Na Malkiory William Matiya

Tatizo lingine linalochangia foleni ya magari ni kutokuwa na barabara za uhakika, barabara ambazo zimejengwa kitaalamu kukidhi mahitaji na wingi wa magari.
Nini kifanyike hapa basi; je ni tatizo la ukosefu wa wahandisi wabunifu wa mambo ya barabara, au pengine ni ukosefu wa mwamko na ubunifu miongoni mwa viongozi wahusika katika masuala ya mipango miji/ city planning? Hapa nitawalenga moja kwa moja watu kama vile meya wa jiji, pamoja na wahandisi wakuu wa jiji n.k au ni tatizo la ukosefu wa fedha za ujenzi wa barabara hizi muhimu za katikati ya jiji ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kero za foleni?
Fuatilia mada hii katika Michuzi Post:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Tatizo kubwa ni city planning kwa ujumla. Kama hiyo plan ipo basi haifuatwi sababu walaji ni wengi. Ukiwa kwenye ndege juu ukiangalia utaona magari yote yanaelekea city centre. Hii ni kwa sababu Biashara na ofisi nyingi zipo city centre. City ikipunguza biashara nyingi city centre itasaidia sana. Kukiwa na shopping centres katika kila wilaya na parking hii itasaidia sana. Wahandisi wakune vichwa namna ya kupanua barabara. Miji mingi ya wenzetu wanakuwa na ring road ambapo gari hazisimami. Hii inasaidia kuharakisha upitaji wa magari pembeni ya city centre. Kwa hiyo kazi kwa Wahandisi.

    ReplyDelete
  2. Mbona mnapenda kurudia mada hizo hizo kila siku, jitahidin kubadilika na kuleta mada zenye kueleweka. Hata kama zikijengwa barabara za juu na chini kama ishirin tatizo litabaki kuwa palepale, hiyo yote ni kutokana na ofis kurundikana sehemu moja basi,na mahitaj muhimu ya watu sehemu moja basi....

    ReplyDelete
  3. Traffic congestion in Dar is the result of poor planing of roads but it is my belief that many roads were and are built thru grants and loans. Thus we have limited choice of making our own judgement and decisions, in design and future expansion or modifications of our roads.The only alternative is to redesign the existing open drainage along the middle and sides the roads.We have to put in place covered drainage so as to make use of the vast amount of the area.Anyway the present open drainage is an eyesore with over grown grass and filth.Lets start using huge pipes underground and abandon the ancient open trenches.

    ReplyDelete
  4. Pia Watumiajimia Wenye uwezo tofauti, wa kufikiri, na busara limekuwa ni tatizo kubwa......

    ReplyDelete
  5. Nimeshangaa jamaa mmoja kakandia kurudiarudia hii mada, ni bora irudiwe hata mara mia, kwani ni kero kubwa sana.
    Kwa tunaopanda daladala tunaiona hii, fikiria mtu unatumia masaa matatu na zaidi kutoka Msasani hadi Gongolamboto, huku mumesimama, mumejazana,...inakera na inaumiza.
    Tumeshuhudia watu wakizimia ndanii ya magari hayo, kupigana, na vituko vya ajabu-ajabu!
    Kiafya inatuathiri sana, na kupoteza muda mwingi njiani, kwani wengine tunawaacha watoto wamelala, tunawakuta wameshalala, sababu kubwa ni hiyo foleni na hasa wakiwepo matrafiki kama ndio waongozaji badala ya mataa yenyewe.
    Mapendekezo yametolewa mengi , lakini hakuna utekelezaji, sasa tukae kimya, tuumie, hapana, turudieni hata mara mia, ili wajue kuwa tunaumia.

    ReplyDelete
  6. Tatizo si sana miundombinu bali tulivyo wabongo. Kila mtu anajifanya kaidi na anajua zaidi. Daladala hawaegeshi kwenye bus bay, magari mengine yanaisha mafuta au yapata pancha inakuwa haki kuzuia wengine maana haifanyiki juhudi kuyaondoa.Hivi kutumia treni toka Ubungo,ukonga na boti toka kawe,kunduchi msasani nk c ingepunguza kero za daladala? na hayo mapendekezo yapo daima ila yamefunikwa.

    ReplyDelete
  7. Kila mtu atasema lake kuhusiana na jambo hili kwa kuwa hali ya kawaida kila kitu tunakiona kwenye makaratasi lakini hakuna utendaji wa aina yoyote. Foleni ya Jiji letu kwanza kabla hatujaenda mikoani inatatulika ila kwa kuwa wenye madaraka hawataki kuongea na wadau ili wapate ushauri wanafanya kile wanachokijua ndio maana bado tunateseka na hizi foleni, unakuta mkurugenzi labda wa jiji hata siku moja hajawahi kupada dala dala au hata kiongozi wa sumatra hata mmoja hajawahi kupanda dala dala sasa je atajuaje taabu ipatikanayo humo au atajua mwanafunzi ananyanyaswa kwa namna gani, nirudi kwenye swala la foleni kwa ukweli kama tunataka kuondoa foleni jiji wafikirie kuweka ushuru kwa magari kwenda mjini kwa mfano, magari ya serikali, waandishi wa habari, dalala na magari ya shule ndio yaruhusiwe pekee kuingia mjini, magari ya watu binafsi yatozwe ushuru wa elfu 15,000 kila aendapo mjini na fedha hizo zijenge miundombinu mipya ya bara bara, miji mingine ya nchi za wenzetu zina bara bara za baiskeli na hata viongozi wa serikali anaweza kwenda kazini kwa baiskeli maalumu lakini kwa kuwa sisi tunaona kuwa baiskeli ni usafiri wa watu maskini basi tutabaki kwenye foleni na maendeleo hakuna mpaka tufe

    ReplyDelete
  8. Bongo hamna vipaumbele, hata planners wangefanya kazi nzuri vp, kama vipaumbele co barabara usitarajie mambo yatakuwa poa. Viongozi wetu wako kwa masiahi yao kuliko ya umma.
    Bro hapo juu anaesema maada hii imechosha, atoe maada yeye anayotaka.
    Ankal ''The beautiful one's are not yet BORN''

    ReplyDelete
  9. Mc Kessy, sie wengine wavaa mashati meupe na suti kila siku baisikeli hatuwezi, fikiria kuendesha baisikeli toka Boko mpaka Posta alafu unatakiwa umfuate mteja Mbagala, alafu urudi ofcini, hivi utatamanika!!!!!
    Nafikiri ni bora 'feeder roads' zingewekewa lami, mfano fikiria ile barabara za Kijitonyama za kupunguza foleni ktk barabara ya Bagamoyo bado ni mashimo ya kufa mtu, hivi hata kuziba wanashindwa au mpaka uchaguzi?????? Pia mabasi makubwa ya kubeba abiria 150 au zaidi yakiwa na muda maalum wa kuondoka nina imani wengi tutaacha magari yetu nyumbani.

    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete
  10. Maoni yote yaliyotolewa hapo juu yana mantiki na yanalenga zaidi katika mipango ya Serikali. Ninaomba kutoa maoni yangu pia kwa upande wa watumiaji wa barabara zetu. Ninaamini kabisa kwamba hata kwa mfumo wa barabara uliopo sasa, tatizo hili linaweza kupatiwa ufumbuzi kwani liko ndani ya uwezo wa watumiaji wa barabara. Msingi mkubwa wa tatizo hili ni kuwa watumiaji wa barabara HATUHESHIMIANI NA WALA HATUFUATI SHERIA ZA USALAMA BARABARANI. Msongamano mkubwa wa magari katika jiji la Dar es Salaam unasababishwa kwanza kabisa na Dala Dala ambazo hupenda kupakia juu kwa juu na hawafuati sheria za usalama barabarani, wao kila wakati ni mashindano ya kuhesabu vichwa tu. Pili ni wale maDereva wanaopenda kutanua na kupita vipembezoni mwa barabara halafu wanakwenda kufunga njia mbele ya safari - huo ni ubinafsi tu wala si sababu nyingine. Tatu ni askari wa usalama barabarani ambao husababisha msongamano kwa kuruhusu magari ya upande mmoja kwa muda mrefu. Hivi kama taa za barabarani zinafanya kazi, kwa nini askari wa usalama barabarani asimame tena katikati kuruhusu magari? Yeye anatakiwa kuwa pale kuwakamata wanaovunja sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na wale wanaopita kwenye taa nyekundu. Nne ni foleni za kusubiria viongozi watoke nyumbani kwenda ofisini, utakuta magari hasa ya upande ule wanakoishi viongozi yanasimamishwa hata nusu saa kabla ya msafara wa kiongozi - hili nalo linaleta msongamano mkubwa. Matatizo mengi ya msngamano wa magari kusema kweli ni ya kujitakia wenyewe na yako ndaNi ya uwezo wetu kuyatatua wakati tukisubiria mipango mikubwa ya Serikali ya kuboresha na kuongeza miundo mbinu. Lazima tukubali kwamba wote in wadau wahusika katika jambo hili na kila mmoja wetu ana jukumu lake katika matumizi bora ya barabara zetu. Kwa misingi hiyo basi, serikali ina jukumu lake, nasi pia kama watumiaji wa barabara tunalo jukumu la kuhakikisha utumiaji mzuri wa barabara hizo ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani.

    ReplyDelete
  11. Kuna mmoja ameongelea ukosefu wa busara hapo juu. Unakuta dreva annamua kufunga barabara mwenyewe na kusababisha foleni. Labda ni kwa kuwa madereva wengi hawajui kusoma wala kuandika, kwa maneno mengine shule hawakuiona kwa hiyo busara zinagomba.

    La pili ningeshauri badara ya kutengeneza barabara za juu kwa juu , serikali itengeneze barabara zetu za mitaani hizi nazo husaidia sana madereva wengine wanapochepukia huko msongamano hupungua. Mfano zile daladala zilizokuwa zikikatisha mitaa ya kijitonyama zilipunguza msongamano sana kwenye barabara ya kutoka mjini kuelekea mwenge. Lakini kasheshe ilianza wakati hizi barabara zilipoharibika kwa nvua na kelele za msongamano ndipo zilizidi.

    ReplyDelete
  12. Ninamuunga mkono Elizabeth kwa asilimia mia. Ametoa hoja kubwa ambayo wengi wetu hatutaki kukiri kuwa nasi tu sehemu ya tatizo. Kwa kupanua tu hoja yake, ni kwamba anajaribu kusisitiza suala tunaliita utamaduni. Utamaduni (kaida ya kufanya jambo fulani) haudondoki kama mvua, bali unajengwa (hususan kwa kufuata sheria na kuhimiza sheria). Wabongo tuna sifa moja kubwa duniani kuwa tu watu wa amani, utulivu , na upendo pamoja na kuheshimiana. Ni utamaduni uliojengwa na misingi ya mfumo wa siasa wa awamu ya kwanza na hadi leo hii umeendelea kuwa mtaji. Ni utamaduni mzuri. Lakini ikija katika utamaduni wa matumizi ya barabara hususan kwa waendesha magari hapo utulivu, upendo, heshima, na amani vinayeyuka. Tunakuwa kama wanyama hivi, kama wendawazimu hivi: si kijana, si mzee, si bosi, si pangupakavu, si mama wala baba, nk kila mmoja anataka kuonyesha kuwa ni bingwa!!!! Kila mmoja anataka kuonyesha ni jinsi gani anavyoweza kuwaziba waendeshaji wengine hata kama wanaelekea upande tofauti na wake. Shame on us Bongoleses!!!

    ReplyDelete
  13. Trafik kuongoza magari sioni kama ni tabu. kwanza sasa hivi madereva hasa daladala hawaheshimu taa za barabarani, mfano angali Ubungo mataa kama hakuna trafik gari yanashonana katika kati ya barabara taa zikiwa zinawaka.
    Kwa ni wakati sasa wa wahusika kuamka, camera za barabarani zitumike ili wakosaji watafutwe wapewe adhabu kali (hasa faini) ili mapato yaongezeke. Jambo lingine wote wanalisema feeder loads zijengwe kwa kiwango cha lami.
    Lakini lingine pia magari makubwa yasiende mjini wakati wa mchana. Na magari makubwa yanayotumia mandela Road yawe na muda maalum wa kutoka, pia ni wakati sasa wa bandari kufanya kazi 24hrs. Magari ya mizigo yaruhusiwe kuanzia saa 3usiku mpaka saa 10, ili by saa 12.00asubuhi yawe yameshatoka mjini.
    Lakini pia waendesha baiskeli wajengewe barabara zao na ziheshimiwe

    Nawatakia utekelezaji mzuri.

    ReplyDelete
  14. 1.JENGENI BELTWAYS KAMA NNE HIVI ( 195/295/35/495) MIJI YOOOTE MIKUBWA HUKU USA INA BELTWAYS ILI KUEPUKA TRAFFIC CONGESTION
    2.JENGENI SUBWAY/LIGH TRAIL WATU WATATUMIA PUBLIC TRANSPORT KAMA ILIVYO NYC NA SIO DALADALA ZENYE MAJASHO NA KUKOSA USTAARABU
    3.PELEKENI BIASHARA/MAOFISI NJE YA JIJI SIO UKITAKA KILA KITU BASI LAZIMA UENDE MJINI
    ....MTASEMA OOOH HELA ZA UJENZI WA SUBWAY HAKUNA. LAKINI HELA ZA UNUNUZI WA RADAR, EPA, ZIPO:)
    GOOD LUCK

    ReplyDelete
  15. Siku tutakapokuwa tayari kujiuliza kwa nini kila mtu anakimbilia Dar ndio siku tutakayopata jibu la kupunguza foleni kwenye jiji.
    Majiji makubwa mnayoyasema ulimwenguni mara yana beltway mara yana skyover lakini bado yana foleni. Jibu ni mfumo mzuri wa usafiri wa umma na kuboresha maisha nchi nzima, sio Dar peke yake. Nani atataka kupanga chumba kimoja Manzese na kuishi kwa kuhanjahanja na kupiga debe wakati anaweza kuwa na kajumba kake kazuri kenye umeme na maji mkoani huku akijipatia riziki kwa njia mbadala?

    ReplyDelete
  16. hii mada ni muhimu wacha irudiwe tu. ila kwa kweli waleta foleni ni madereva wenyewe na si matrafik, matrafik wamejitahidi sana kipindi hiki kukaa barabarani na kukamata watumiaji wa njia za pembeni imesaidia sana,sasa kwa kuwa mkoa umekuwa ni mdogo kulinganisha na idadi ya watu na magari basi tujipange kwa kutumia barabara vituri madereva ni wabinafsi sana wanataka kukatiza tu, kwakweli tukijipanga kwa umakini inasaidia sana foleni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...