Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Mohamed Gharib Bilal akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe baada ya kuingia Wilayani Nachingwea.
Wananchi wa Nachingwa wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais Dk. Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Nachingwea katika uwanja wa Sokoine leo mchana
Mgombea Mwenza wa urais ,Dk. Gharib Bilal akiongozana na Mgobea Ubunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe baada ya kupokelewa mpakani mwa Wilaya ya Liwale na Nachingwea wakati wa zaiara yake ya kunadi ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kampeni za kukiombea kura Chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajia kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Mohamed Gharib Bilal, akipokelewa na Diwani wa Viti maalum, Asina Lutumbo na Mwenyekiti mstaafu wa UWT, Anna Abdalah, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine wilayani Nachingwea alipofika kufanya mkutano wa kampeni leo

kwa picha zaidi
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kaka Michu vipi umetubania wana CUF leo tumezindua kampeni hakuna picha wala nini. Lakini Im sure kesho Chadema wakizindua kampeni yao najua patapambwa hapa na mapicha. This is not fair at all

    ReplyDelete
  2. I hate this guy Chikawe.

    ReplyDelete
  3. wewe mtoa maoni wa kwanza, wacha ushamba. Hii blogu ya mtu binafsi, anafanya atakavyo, na anaruhusu kile akitakacho. Yeye kaamua kujiunga na ziara ya mgombea wa chama tawala hivyo ni dhahiri kila ukifungua sait utakutana na rangi ya wakulima na wafanyakazi, nyie wajuvi wa mambo muanzishe gulobu yenu alah!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...