Jina la Madaraka Nyerere (pichani) sio geni miongoni mwa watanzania.
Ukiachilia mbali ukweli kwamba yeye ni mtoto wa sita wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kitu ambacho bila shaka kinampa automatic celebrity status), yeye pia ni mwandishi,mfanyabiashara na mtu ambaye huwa hasiti kuelezea hisia zake kuhusu mambo mbalimbali iwe ni katika nyanja za kisiasa,kijamii na hata kiuchumi kila mara fursa ya kufanya hivyo inapojitokeza.

Mwaka jana mwezi wa nne(April) yeye na Jaffar Amin(mtoto wa Iddi Amin-Rais wa zamani wa Uganda) waliingia katika vitabu vya kumbukumbu vya wapenda amani duniani walipokutana kwa mara ya kwanza ikiwa ni ishara ya amani na usuluhisho barani Afrika na kwingineko.

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuzungumza naye kuhusu mambo kadhaa yakiwemo ya kifamilia na pia kupata maoni yake kuhusu mambo mbalimbali.Je,ni kwanini mpaka leo hii hajajiingiza katika masuala ya siasa au uongozi?Anamuelezeaje Hayati Baba wa Taifa kama baba yake na kama kiongozi?

Ana ushauri gani kwa wapiga kura katika mwaka huu wa uchaguzi? Ana mtizamo gani kuhusu viongozi mbalimbali ambao hupenda kumuenzi Baba wa Taifa kwa maneno huku vitendo vyao vikiwa tofauti kabisa? Unataka kujua kwanini alipewa jina la “Madaraka”? Ana ushauri gani kwa vijana kuhusu suala zima la kujiletea maendeleo? Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo kwa ku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. HUWA WANASEMA LIKE FATHER LIKE SON, NA PIA…MTOTO WA NYOKA NI NYOKA! Naamini kila mzazi ana uwezo wa kumuandaa, kumfunda, kumuendeleza, kumfadhili na kumkuza mtoto wake awe angalau kama alivyokuwa yeye lakini zaidi sana, zaidi ya alivyokuwa yeye. Nampenda sana na kumheshimu sana baba wa taifa, lakini nafikiri katika suala zima la kuwarithisha akina Madaraka kile alichokuwa nacho, au ikibidi wafanye zaidi ya alivyofanya yeye, mzee hakufanikiwa. Watoto wake wako mbali sana na alikokuwa yeye. Yamebaki majina tu! Kama Nyerere angekuwa mtu wa kawaida akina Madaraka tusingewafahamu kabisa, tunawafahamu na kuwasikia kwa sababu ya umaarufu wa baba yao. Ona Makamba anachomfanyia Januari, Kikwete anachomfanyia Ridhiwani, Mzee Mwinyi alichomfanyia Dr Mwinyi, Kighoma Malima alichomfanyia Adam, George Bush snr to George Bush Jnr, mzee Nnauye kamwacha wapi Nape,…wengi sana tu..Biblia inasema NABII HUZAA NABII. Wazazi tuna jukumu la kuwarithisha watoto wetu vipawa vya hali ya juu alivyotupa Mungu toka utotoni mwao. Ili legacy yako..kazi yako..fikra zako, huduma yako iendelee lazima uwe na mrithi kutoka katika uzao wako. Hawa wahindi wanaofaidi utajiri wetu hapa Tanzania wanarithishana biashara. Utakuta mwanzilishi wa biashara alikufa mwaka 1900 huko lakini wajukuu na vitukuu wanaendeleza kazi ya ancestor wao kizazi hadi kizazi. Leo tulipaswa kuwa na Nyerere mmoja either Rais au Waziri Mkuu au waziri..ili fikra za baba wa Taifa ziendelee kudumishwa. Tunamwita mwalimu kwa sababu ni kweli aliwafundisha wengi na mpaka leo sauti yake inatufundisha, lakini nafikiri wanafunzi wake wa kwanza na muhimu zaidi walipaswa kuwa watoto wake, na leo wangevaa joho la baba mwalimu na kuendeleza pale alipoishia yeye na kufanya mambo makubwa zaidi kwa ajili ya maslahi ya taifa. Mungu atupe hekima wazazi tuwawezeshe watoto wetu kuendeleza vizuri tulivyonavyo.

    ReplyDelete
  2. Mwalimu aliwafundisha vema wanae ndio maana hawako katika kundi la mafisadi. Mwalimu hakutaka watoto wake Kuingia katika siasa eti kwa sababu ya kufanyakazi za baba bali kwa utashi na nia yao. Makongoro na Rose ni wanasiasa wazuri na waadilifu. Nadhani Mwalimu alifanya vizuri kuwaacha wanae wajichagulie kazi kulingana utashi wao na si kutumia madaraka yake kuwapa nafasi kama hao wanaotajwa. Ila ukweli ni kwamba Tanzania inamuhitaji Nyerere mwingine aje kuikomboa.

    ReplyDelete
  3. Nyerere hakutaka kujenga ufalme wa kifisadi. hao wana ajenda zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...