MAREHEMU REDEMPTUS ANGELO
Uongozi wa Kampuni ya MEDIA SOLUTIONS LTD wachapishaji wa magazeti ya ThisDay na KuliKoni unasikitika kuwatangazia kifo cha ghafla cha mfanyakazi wake, Redemptus Angelo kulichotokea Jumapili Agosti 01, 2010 Saa 4.00 usiku katika Hospitali ya Mwananyamala.
Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwake Tegeta,
Dar es Salaam na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.


oooh my god redemptus a.k.a TEMBE siamini kabisa poleni sana mke na mtoto wake. ni huzuni kweli
ReplyDeleteJamani Reddy. Umekuwa rafiki na msaidizi wangu wa karibu sana tangu THISDAY, KULIKONI na hatimaye kwenye gazeti letu wenyewe la MAWIO. Sasa tena nasikia tena umetangulia mbele za haki, ambako hata hivyo sina uhakika mlango gani umepitia na wala sina uhakika ni mlango gani utatokea pamoja na kuwa na imani kuwa umeenda vyama. Hiyo anajua Mungu Mkuu. Hata hivyo tangulia nasi wafuata. Najua ulitengeneza gazeti la THISDAY liliko mitaani leo na hata MAWIO ambalo limekuwa likienda hewani kivingine bado uliendelea kuwa nalo na kuwekeza imani kubwa kuwa huenda siku moja litakuwa gazeti kubwa pamoja na kuanguka na kunyanyuka. Ulale pema ndugu na rafiki yangu Reddy. Hakika umekuwa pigo kubwa na utendaji wako tutaukosa kwani hukujali kula wala kunywa wakati ukifanya kazi yako na zaidisana ulipenda kazi iliyotukuka. Tangulia mwenzetu
ReplyDeleteMbona twasikia na na yule mwandishi mahiri bwana Johnson Mbwambo wa Gazeti la Raia Mwema amelazwa Agha Khan hoi taabani?? Hebu Michuzi tueleze ukweli wa jambo hili.
ReplyDeleteRede tutakukumbuka daima..Nakukumbuka kipindi kile tupo wote "Thecitizen" saa nne usiku tunaghaika na kukamilisha gazeti..Ulale salama Rede...
ReplyDeleteWee anony wa 08/02 huo unaitwa uchawi. Yakutakia nini kama mtu anaumwa awekwe kwenye media. Wee ukilazwa unataka kila mtu ajue, SO WHAT??? Wee ndio doctor wa Johnson. Hebu kaa kando hangaika na shughuli zako. Kama anakuhusu sana ungeishajua habari zake!!! Mtafute kwa muda wako. WATU!!!!!
ReplyDeleterest in peace our brother rede, we (Richard, Malelo, benson, Queen)will always miss you. ni ngumu kuamini lakini tutafanyaje yote tunamwachia mungu.
ReplyDeleteRIP Rede, ni ngumu kuamini! Nitakukumbuka daima kamanda kwa uchapa kazi wako, tulipambana pamoja kuanzisha The Citezen, tulikuwa pamoja pia tulipounda Timu ya Media Solutions, na kuanzisha THIS DAY na KULIKONI. those days za kukaa ofisini mpaka usiku wa manane.
ReplyDeletemoleli sana! Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu! Bwana ametwaa jina lake libarikiwe!
ReplyDeleteSHEMEJI UMETUTOKA WAKATI TUKIWA TUNAKUHITAJI, NAKUMBUKA UCHESHI WAKO WAKATI WA MAANDALIZI YOTE YA HARUSI YA MDOGO WAKO RICH ALIYEMUOA MDOGO WANGU TINA, FAMILIA YA AKINA TINA TUNAMUOMBA MUNGU AKUPOKEE, REST IN PEACE MAN!
ReplyDelete