Home
Unlabelled
Mapenzi Ya Nitesa - Mbaraka Mwinshehe 1972
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ah, jamani! Watukumbusha mbaaaali saaaana!
ReplyDeleteMapenzi yanitesaaaa!
Hiyo, na ile nyingine sijui ya nani ile, inaenda kama hivi,
Rozi waua, Rozi waua,
Jinsi ulivyoumbika suraaaa,
Rozi waua, Rozi waua,
Mwenzio nakuzimia sanaaa
Yaani! Weeee acha tuuuu!
thank youu mdau uliyeshusha hii mambo, nyimbo tamu sanaaa, michuzi wanitesaaa moyoooniiii... tirii ti ti ti tiii riiii
ReplyDeleteMie yanitesa hata sasa, gwiji aliona mbali.
ReplyDeleteDu Ankal yaani umenirudisha mbaaali nikiwa mtoto mdogo miaka ya mwishoni ya 1978-79 , ktk hii posti nimekuta nyimbo ambazo ni:
ReplyDeleteMapenzi Ya Nitesa
Dawa Ya Mapenzi
Kifo Cha Pesa
Mdau
Ughaibuni.
RIP mwinshehe na ahsante kwa rudani uliyotupa ktk muda mfupi uliokaa duniani. wengu wetu tumezaliwa wakati ymshaondoka duniani ila tumekujua kwenye tungo zako nzuri. NI wewe Mbaraka Mwinshehe, Marijani Rajabu, Tx moshi William na Hemed Maneti ndio MAJABALI NA NGULI wa muziki wa Tanzania. Ahsanteni kwa burudani tamu mliyotupa enzi za uhai wenu.
ReplyDeleteNakumbuka alipopita shuleni SAME SEC. akielekea KENYA akatumbuiza ile mmbaya nakuahidi akirudi atapitia tena lakini akh BINADAMU hafahamu siku yake ya MWISHO kumbe anaenda kukifuata KIFO.Mjukuu wa Mzee Sultan (OHIO-USA).
ReplyDeleteAhsante ahsante hao ndio magwiji wa mziki Tanzania bwana. hao ndio wanaojua mziki. Tuletee Hemed maneti basi. hasa maria eeeh, au bunjumbura ya burundi.
ReplyDeleteAHSANTE SANA MDAU ULOTUMA WIMBO HUU. UMENIKUMBUSHA MBALI SANA NDUGU YANGU. INANIKUMBUSHA MIAKA YA 70 WAKATI NASOMA SHULE YA MSINGI KAMUNYONGE MUSOMA (1977-80s).DAH, NIMEWAKUMBUKA SANA WASHIKAJI ZANGU ENZI HIZO. HAKIKA MACHOZI YANANILENGALENGA. MAISHA YALIKUWA SWAFI SANA BYTHEN.
ReplyDeleteRIP MBARAKA MWINSHEHE.
MDAU UGHAIBUNI.
Ahsante sana Mithupu kwa kutuletea na kutukumbusha huyu soloist vocalist maestro Mbaraka Mwinshehe.BINAFSI niliingia muziki wake 1972 nikiwa mwanafunzi , tena buree, baada ya kutuona wanafunzi tukimchungulia madirishani pale social hall, Kibaha.
ReplyDeleteYeye mwenyewe akaomba waalimu waturuhusu tuingie tumsikilize kwa nyimbo mbili.Lakini akaishia kutupigia karibu nyimbo 10 nasi tukaridhika kabisa na kwenda kulala.
Kitendo hiki kinanikumbusha sana upendo kwa vijana kwa gwiji huyu wa miziki.
Ni wanamuziki wachachche sana walioweza kufikia upeo wake katika muziki.
Mkuu umenikumbusha mbali sana. Huyu jamaa alikuwa moto wa kuotea mbali. Sijui kama angekuwepo mpaka leo mambo yangekuaje. Lakini vizuri havidumu. Kuna vingine ambavyo mimi hiniacha hoi kama "hakuna dawa ya mapenzi"
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=-NOKkLco5TM&playnext_from=QL&feature=bf_play&playnext=1
RIP Mbaraka
Mdau Mbezi Louis