Meneja Huduma na Bidhaa wa Vodacom, Elihuruma Ngowi (kushoto) akishikana mikono na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari na Utamaduni, Herman Mwansoko katika hafla ya uzinduzi wa semina ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini katika Hoteli ya Giraffe jijini Dar. Wengine kutoka kushoto ni Mshauri wa Miss Tanzania Dk Ramesh Shah na Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.

MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency , ambaye pia ni Mratibu wa shindano la Vodacom Miss Tanzania Hashim Lundenga leo ametangaza majina ya warembo 31 watakaoingia kambini Agosti 16 mwaka huu.

Lundenga ilitaja majina ya washiriki na maeneo wanayowakilisha katika mabano ni hawa wafuatao Ester Dennis na Gloria (UDSM),Shadia Mohammed, Furaha David na Mary Kagali (Nyanda za Juu Kusini).

Wengine ni Bahati Chando, Salma Mwakalukwa na Consolata Lukosi (Kanda ya Kati),Flora Florence, Mary Adam na Angelina Ndege (Kanda ya Mashariki), Alice Lushiku, Irene Hezron na Amisuu Malick (Kanda ya Kinondoni), Genevive Emmanuel, Anna Daudi na Britney Urassa (Kanda ya Temeke), Glory Mwanga, Prisca Mkonyi na Jally Murei (Kanda ya Kaskazini).

Wengine ni Gloria Mosha na Christine Justine (Kanda ya Chuo Kikuu Huria), Flora Martin, RachelSindbad na PendoSam (Kanda ya Elimu ya Juu), Fatma Ibrahim, Buduri Ibrahim na Margareth Godson (Kanda ya Ziwa).

Taarifa hiyo ilisema kuwa warembo wote wanatakiwa kuripoti Agosti 16 saa tatu asubuhi katika ofisi za Kamati ya Miss Tanzania zilizopo mtaa wa Samora na Mkwepu baadaye watapelekwa katika hoteli ya Giraffe iliyopo Jangwani beach ambako ndipo itakuwa kambi yao.

Aidha washiriki wote wametakiwa kufika katika muda uliopangwa na si vinginevyo, mshiriki atakayechelewa kufika bila ya kutoa taarifa atakuwa amejitoa katika fainali hizo.

Wakiwa kambini washiriki hao watapata mafunzo mbalimbali kutoka kwa wakufunzi walioandaliwa pamoja na wataalamu wa nyanja tofautitofauti.

Fainali za shindano la kumsaka Miss Tanzania zimepangwa kufanyika Septemba 11 Jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...