
Jarida hilo lililoandaliwa na timu ya wanahabari wachambuzi linapatikana nchi nzima likiwa na dodoso kuhusu mustakabali wa Taifa kama zile zinazohusu siasa za Zanzibar hususani kilichopo nyuma ya pazia katika uteuzi wa Dk. Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais wa CCM Visiwani.
Kama hiyo haitoshi UMOJA limefanya mahojiano mazito ya ana kwa ana na watu mashuhuri nchini, kama vile Zitto Kabwe, January Makamba, Tausi Likokola, na Lillian Mduda.
Jarida hilo pia lina wasifu wa mwanadiplomasia aliyetukuka nchini, Dk. Asha-Rose Migiro likiwa pia na makala nyingine nzito za kitaifa na kimataifa ikiwamo moja ya michezo inayogusa safari ya ukocha nchini ya Kocha Mbrazili Marcio Maximo aliyemaliza mkataba wake hivi karibuni.
Waandishi wenye majina nchini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Absalom Kibanda, Ratifa Baranyikwa, Charles Mullinda, Alloyce Komba na wengine wengi wamejumuika ili kuwaandalia wakazi wa nchi za Afrika Mashariki wanaozungumza Kiswahili bidhaa ambayo haijapata kuwapo kabla hapa nchini.
na siye kwa kuiga..hawakuweza kuja na lao creative thinking tz iko wapi
ReplyDelete