National Arts Council BASATA
MKAKATI WA KUIMARISHA UONGOZI KATIKA SEKTA YA SANAA
MKAKATI WA KUIMARISHA UONGOZI KATIKA SEKTA YA SANAA
Baraza la Sanaa la Taifa liko katika mpango wa kuimarisha Uongozi katika Sekta ya Sanaa kwa kuunda MASHIRIKISHO YA SANAA YA TAIFA nchini.
Mashirikisho hayo ambayo yataunganisha vyama vya kitaifa na mikoa yamegawanywa katika maeneo yafuatayo :-
1. Sanaa za Maonyesho
2. Sanaa za Ufundi
3. Sanaa za Muziki
4. Sanaa za Picha Jongevu (filamu)
Mashirikisho hayo ambayo yataunganisha vyama vya kitaifa na mikoa yamegawanywa katika maeneo yafuatayo :-
1. Sanaa za Maonyesho
2. Sanaa za Ufundi
3. Sanaa za Muziki
4. Sanaa za Picha Jongevu (filamu)
Mchakato huo ambao uliwashirikisha Wataalamu wa Sanaa, Wadau, Viongozi wa Vyama vya Sanaa na Wasanii ulianza mapema mwaka 2009 baada ya kubaini uwepo wa vyama vya sanaa ambavyo utendaji wake hauridhishi.
Hatua zilizopitiwa katika uundwaji wa Mashirikisho hayo ambayo yatakuwa kiungo kikuu katika kuviunda na kuvisimamia vyama vya sanaa ni kama ifuatavyo.
• Ulifanywa utambuzi wa vyama vya sanaa vilivyopo
• Viongozi wa vyama walikutanishwa kupata mustakhabali wa vyama vilivyopo
• Wataalamu wa Sanaa walikutana na kutoa ushauri wa mwelekeo wa Mashirikisho
• Wadau walishirikishwa na kuunda kamati kazi zilizoandaa rasimu za katiba za Mashirikisho hayo
• Wadau na Viongozi wa vyama walipitia rasimu za katiba za Mashirikisho.
Hatua tuliyonayo hivi sasa ni uchaguzi wa viongozi na kuunda Mashirikisho hayo kwa kalenda ifuatayo :-
10/08/2010 Shirikisho la Sanaa za Ufundi – SHISUTA
11/08/2010 Shirikisho la Sanaa za Muziki - SMT
12/08/2010 Shirikisho la Sanaa za Maonyesho – SHISAMA
13/08/2010 Shirikisho la Sanaa za Picha Jongefu – TAFF
Hizi ni chaguzi za Viongozi wa muda
wa Mashirikisho hayo ambayo watawajibika.
• Kuandaa mazingira ya Uchaguzi Mkuu wa kila Shirikisho
• Kuandaa Kanuni mbalimbali za Mashirikisho
• Kujitangaza na kupata vyama wanachama vyenye nguvu ya kuhudumia Wasanii nchini
Baraza la Sanaa la Taifa linatoa wito kwa Vyama vyote vya Sanaa vilivyosajiliwa na Baraza kwa mujibu wa Sheria Na. 23 ya mwaka 1984 kujitokeza na kuleta wanachama wapiga kura ili kufanikisha uchaguzi huo.
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI
Barua zote ziandikwe kwa Katibu Mtendaji
All correspondence to be addressed to The Executive Secretary
BASATA Arts Centre,

Ilala Sharif Shamba,
P.O. Box. 4779,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Telephone: 2863748/2860485,
Telephone: 2863748/2860485,
Fax: 0255 - (022) - 286 0486
E-mail: info@basata.or.tz
Website: www.basata.or.tz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...