambayo ni majungu.
    Tubadilike tuachane na wivu wa 'kiswahili' mpira ni vitendo na siyo maneno.

    Mdau JJ

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2010

    Taarifa za magazeti zinasema kwamba mheshimiwa kocha huyu mzungu, ndiye atakayepewa mkataba mnono wa miaka mitano na marupurupu kibao, lakini atakuwa na wasaidizi wake wawili wazalendo ambao hawatakuwa na mkataba, bali wataendelea kufanya kazi chini ya huyu mzungu, wakiganga njaa!! Ni yale yale baada ya miaka mitano - timu ya taifa ya England itakuja kucheza na Zanzibar mechi moja ya kirafiki, kiingilio kitakuwa dola 200 na itafungwa magoli 5-1 (mgeni rasmi Rais Dk. Shein) tutapiga makofi, biashara imekwisha!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2010

    we unaesema kuna makocha wazalendo wengi wako wapi hayo majungu kwa makocha wa kigeni nyie ndio mnafanya soka la bongo lisiendelee we ni m2 wa kuogopwa kabisa au we mwenyewe ni kocha wewe kubali maendeleo ya watu kijana wazungu wako juu tu hata ufanye nini kama hutaki shauri yako angalia hapo sauzi makocha wote wazungu kasoro timu za asia tu kwa vile wale wako juu na wanafundishika yaani wasikivu kwanza wazalendo mpira wanacheza mdomoni kabla ya uwanjani na fitina alafu nimegundua wa kwanza we hujui mpira hivyo siwezi bishana na wewe

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2010

    sasa wachezaji wala urojo kabla ya mechi tutafika wapi namna hii..

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2010

    napingana kabisa na wewe anony wa saa 10:03 am. kwa upande wangu kocha wa kizalendo ambao tumekuwa nao siku zote hawapewi nafasi ya kufundisha. wakipewa timu wanaingiliwa sana na viongozi. hilo ni tatizo la kwanza. la pili hawapewi ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau.

    maoni yangu kocha wa ndani wapelekwe shule huko nje kwa lengo la kuja kufundisha nyumbani. halafu kuwepo na utaratibu wa kuwapeleka mara kwa mara kwenye mafunzo kwani kila kitu kinabadilika kutokana na maendeleo.

    maoi yangu yanatokana na sababu kwamba kocha wa ndani anajua zaidi mahitaji ya wachezaji na uchezaji wao kuliko mgeni. hilo ndo limefanya nchi nne za Amerika ya kusini kufikia hatu hii kwenye kombe la sasa la duni.

    huo ni mtazamo wangu

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2010

    Anony Thu Jul 01, 11:14:00 AM unatunyima pumzi, ebu rudi shule ya msingi ukajifunze kuweka nukta,mkato, herufi kubwa, nk.
    Halafu unaonekana una jazba sana, sasa sijuwi wewe ndio mmoja wa hao makocha wasaidizi wanaoshindia urojo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2010

    MNGEJUWA WANAVOFUKUZA WAGENI HUKU NA NYINYI NDO MNAWAKUMBATIA TU. HUKU HAWATAKI WAGENI KABISA WANA-DEPORT KILA KUKICHA, SASA HUWEZI PATA KAZI HUKU KABLA YA MZAWA KAMA KUNA MZAWA ANAWEZA FANYA KAZI HIYO HATA KAMA SIFA ZAKE NI NDOGO KULIKO ZA KWAKO ATAPEWA YEYE, SASA SISI TUNAWAKUMBATIA, INATUBIDI TUAMKE KILA MTU NA KWAO KAMA WANATUFUKUZA HUKU NA SISI TUWAFUKUZE HUKO NA KAMA TATIZO NI WATAALAMU HATUNA THEN TUCHUKUWE MAKUSUDI MAZIMA YA KUTAFUTA WAZALENDO WENYE NIA NA SIFA ZA KUWEZA KUSOMEA MAMBO YETU NA KUWAPELEKA SHULE NA KURUDI KULITUMIKIA TAIFA, AFTER ALL ENGLAND HAKUNA MPIRA WA KUTISHA HIVYO, TECHNICALLY NI WACHOVU NI MEDIA TU NDIZO ZINA-HYPE FOOTBALL YAO HAWANA LOLOTE SI MMEONA WORLD CUP. HIZI AJIRA ZIEENDE KWA WAZALENDO NA KAMA HATUNA TUWAPELEKE SHULE NA IKISHINDIKANA KABISA TUCHUKUWA WATU TOKA NCHI ZA MPIRA SI ENGLAND WABAGUZI NA SERA ZAO MBOVU ZA UHAMIAJI WAKISINGIZIA RECESSION

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 01, 2010

    Jamani nini tena huko minazi? Hawa mnaowaita makocha ni matapeli tu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2010

    Hata rafiki yangu aliniauliza hili juzi. Kwanini hamajiri makocha wanaotoka nchini kwenu? kwavile wnaelewa ugumu na mazingira ya maisha yetu watatufundisha at our own phase.

    Huyo anayesema wazalendo miaka 40 je huyu tunayeona anaagwa juzi yeye katusaidia nini?

    Wazalendo wakipewa kazi hamna anayewaachia pumzi ni kuwa control tu na kuwapa kimshahara kidogo. Mpe mtu mshahara kama huyo wa nje uone atakavyowajibika.

    Kweli tunasujudia watu wenye ngozi nyeupe sana. Na huko lwao walikua wanafundisha high school tunakuja wapa mateam yetu ya taifa.

    Shame on us

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 01, 2010

    Wewe anoy Thu Jul 01, 12:21:00 PM: Kama umwenyimwa karatasi na Her Majesty Goverment seme uweleweke acha chuki za kipuuzi, UK for life kwa wenye kinyago wewe zugazuga wakikumata siku moja unatoka OFLICENCE na 4 Fosters for £2 basi ndio mchezo umeisha. Angalia kipindi UK BORDERFOCE halafu utie akili ili tumbo joto lizidi.
    Now Turudi kwenye Football, Makocha wachovu kama hawa ambao hawana record ni kutokana na dili wanakula hao wajanja, wanaandika kocha analipwa £100,000 a year lakini yeye anapewa contract inaseme £50,000 hivi ndio inavyokwenda

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 01, 2010

    NYINYI NYOOTE NI PUMBA TU HIZO MNAZOZANA BURE TU, HATA UK WENYEWE WANAKOCHA MGENI SEMBUSE SISI!!

    SASA KWA TAARIFA YENU HAO MAKOCHA WA KIZALENDO MKIWAPA MPIRA UTACHEZEWA BAR (BAAA)

    NI BORA HAO HAO WAGENI (siyo lazima wazungu hata wahindi na waafrika wengine) NA WASAIDIZI WAWE WABONGO KAMA KAWA. KAMA POSHO HAITOSHI WAOMBE WAONGEZEWE, SIO KAMSHAHARA KA KOCHA MKUU KALINGANE NA MSAIDIZI - WAPI NA WAPI?

    HAPO NIDHAMU ITAKUWEPO - NANI ASIYE MUHESHIMU ALIYE MZIDI KIPATO (kuna mwenye swali?)

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 02, 2010

    Kwenya interview ya EMANUELL ADEBAYO aliulizwa na BBC anaonaje kuhusu Africa kuwa na makocha wa Kiafrica akasema ni bora hao wa kizungu sababu makocha wa kiafrica wanataka rushwa ili wakuchague kwenye National team au wanataka uwanunulie jezi za masters sasa kama nchi zao ambazo zina mpira mkubwa sana kuliko east african na wanataka kocha wa nje itakuwaje na makocha wetu njaa wa kibongo

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 02, 2010

    Maji shida, umeme shida, ajira shida, elimu shida, afya shida ...lakini fedha za kumajiri kocha wa kigeni kwenye kandakanda zipo kibao...hii ni haki kweli ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...