Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za Italia, Jumamosi ya 31/07/2010, walijumuika katika hospital ya Mtakatifu Camillo (San Camilo), mjini Rome, kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Hamisi Abdalla George, aliyefariki 18/0 7/2010 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mapema wiki hii mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa mazishi. Habari Kamili juu ya siku na saa kamili mwili wa marehemu kuwasili nchini Tanzania mtajulishwa mapema iwezekanavyo.

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome unatoa shukurani za dhati kwa maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Jumuiya za Watanzania Napoli, Genova, Modena na jumuiya ya Mt. Egidio kwa kujitolea kwa ukarimu kwa hali na mali katika msiba huu. Mwenyezi Mungu awajaze maradufu mlichokitoa. Kwa habari zaidi na picha tembelea
www.watanzania-roma.blogspot.com.
Watanzania Rome wakimuombea marehemu wakati wa kumuaga


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Rest in Peace Hamisi. Pole kwa ndugu jamaa na marafiki popote pale mlipo. Ongeleni pia Jumuiya ya Watanzania Rome kwa mfano mzuri wa kiubinaadamu.

    ReplyDelete
  2. Naona kuna makosa katika kuandika majina. Akina George ni wakristo.

    ReplyDelete
  3. Hakuna Kosa lolote ilo ndio jina lililopo kwenye passport ya marehemu.Sababu ya kuliweka hilo jina kwenye passport mimi na wewe hatujui.Asante.Kazi njema!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...