
Mgombea urais kwa Chama cha NCCR Mageuzi, Mh. Hashim Rungwe akionyesha ilani ya uchaguzi ya chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho leo jijini Dar.
Chama cha NCCR-Mageuzi kimezindua ilani yake ya Uchaguzi huku kikitaja mambo 12 ambayo chama hicho kitaelekeza nguvu iwapo kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi.
Wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa chama hicho taifa James Mbatia alisema chama chake kitazindua kampeni zake kitaifa Septemba 11 baada ya mfungo wa Ramadhani ili kutowakwaza Waislam ambao wako kwenye mfungo wa mwezi mtukufu.
“Ajenda yetu kuu itakuwa ni katiba, tumeanisha mambo yatakayokuwemo kwenye katiba hiyo, hili ndilo nataka wagombea wetu mlizungumzie kwa kina,” alisema Mbatia.
Lakini pia Mbatia aliwataka wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho kuendelea na kampenzi zao katika maeneo yao, lakini waepuke kuwasema watu au kutumia lugha za matusi badala yake amewataka wazungumzie hoja na matatizo yanayowakabili wananchi.
Kutokana na baadhi ya mambo hayo, Mbatia aliwataka Watanzania wakichague chama hicho kwani kitendo cha Oktoba 31 kinaweza kuwafanya wajutie kama watarudia makosa ambayo wamekuwa wanayafanya katika chaguzi zilizopita.
Lakini pia aliwataka wagombea hao kuacha tabia ya kutumia majukwaa kuzungumza watu na kueleza kuwa kufanya hivyo ni umbeya. “Epukeni kujadili watu, msitumie matusi kwani mtakwaza watoto iwapo mtatumia matusi.”
Alisema wagombea wakichambua hoja Watanzania wanajua mchele na pumba, na kwamba kuna matatizo mengi yanayowakabili Watanzania ikiwemo ukosefu wa maji, lishe “lakini kikubwa mwaka huu hoja yetu kubwa itakuwa ni katiba.”
Is this guy serious?
ReplyDeleteHe is serious if you are....
ReplyDeletewatu wengine bwana. maudhi tu
ReplyDeleteKimeo hichoo...sura yenyewe hana wala mvuto...
ReplyDeleteNi nini haswa kilichokuudhi? Badala ya kuchukia umaskini wakujitakia, ambao umetawala nchi yako. Unaudhika unapoona watu wanataka kubadilisha mambo. Kaazi kweli kweli...
ReplyDeleteJamani mwenye ilani ya uchaguzi ya NCCR Mageuzi, CCM, CUF na CHADEMA anitumie kwa kawogo@yahoo.com
ReplyDelete