Libeneke rasmi la JK na Dk. M. Gharib Bilal sasa lipo hewani:

www.kikwete2010.co.tz

Libeneke hili maalumu la Mgombea Uraisi na Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM mwaka 2010 limesheheni habari mbalimbali kama:

· Wasifu wa Wagombea – Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. Mohammed Gharib Bilal.
· Mafanikio katika sekta mbalimbali.
· Sera na Malengo 2010 – 2015.
· Ratiba za kampeni.
· Hotuba maalumu.
· Matoleo ya Habari.
· Video na picha.
· Mitandao ya Facebook,Twitter na Youtube.
Kupitia tovuti hii na mitandao yake utaweza kupata taarifa mbalimbali na kutoa maoni yako.

“ PAMOJA TUZIDI KUSONGA MBELE”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ujumbe wa mwaka huu (2010) " Pamoja Tutafika"
    Ujumbe (2005) Maisha bora kwa kila mTZ
    Ihali takwimu hazidanganyi..........

    Watoto wachanga 130 hufariki dunia kila siku nchini

    na Rahel Jeremia

    WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, imesema watoto wachanga wanaozaliwa nchini kila siku kati yao 130 hufariki dunia kila siku.

    Katibu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni, alisema hayo juzi wakati akizindua mpango wa kitaifa wa kuhamasisha unyonyeshaji watoto maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo.

    “Utapia mlo unachangia kwa kiasi kikubwa vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, hapa nchini tatizo hili linachangia theluthi moja ya vifo ambavyo vinakadiriwa kufikia 130 kila siku,” alisema Nyoni.

    Alisema kwa mujibu wa taarifa ya hali ya afya ya mwaka 2004-2005 watoto 38 wenye umri chini ya miaka mitano kati ya 100 wamedumaa, hali inayoashiria utapiamlo umedumu kwa muda mrefu.

    Alisema ulishaji duni wa watoto katika jamii, unatokana na sababu mbalimbali ikiwemo mila, desturi, imani potofu na jamii kukosa taarifa sahihi kuhusu ulishaji wa watoto, hivyo wazazi waweze kujenga tabia ya kutumia huduma ya afya ya uzazi na watoto ikiwa na maana ya kuhudhuria kliniki ili kuweza kupunguza tatizo hilo.

    Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha unyonyeshaji watoto maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo umewakutanisha wadau mbalimbali wa masuala ya lishe.

    Alisema moja ya changamoto kubwa inayowakabili wadau wa lishe ni usambazaji na uuzaji

    ReplyDelete
  2. Nitawatumikia vijana wa nchi, kwa sababu hakuna vijana walioka hiimilia kama WACCM- Dr. Bilal,

    wengine vijana wote walie kama huko kwenye chama, au chama chengine chochote..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...