Mgombea Mwenza Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Rufiji kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk. Seif Rashid, wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Muhoro, Tarafa na Kata ya Muhoro, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani
Kamanda wa Chipukizi wa Wialaya ya Kilwa Masoko, Chekeni Omar, akimvisha Skafu Mgombea Mwenza, Mohamed Gharib Bilal, wakati wa mapokezi ya mgombea huyo eneo la Somanga, akitoka Wilaya ya Rufiji kuingia Wialaya ya Kilwa Masoko kuendele na Mikutano ya Kampeni.
Mgombea Mwenza wa Urais Tanzania,Dr. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na wakazi wa Somanga, mpakani mwa Wilaya ya Rufiji na Kilwa Masoko wakati wakazi hao walipokuwa wakimpokea mgombea huyo aliyekuwa akiingia Wilaya hiyo kuendelea na mkutano wa Kampeni.
Umati wa watu, Wakazi wa Somanga wakimzunguka Mgombea Mwenza na kufunga barabara kwa muda ili kumpokea mgombea huyo alipokuwa akipita eneo hilo kuelekea Wilaya ya Kilwa Masoko.


kwa habari kamili
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. jamani naomba mnisaidie .. kwanini viongozi wanachaguliwa wazeee ?
    kwani hatuna vijana ?
    jamani wazee wengine hata kutembea hawawezi sasa wanapewa uongozi ..

    au upeo wangu mdogo ? nisaidieni

    ReplyDelete
  2. Tuzidi kuelemishana wakati wote, hata kwenye blog:

    Mgombea Mwenza Mohamed Gharib Bilal...inaleta utata.

    Iwe:

    Mgombea Mwenza wa Jakaya Kikwete (CCM), Mohamed Gharib Bilal...

    ReplyDelete
  3. Uzee dawa wee mtoto wee uliyekoment kwanza. Kama hujui maana kaulize maana. Halafu usicheze na huyo mtaalamu wa nyukilia!

    ReplyDelete
  4. Nyuklia inaishia kwenye porojo....! wakati Uranium tunayo! Ahmedinajad ananyima usingizi wanaume huko!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...