Andrea akiwa kitandani pake

Mtoto Andrea Kipangula ni mtoto yatima kati ya watoto wanaosaidiwa vifaa vya shule na TAWLAE kwa msaada wa USAID/AED/ AGSP.

Ana miaka 10 (kumi) na anasoma darasa la nne (4) katika shule ya Kibao, wilaya ya Mufindi, kwa sasa, kwa masaa anayoweza kumudu anasoma shule ya msingi ya Makuburi, wilaya ya Kinondoni.

Mtoto huyu ana tatizo la kutopata choo kwa muda mrefu kwa vile njia yake ya haja kubwa inahitilafu. Madaktari wamemfanyia upasuaji mara saba hosipitali ya rufaa ya Muhimbili ili kurekebisha hali yake.
Kwa sasa imebidi atumie utumbo mkubwa kutolea choo ambao upo nje ya tumbo lake, hali ni ngumu kwa mtoto huyu.

Bibi yake ambaye ni mzee sana pamoja na shangazi yake ambaye ni mjane, hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu na maisha.
Wale watakaopenda kusaidia kwa njia ya benki,

tafadhali weka katika akaunti namba
012103000838
ya NBC Samora Branch Dar-es-salaam,
ukishaweka tuarifu kupitia simu namba
0754-360215, 0754-360215, 0754-360215
au +255(22)2700085, +255(22)2700085, +255(22)2700085,
au fax pay in slip ya benki kwenye namba +255(22)2700090 +255(22)2700090 +255(22)2700090
Vinginevyo tuletee msaada kwenye ofisi zetu zilizopo
MARI-MIKOCHENI
Plot namba 24 “b”
Sam Nujoma Road
kuelekea kiwanda cha Cocacola,

Tafadhali tunaomba msaada wako ili kumsaidia mtoto Andrea.
Aksante.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Mwezi wa machumo ndio huu kwa waasilamu, tenda hii kwa wenye uwezo, kama unahitaji pepo tiketi ndio hii

    ReplyDelete
  2. Hiyo hali ya mtoto Andrea, pamoja na kwamba itashtua wengi, si ya ajabu hata kidogo.

    Ushari wangu tu, Michuzi kama unaweza kuwafikishia ujumbe, TAFADHALI WAMPELEKE KCMC KULE MOSHI. MUHIMBILI SIKU HIZI NI BALAA TUPU PALE, HAKUNA KINACHOENDELEA.

    TAFADHALI, NENDENI KCMC..labda hata Bugando au Mbeya wanahuduma nzuri, ila mimi uzoefu wangu ni kuhusiana na KCMC na ndio ushauri ninaoweza kutoa.

    Mungu akujalie upate huduma Andrea, na upone

    ReplyDelete
  3. Huyu mtoto anasikitisha saaana. Aliyeshauri apelekwe kcmc au bugando ni sawa kabisa. Angeanzia huko tayari angeishapata nafuu sana. Muhimbili wamekalia kupewa kitu kidogo ndio kazi inaenda. Pale hakuna madaktari wote wanafunzi.

    La pili ni kwamba hela zilichangwa zikawekwa kwenye account zitaliwa tu hazitafanya kazi yoyote. Kama walivyosema kuwa walezi hawana uwezo, vile vile aliyetaja hiyo account nafikiri sio mlezi wa karibu wa mtoto. hana uchungu lazima hela zitaliwa tu.

    Cha msingi wamuhamishe mtoto wampeleke bugando ndio wenye mapenzi mema waanzw kuchakalika. au, waonyeshe nia ya kumuhamisha, ili pesa alipwe msafirishaji kama ni ndege tujue ni shirika gani lilipwe. Vinginevyo huo ni mtaji wa wenye meno . Siku hizi ubinadamu haupo.

    ReplyDelete
  4. wewe unaesema nikitu cha kawaida naomba ufute huo usemi,kumbuka HUJAFA HUJAUMBIKA.usimkufuru mwenyezi Mungu.pole sana andrea mwenyezi mungu atakusaidia utapona na utaendelea vizuri na masomo yako.poleni wazazi.

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi, mimi niko nje ya nchi, naomba contacts zote za hiyo benki ya Andrrea. Kwa mfano, address, routing no. etc.

    Asante sana kakangu.

    ReplyDelete
  6. kweli hujafa ujaumbika,inatia uchungu mno.Kwa ushauri wangu hili tangazo halitashawishi watu wengi,sababu kinachotakiwa uchunguzi ufanyike kujua ni hospitali gani wataweza kutatua tatizo na kwa gharama gani ili tangazo linavyotoka litaje moja kwa moja kiasi kinachohitajika.hivihivi mtu hawezi kujua atoe shilingi ngapi ili mtoto aweze kupata matibabu.

    ReplyDelete
  7. Kwa keli hali ya huyu kijana mdogo inasikitisha sana. Na tujitokeze kumsaidia, Ila jambo jingine serikali yetu haiwezi toa msaaada kama huu? viongozi wetu wengi mamilionear wanashindwa guswa na suala kama hili? realy not fear......
    Nchi za wenzetu serikali zao zinajitahidi sana kutoa misaada kama hii tafadhalini tuige mifano....naomba ujumbe huu uwafikie viongozi wetu. Kijana huyu anaweza kuwa mtu muhimu kwa taifa letu na kwa jamii nzima.... toeni taarifa nyingi magazetini ili mtoto apate msaada. kama nilivyosoma comment ya hapo juu hospital zetu zinaonekana kushindwa kumtibu, basi apelekwe hospital zinazomfaa. kama wanavyofanyiwa viongozi wakubwa na family za.
    deak
    Oslo norway

    ReplyDelete
  8. HAKIKA KIJAMNA ANAMTIHANI MZITO. NAFIKIRI WALE TULIOGUSWA NA HALI YA MTOTO HUYU TUNAYO NAFASI YA KUJITOLEA JAPO KIDOGO KUMSAIDIA MTOTO HUYU. UKIMTAZAMA VIZURI UNAONA NURU YA KIJANA HUYU IKIHITAJI MSAADA WETU. JAMANI NDUGU ZANGU TUNAYO NAFASI YA KUTIMIZA NDOTO YA KIJANA HUYU KUEPUKA HUU MTIHANI. HUYU NI MWALIMU WETU, MHANDISI WETU, RAIS WETU HEBU TUJITAHIDI HATA KWA USHAURI KWA WALE WENYE UTAALAMU. HEBU SHIME TUPENI MCHANGO WENU AENDE WAPI KUPATA TIBA YA UHAKIKA. KCMC, BUGANDO,WAPI JAMANI?...KUTOA NO MOYO. KIJANA POLE SANA MUNGU AKUPE NURU NA KUWA NA AFYA NJEMA.

    DEE WA DAA.

    ReplyDelete
  9. jamani hivi wizara ya afya haioni kwamba case kama hizi wangetakiwa wasaidie angalau mtu apate matibabu, nasema hivyo kwa kuwa liko ndani ya uwezo wao, ingekeua labda anatakiwa kwenda kutibiwa india hela nyingi tungesema sawa, lakini hapo hapo kwetu, muhimbili, hii ni aibu kubwa sana, tena sana!! waizara imsaidie mtoto huyu jamani.

    ReplyDelete
  10. mtoto yuko kwenye hali kama hii na nchi imeshikwa na mafisadi.inamana hawa mafisadi hawana huruma hata kidogo hata kwa kutumia hela za wizi kumsaidia huyu mtoto apate matibabu?

    kweli naamini kwamba sisi binadamu ndio mashetani wenyewe.


    mungu atamsaidia huyu mtoto.

    ReplyDelete
  11. Kaka Michuzi nahitaji kujua jambo moja.Je fedha zinazotakiwa kwa ajili ya matibabu ni ili atibiwe hapo hapo Muhimbili au? maana umeandika kuwa alishafanyiwa matibabu(surgery) hapo mara saba!
    Lingine.Je plan ya kumsaidia mtoto huyu ikoje zikipatikana pesa? maana serious mtoto ana wakati mgumu.
    Halafu, wakati tunajiandaa kumsaidia mtoto huyu, naomba niseme kuwa serikali inapaswa sana kuchukua jukumu la kumsaidia mtoto huyu.Ni aibu kwa mtoto kuteseka hivi wakati serikali ipo.Fedha zipo za kumpeleke nje kwa matibabu! Please Michuzi lipigie sana suala hili kelele mpaka kieleweke.
    Moses Gasana
    London

    ReplyDelete
  12. Point tumeipata, Andrea anahitaji msaada...na anatatizo hilo. Lakini bwana Michuzi...Dang! Japo kumsitiri kwa kumfunika kabla ya kumpiga picha. Naelewa lengo ni watu waone hali halisi....lakini inabidi kumsitiri...it's too graphic, 5 years later kama akiwa amepona God willing akiona hii picha yake in the web atajisikia vibaya.

    ReplyDelete
  13. MICHUZI TAFADHALI FUATILIA JINA LA AKAUNTI..MBONA TUMEPEWA AKAUNTI NAMBA TU. NA JE PLAN B, WANAYOFIKIRIA KUIFANYA NI IPI, BAADA YA KUPATA MSAADA. MAANA NI MSAADA WA HELA UNAOMBWA LAKINI HAILEZI PLAN B YA MATIBABU NI IPI ILI MTU AWEZE KUFIKIRIA KIWANGO ATAKACHOCHANGIA. JE WANA MPANGO WA KUMSAFIRISHA KWENDA NJE KWA MATIBABU AMA NI HAPA HAPA TANZANIA, NA GHARAMA JUMLA WANAZOTEGEMEA KATIKA MATIBABU NI KIASI GANI. NAONA TUKIPATA PICHA KAMILI, MTU ATA EVALUATE ATOE KIASI GANi?

    ReplyDelete
  14. Jamani hali ya mtoto huyu si nzuri, anahitaji msaada wa haraka iwezekanavyo, kinachonishangaza suala kama hili Serikali inajifanya haioni? we really dont have a serious government, watu wataanza kuchangishana hadi lini wakati mtoto anaendelea kuteseka. Serikali imalize hili tatizo ASAP. Wao wakiugua mafua tu wanaenda nje ya nchi. Waziri wa Afya be serious please.

    ReplyDelete
  15. pole mtoto na utatibiwa utapona
    ila hii ya akaunti kwakweli siku izi hakuna kuaminiana hata kidogo na uyu mwenye akaunti ni nani?
    hasa wanachotakiwa kufanya ni km apo juu walivosema WASILIANENI na hosp ya BUGANDO na KCMC then mjue gharama zake,usafiri,adi malazi then m-post hapa ndio watu waanze toa msaada,,,laa sivo watu hawana ubinadamu likija suala la pesa!

    ReplyDelete
  16. Kama harusi tunachangishana kwa nini tushindwe kunusuru hali ya mtoto huyu. Watanzania wote tuliochangia hapa ni wanafiki. pamoja na mimi. Harusi tupo mstari wa mbele. Mtoto tunasema serikali. Ujinga mtupu.

    ReplyDelete
  17. Kweli hujafa hujaumbika. Naomba lawama zangu nizielekeze kwa Serikali yetu hii awamu ya nne (ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya) hiyo ari iko wapi???? Tuna Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kweli ustawi wa jamii uko wapi, afya iko wapi??? kweli huyu mtoto angetakiwa michango ya watu tena au Wizara ichukue nafasi yake.

    Pili tuna Wizara ya Maendelea ya Jansia, Wanawake na Watoto. Katika hii Wizara watoto wako wapi?? si mtoto huyo na Wizara ina fungu kwa ajili ya watoto kama hawa wenye matatizo au fungu ni kwa ajili ya watoto wa wakubwa?????

    Na bado Wizara hii ina uwezo wa kuomba hata kwa donors kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyu, kuna mashirika ya UN yanayoshughulikia watoto, Wizara imeshindwa kushughulikia hapa???

    Sasa hapo huyo yuko hospitali na ndugu Michuzi ameweza kumfikia Serikali iko kimya kiasi hiki je wale ambao hata uwezo wa kufika hospital hawana inakuwaje.

    Mheshimiwa Kikwete iko wapi sera yetu ya ari, nguvu na kasi mpya???

    ReplyDelete
  18. Kaka Michuzi minapendekezo moja tu kwa watu tunaohitaji misaada, tujitahidi kupata njia rahisi ya kuchangia hapa nimaanisha kwa kutumia simu za mkononi ambapo mtu anaweza kucahngia kuanzia 1000 na kuendelea hapo tungeweza kupata nyingi na kwa muda mrefu .maana kila mtu akisoma hii post anaguswa lakini kwenda benki labda hiyo pesa hana ama anona shida/aibu kutoa 5000 au 10,000 na ndio uwezo wake. Changamoto kwa wadau wanojua utaratibu wa kulipia kwa SMS watujulishe ili tuweze kutumia kwa kila msaada unaoweka kwenye blog yetu.
    PAMOJA TUNAWEZA!!!!!!!

    ReplyDelete
  19. Hahahaah!! sicheki Nafurah Nacheka naumia nashangaa!!!!! ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA EENH!!! MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!! MIFOLENI INAZIDI KUONGEZEKA!! BIDHAA MASOKONI HAZIKAMATIKI!!!! HAYA HYU MTOTO JAMANII NDIO HIVYO INABIDI SISI WEMYEWE WANA JAMII TUJIPIGE KILE KIDOGO TUKIPATACHO MAANA MISHAHARA YENYEWE NDIO HIYOO! Uwiii Tutasaidiwa nani sisi watanzania!! Viongozi hawana habari na sisi Sijui wanaongoza nini Semina na Vikao vinaongezeka tuu!!!!!!!! Mungu msaidie mtoto huyu apate matibabu apone. Mungu tubariki watanzania hatuna wa kumlilia

    ReplyDelete
  20. anonymous 19/08 10:11 nakuunga mkono.Tunaleta unafiki.
    Tutafute njinsi ya kumsaidia huyu mtoto apone.mambo ya serikali tuachane nayo.nikupoteza muda.Kaka michuzi fatilia habari kamili za mtoto huyu yaani Jina la mwenye Ac,ni nani yake.mipango ya kumtibu ikoje ili kama baadhi ya wachangiaji walivyosema tujue gharama kamili.gharama hizo ni kama ifuatavyo:
    1.usafiri dar- moshi-dar
    2.gharama za matibabu
    3.gharama za kujikimu.
    naamini tutaweza kumpatia matibabu mtoto huyu.

    ReplyDelete
  21. Ningependa kutoa msaada ila hiyo account wekeni SWIFT, IBAN ili kwa walio nje tuweze ku2ma.
    Secondly huo msaada ni wakumsafirisha sehemu nyingine ama kummaliza Muhimbili?

    Lord have Mercy

    ReplyDelete
  22. Naomba kutoa wazo. Kwa kuwa hii taarifa tumeipata kupitia blogu ya jamii, naona itakuwa ni vyema kama pesa tutakazochanga wengi wetu ambao tumeguswa na hali ya mtoto huyo zikapitia kwa Michuzi,kwani nina uhakika yeye ni mzalendo atafikisha michango hiyo mahala inapostahili au hata kufanikisha mipango ya kumpeleka mtoto huyo huko hospitali KCMC ambako wengi wetu tunaona atapata msaada anaostahili. Mungu awabariki wote wenye nia nzuri ya kumsaidia huyu mtoto kwani kutoa ni moyo.

    ReplyDelete
  23. Michuzi kwanini hao USAID, AED NA AGSP wanaomsaidia vifaa vya elimu pia wasijulishwe kuwa mtoto wanayemsaidia vifaa hawezi kusoma vizuri bila ya kuwa na afya nzuri. Ikiwezekana wamsaidie pia matibabu isikute hawajue kama ni mgonjwa. Tunapenda kuchangia lakini tunauhakika gani na hiyo akaunti namba kama sio ya matapeli

    ReplyDelete
  24. Kaka michuzi, tusaidie kujua maendeleo ya mtoto Andrea, mimi nimeshiriki katika kutuma pesa kwa ac tajwa.Ningependa kujua mpaka sasa hatua gani zimechuliwa kumpatia matibabu sahihi.
    najua uko busy ila natumaini itakuwa vema ukitupa "feedback" au kwa kiswahili mrudisho nyuma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...