Kocha mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Jean Paulsen (kati) akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitangaza kikosi kipya cha timu hiyo kitakachokwenda nchini Algeria kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Algeria hapo Septemba 4,mwaka huu.kulia ni Afisa Habari wa TFF, Florian Kaijage na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Arusha ambaye pia ni mjumbe wa TFF,Alfa Mgonja wakimsikiliza kwa makini kocha huyo.


Na Woinde Shizza,Arusha

KOCHA wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ,Jean Paulsen amezitaka timu zinashiriki katika ligi kuu ambazo wachezaji wake hawakubahatika kuchaguliwa katika kikosi cha timu ya Taifa kuwafanya wachezaji wao waweze kujituma na kujitahidi zaidi haswa katika kipindi hiki cha ligi kuu ili waweze kuonekana na kuchaguliwa.

Kocha huyo aliyasema hayo wakati alipokuwa akitangaza kikosi cha timu ya Taifa ambacho kinataraji kwenda nchini Algeria kushiriki mechi ya kirafiki dhidi ya timu hiyo ya Algeria ambayo inatarajiwa kuchezwa September 4 mwaka huu..

Alisema kuwa amechagua wachezaji hao kutokana na sifa za timu zao pamoja na viwango ambavyo ameviona kutoka kwa wachezaji hao katika mechi zao chache ambazo wamezicheza.

Alibainisha kuwa wachezaji kwa ujumla wanatakiwa wafuate sheria ambazo wanafundishwa na waalimu wao pamoja na kuzingatia sheria za mpira na kuzingatia mazoezi sana.

Alisema kuwa bado hajamaliza kuchagua kikosi cha timu ya taifa kwani ataendelea kuchagua kutokana na mechi ambazo ataziudhuria na kuziangalia na ataangalia viwango vya wachezaji pamoja na timu ambazo wanatoka na zinavyoongoza.

“mimi nimechagua wachezaji kulingana na timu zao pamoja na ubora wa mchezaji mwenyewe pamoja na uwezo wake wa kucheza mpira,napenda kuwasihi ambao sijawachagua kuwa wanatakiwa wajitahidi sana na wakionyesha ubora nitawachagua wala wasiwe na wasiwasi’’alisema Paulsen

Katika timu hii ambayo kikosi chake kimetajwa rasmi, kinajumla ya wachezaji 26 ambao na katika kikosi hiki kuna baadhi ambao watachujwa na pia katika kikosi hiki hakina tofauti sana na kikosi kilichopita.

Kocha mkuu wa timu hii ya taifa alisema kuwa katika kikosi chake hakumteuwa Kiggy Makasi pamoja ya kuwa alikuwa anauwezo wa kucheza kutokana na sababu za kiafya ambazo zinamsumbua mchezaji huyu.

Kikosi hiki cha timu ya Taifa kinatarajiwa kuondoka Agosti 31 kuelekea katika mechi yao ya kirafiki baina yao na timu ya nchini Algeria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Tunawasubiri kwa hamu. Lini mnakuja? Msijetuaibisha kama wale mabondia wetu wa ambao waliungurumisha bonge ya miayo wakiwa ulingoni, ha haa! Walikuja bila hata gulovu na viatu vyoa mchezo masikini wa Mungu. Wiki chache baadaye tukasikia wamekamatwa na hashishi kule visiwa vya Morishazi! Kama nanyi mambo nd'o ivo, bora mtutonye, tutakula uzi wa 'Lajerii' tupate raha yaan an du trwaa ...

    ReplyDelete
  2. Jamani mwandishi uliendaika habari ya Taifa stars hapo juu tafadhali usipotoshe umma wa watanzania hiyo mechi siyo ya kirafiki ni mechi ya qualification ya CAN 2012.Jamani fuateni kanuni za uandishi kama kitu hujui ni heri uulize kuliko kuandika vitu ambavyo sivyo hivi tunaenda wapi sisi watanzania au ndio wale waandishi non qualified na ndugu yetu michuzi tunaomba ukague hizi habari kabla haujazipost kwa sababu ni aibu kwa mwandishi kuandika kitu asichokijua. Ok ahsante;

    ReplyDelete
  3. Mkuu ungetutajia na majina ya wachezaji wanaounda kikosi ingekuwa bomba sana.

    ReplyDelete
  4. Sasa unapoweka kichwa cha habari 'Kocha wa taifa stars atangaza kikosi chake kitakachochuana na algeria septemba 4' halafu majina ya hao wachezaji wenyewe huwaweki hii habari bado haijakamilika na haikidhi kichwa cha habari chenyewe.Kama habari haijakamilika muweke linki ya kutupeleka kwenye habari kamili.

    Sisi tunategemea habari ikidhi kichwa cha habari na sio kama hii habari.Halafu mchezo na Algeria sio wa kirafiki,mnapotosha umma(wasomaji),jamani fuateni miiko ya uandishi wa habari mimi nategemea habari kabla ya kuwa posted iwe imekamilika na imehaririwa vizuri.
    Nafikiri ujumbe wangu umefika.

    ReplyDelete
  5. ebwana hiyoo mech inafanyika tar tatu sio nne,,,!tutawasubiria tukapige kidedea tar moja na mimi nitakuwa airport kuwangoja,,,one two three viva la tannzanie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...