Bongo star search ni moja ya kipindi kinacho rushwa na television hapa nchini Tanzania ambacho kime fanikiwa kwa kiwango kikubwa kabisa kuinua vipaji vya wanamuziki wa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa mwaka jana kampuni ya kutengeneza bia hapa nchini TBL kwa kupitia kinywaji chake kinachojihusisha na maswala ya muziki,Kilimanjaro premium lager. Ilishiriki kama mmoja wa wadhamini wa shindano hilo.
Uhusiano huu mkubwa wa kampuni hizi mbili umetokana na sababu kuu kwamba BSS inahusika kutafuta na kuinua vipaji vya wanamuziki hasa vijana wa umri wowote ambapo Kilimanjaro premium lager kufuatia kauli mbiu yake ya Kufikisha Muziki wa Tanzania Kilele cha mafanikio kwa upande mwingine ina husika na muziki wa vijana wa Kitanzania.
Kilimanjaro premium lager imekua ikunga mkono juhudi za kuendeleza Muziki hapa Tanzania kwa kiwango cha juu.. Ikiwa mdhamini mkubwa kwenye zoezi la kutoa Tunzo za Muziki Tanzania kila mwaka,Tunzo zinazojulikana kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Ndio maana Kilimanjaro premium lager imeona hakuna sababu ya wao kutoshirikiana na BSS 2010 katika kuinua vipaji vya wanamuziki wa Tanzania.
Kilimanjaro premium lager imeandikisha mkataba wa kuwa mdhamini wa Bongo star search kwa kipindi cha miaka mitatu ambayo ni BSS 2010, BSS 2011, BSS 2012.
Washiriki wa BSS watashirikishwa katika mambo mbali mbali yakiwemo mashindano yatakayo kua yanafanyika siku hadi siku katika jumba la BSS KILI HOUSE 2010.
BSS 2010 itakuwa ikirusha hewani kila jumapili saa tatu na robo usiku (3:15) kupitia television ya ITV ikishirikiana na Radio one na magazeti ya The Guardian ,Nipashe.unatakia kufuatilia shindano hilo bila kukosa na pia ni muhimu kupiga kura yako ili kuweza kuwachagua watakao weza kushiriki mpaka mwisho .
shiriki nasi ili kuweza kukamilisha ndoto za wanamuziki wetu.


Wakati, Ukuta; Ndiyo Njia Yetu Sote.
ReplyDeleteHicho kipindi kinaelekea kitakuwa kizuri sana.
HIVI HUYU POULSEN ANA ASILI YA KIDESH?
ReplyDeleteDada lakini waambie wenzio wasiwe watukana watu wetu wakati wa kusaka stars. Tunajisikia vibaya kuona watukanwa mpaka matusi ya nguoni hadharani si ustaarabu. Kama mshiriki akikosea msahihishe kwa upendo, na kama ni kumbwaga mgwage kwa upendo. Vinginevyo hapo siku nyingine hapatatosha.
ReplyDeletehabari kwa watu wote wafuatiliaji wa blog ya issamichuzi.
ReplyDeleteingawa niko nje ya nje lakini najitahidi kufuatilia habari za nyumbani.
nimevutiwa sana kutoa maoni yangu katika habari hii nzuri ya kipindi cha bongo star search.
Nazani kipindi hii ni kizuri na ninakikubali ila kwa upande mwingine tunapaswa kuangalia kama kina faida gani na hasara kwetu.Tukianza kuangalia toka kimeanza. Maana kwa maoni yangu kuliko kumpa mtu hela ni bora kumpa elimu ya muziki ili aweze kuendelea kama ninavyoona katika vipindi vingine kama kile kipindi kinachofanyika kenya ili kuweza kumpa nafasi ya kuendelea mbele na sio kupewa hela ambazo hazichukuwi muda anarudi tena mtaani.Tafadhari kama kilimanjaro mmeamua kudhamini basi iwe kweli sio kumpa mtu gari wakati hana uhakika wa mafuta. tafadhari inabidi tubadilike kwa hilo. Madam Ritha nakushukuru kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia kuinua vipaji lakini msiishie katikati,muwape elimu ya muziki waweze kwenda mbali. niwatakie mafanikio na mataharisho mema.
Michuzi plz mpe salamu Ritha Poulsen
ReplyDeletemwambie kila nikimuona moyo wangu huwa unanisaliti natokea kumpenda ghafla. mmmhhh nimesahau kuwa niko kwenye swaumu.
Anony anayomaindi Rita, demu yupo katika chati za juu. Kama unamaindi kaa mstari wa tatu kwa kuwa kuna The Guardian na Woolworth kabla yako. Ulivamie tu mali za watu. Lakini kwa kweli, demu pia namzimia sana. Aliolewa na Mtasha zamani ndio maana jina lake ni la kigeni.
ReplyDelete