Jamani jamani ndugu zangu nisaidie kwa hili:
Baada ya rafiki yangu kupoteza cheti chake cha kidato cha sita na hati ya kusafiria (Passport) alienda kutoa taarifa polisi na kupatiwa RB na baadae alienda Baraza la Mitihani la mtihani pamoja na Migrations wao walimweleza aende kutanganza kwenye magazeti ya serikali (yaani Daily news na Habari Leo) na aende na copy ndipo utaratibu mwingine uendelee. Uhamiaji wao walimwambia anatakiwa kufuata utaratibu ili aweze kupata passport nyingine.
Sasa baada ya kuwa ametangaza alibeba copy zake na kwenda nazo pale Baraza la Mitihani wakamwambia wanashukuru kufanya hivyo ila wao huwa hawatengenezi cheti mara mbili, ila Baraza la Mitihani wanachofanya huwa wanatuma barua ya udhibitisho wa matokeo kwenye ofisi unayokuwa umeomba kazi na unapoomba kazi unatakiwa kuomba na kwao watume barua ya udhibitisho na kila barua ya udhibitisho wa matokeo unatakiwa kulipa tshs. 10,000/=.
Sasa kitu ambacho kinamsumbua rafiki yangu ni kwamba iweje ofisi kama uhamiaji wanauwezo kwa kureprint passport wao baraza la mtihani kwa nini wasiweze kufanya hivyo???
Na pili iweje uwe unalipia tshs.10,000/= kwa ajili ya kupata barua ya udhibitisho kwa kila unapotuma maombi ya kazi???
Naombeni wadau wa elimu mwenzetu anaomba msaada juu ya hili...
blasiokachuchu@hotmail.com
Baada ya rafiki yangu kupoteza cheti chake cha kidato cha sita na hati ya kusafiria (Passport) alienda kutoa taarifa polisi na kupatiwa RB na baadae alienda Baraza la Mitihani la mtihani pamoja na Migrations wao walimweleza aende kutanganza kwenye magazeti ya serikali (yaani Daily news na Habari Leo) na aende na copy ndipo utaratibu mwingine uendelee. Uhamiaji wao walimwambia anatakiwa kufuata utaratibu ili aweze kupata passport nyingine.
Sasa baada ya kuwa ametangaza alibeba copy zake na kwenda nazo pale Baraza la Mitihani wakamwambia wanashukuru kufanya hivyo ila wao huwa hawatengenezi cheti mara mbili, ila Baraza la Mitihani wanachofanya huwa wanatuma barua ya udhibitisho wa matokeo kwenye ofisi unayokuwa umeomba kazi na unapoomba kazi unatakiwa kuomba na kwao watume barua ya udhibitisho na kila barua ya udhibitisho wa matokeo unatakiwa kulipa tshs. 10,000/=.
Sasa kitu ambacho kinamsumbua rafiki yangu ni kwamba iweje ofisi kama uhamiaji wanauwezo kwa kureprint passport wao baraza la mtihani kwa nini wasiweze kufanya hivyo???
Na pili iweje uwe unalipia tshs.10,000/= kwa ajili ya kupata barua ya udhibitisho kwa kila unapotuma maombi ya kazi???
Naombeni wadau wa elimu mwenzetu anaomba msaada juu ya hili...
blasiokachuchu@hotmail.com
Tatizo kwa nchi kama Tanzania lazima upate watu wa kukukwamisha maendeleo, hakuna cha maana sana hapo, na ndio chanzo cha mianya ya rushwa, fikiria passport ilivyo kuwa kitu muhimu lakini inakuwa rahisi kupewa kwa kuwa ulipoteza ya kwanza, baraza la mitihani kuna urasimu mkubwa sana na wana sera za kizamani ngoja hao wajinga wa CCM wakitoka madarakani ndio watajua nchi iko vipi
ReplyDeleteukweli na sheria ni kwamba huwezi kupata cheti mara mbili. cha kufanya ndugu yangu tumia results slip kwani inakubalika duniani kote. hata mm hapa cjawahi kuchukua cheti changu cha form six but huwa natumia results slip kila napoenda. otherwise hakuna optional nyingine japo watu wengi huwa wanatoa kopi ya cheti then unaenda kwa mwanasheria ku certify true copy japo sasa hivi itakuwa ngumu kwani huwa hawakubali hd aone original yake.
ReplyDeletehuo ndio ushauri wangu.
ukiona hivyo labda huyo rafiki yako anafuata sana mstari mnyoofu.kwnn asiongee na mdudu rushwa?ama kama hutaki kutoa kwa njia hiyo basi bora akachonge cheti feki tu.wengi tu wanafanyakazi kwa kutumia docs haramu.
ReplyDeletePole ndugu.
ReplyDeleteYangu ni maoni kwa ujumla kuhusu issue ya kuwa na documents muhimu na matumizi yake mbalimbali kama unavyoeleza hapo juu (birth certtificates/affidavits, Wills etc). Documents za elimu (ngazi zote za elimu) huhitajika in copies na kwingineko in original formats haya yote kuwa issue endapo hizo documents zinaweza kupotea, kuchakaa nk. Je mfumo mwingine unaweza kutumika? Kama baraza la mitihani wanavyosema, iwe unapotafuta kazi, unampa mwajiri "link" fulani wanayoweza kuitumia kuwasiliana na baraza la mitihani electronically kudhibitisha. Huo kama mfumo unaweza kuondoa issue kama hiyo inayompata ndugu yako, pia kuondoa forgeries zinazotangazwa kila siku.
Labda hii inahitaji hoja ya haja/haja ya hoja lakini nakutakia ufumbuzi kwa issue hivi sasa.
KK
Pole mdau ww na huyo rafikiyo..Lkh hio ndio bongo bwana kl idara imeoza na kuna ukiritimba wa mwaka47 bado unaendelea.Wanachojua development wabongo ni ujinga tu km vile mashindano ya umiss ya kl mtaa na sasa itakuja kwa kl familia.Mara mchezo wakiduku,mara cjui nini.Wadau sio kwamba nipo nje ya mada nataka watu wafanye reflection na kuona kwamba kuna mambo ya msingi yanayothiri jamii na maendeleo ya watu ambayo yanayohitajika kushikiwa bango ili yabadilike.Lkn watu tumekua busy na upuuzi..Kumnyima mru document muhimu km hio ni kumfanya asiweze kujiendeleza kielimu km akitaka kufanya hivyo nchi za nje na issue ya kibarua pia itakua tight maana huo uthibitisho cjui utakua na uhalali kiasi gani ukiachilia mbali swala la wapi ataitoa hio elfu10 kl anapofanya application.Huu ni utaratibu mbovu inadidi ubadilike maana akifanya application 10 itakua ametumia hela nyingi kwa ajili ya matokeo kuliko ada ya mwaka mzima kwa shule za serikali,so haya ndio mambo yanayohitaji public support ktk kuyabadilisha co upuuzi amabo hakuna hata nchi1 duniani iliyowahi kuendela kwa mambo hayo.Hayo ni mambo ya ziada baada ya watu kujihakikishia ugali wao..ohooo wabongo lini tutaamka.
ReplyDeleteMimi naona tumezidi kulalamika tu..Hata huku tulipo transcript zinatolewa free mara 3 tu kwa vyuo vyangu vyote nilivyopitia baada ya hapo unalipa. Sijui mambo ya cheti kamili..
ReplyDeleteHiv mnazania admninstative cost ni nani anazilipia. Hilo baraza hela linatoa wapi za kuwalipa hao watu wanao kutolea hivyo vitu. Someone has to pay..
ndio kuna mambo mengine yanaudh i sana Tanzania kama ile nenda huku rudi kule kumbe wanataka rushwa. Lakini na binadamu sisi wa tanzania tunapenda free. Tumia akili... kama wewe unaomba kazi au shule peleka copy uliyonayo baada ya kupata kazi ndio unaomba the real copy kutoka huko. La sivyo utalipa mpaka ukome. na pia tue na mtindo wa kuwa na copy ya vitu vyetu. Watu wengi wakipoteza original copy iwe ya pasi au ya vyeti vya shule ndio basi tena hana hata copy.....Nani alaumiwe...
huku ni kwa copy zako tu. ukituma barua hujaicertified, au hujatumia tracking ikipotea huwezi sema nilituma. Unatakiwa uwe na ushahidi wa kukunack up baada ya hapo kila kitu ni smooth tu...
wewe nawe umekosa shughuli mpaka kuleta case hii hapa kuna kitu chashindikana tanzania?hebu toa rushwa,kama tutakusikia unalalamika,wabunge unaona wanamalizana wenyewe kuingia bungeni kwa kutumia rushwa,kipato 12m,uliona wapi dunia hii,hata ulaya wabunge mishahara yao haiko hivyo na uchumi wetu mbovu
ReplyDeleteNi Baraza la mitihani tu ndo wana sheria hiyo. Mbona hata vyuo vikuu wanatoa vyeti ukipoteza thouhg utachajiwa kiasi. Ninachoona hapo Baraza hawaprint hivyo vyeti( vinnagizwa labda) na kwa vile hawna printing unit na vyeti vinakuja kwa series hawana ujanja wa kutengeneza kingine!!
ReplyDeleteUnless mtu wa baraza kama atasoma hapa atoe a good reason ambayo ni yakisayansi katika karne 21 ni kwa nini wasitoe cheti kingine. sio manager's decision.
Nenda Kagonge mlango kwa secretary wa huyo mkuu umueleze tatizo lako, atakupa kikaratasi ukamuone nani, kwa ujumla ukate mguu wako kila siku, kama hutaki kutowa chochote, kwani hata tanesco ukiwapigia mguu kila siku utapata umeme as long soli yako itakwisha njiani. Tufahamshe ukifanikiwa umetumia njia gani kufanikiwa.
ReplyDeleteKama hili jambo ni la kweli, basi tuko nyuma sana. Sikatai kulipia cheti kama umepoteza kwasababu ni lazima kulipia gharama za uchapishaji ila nafikiri umefika wakati vyombo muhimu kama baraza la mitihani kuboresha utendaji kazi wao. Tatizo ni nini? Hakuna printer, fedha za kununulia printer au ni sera za kukomoana. Hizo barua za majibu zinachapishwa vipi? Suala la kukubalika sio la msingi. Kitu cha msingi ni kuwa professional. Katika dunia hii ya leo ambayo kupata kazi na hata nafasi za kusoma elimu ya juu ni vigumu, ingesaidia sana kupunguza vikwazo vya kijinga kama hivi. Tusiendeleze hali hii maana tukitoka nje ya nchi wenzetu wanatuacha. Tatizo letu tunaendeleza vitu kama hivi na vinaturudisha nyuma. Asanteni.
ReplyDeleteHiyo ndiyo sheria yao, and mind you, hata hiyo results slip ina expiry date yake, iangalie vizuri. Vyeti vya mwaka uliomaliza shule vikishakuwa tayari na vikatumwa mashuleni, automatically results slip inaexpire
ReplyDeletePole kwa yaliyokukuta, kwa ni kupoteza docs. ni kawaida waweza pia kuibiwa.
ReplyDeleteKulipa tshs 10,000 kwa kila appl. is too expensive. Kweli kutoa vyeti mara 2 tulivyozea haipo(yaweza kuwa ni sheria au policy).
Ila baraza la mitihani linapaswa kuangalia hili kwa makini. Wawe wanatoa certified true copy kusaidia waliopoteza vyeti. Ukiachilia mbali gharama za barua pia muda wa kwenda kila unapofanya appl. na kusubiri, kwa nchi yetu unaweza kuambiwa njoo kesho anahusika hayupo. Its better utoe hata zaidi ya hiyo ela lakini ushughulie hili jambo mara moja tu.
basi hii sheria ni mpya, mimi nilipoteza vyote vya O na A level. Ila ikafika kipindi 2004 nikawa navihitaji, nikaenda shule niliyomaliza na kuwauliza wakaniambie niende baraza nikafata process ya baraza na kupata vyote viwili ambavyo ni duplicate.
ReplyDelete