Zanzibar For Democracy inachukua nafasi hii kuwapongeza wazanzibari kwa uamuzi wa kihistoria waliouchukua kwa kupiga kura ya NDIYO katika zoezi la kura ya maoni.
Sisi tunaamini kuwa uamuzi huo utafungua ukarasa mpya wa maendeleo na kuipeleka Zanzibar katika Demokrasia ya kweli ambapo wananchi wenyewe watakuwa ndio watakaokuwa na mamlaka, madaraka na uamuzi wa mwisho kuhusu mambo yote ya nchi yao.

Ushindi huo wa kura ya NDIYO unaweka bayana kuwa wananchi wamekubali kujenga jamii mpya yenye kuthamini utu wa mtu na ubinadamu na kuhakikisha kuwa Zanzibar itaongozwa kwa sera zenye kufuata misingi ya uhuru,haki, udugu na amani yenye kudumisha SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ambayo itakuwa ni kichocheo katika nyanja zote za maendeleo na utamaduni wa Visiwa Vyetu na watu wake.
Ahsante,
UONGOZI,
ZANZIBAR For Democracy,
LONDON,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Alfu Mabruk ya daulatil Zinjibar.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. Sasa wewe US blogger wa kwanza, hicho kiarabu umejiandikia mwenyewe ndo uelewe au?

    ReplyDelete
  3. tunaelewa sisi wazenj hiyo.US blogger umeeleweka

    ReplyDelete
  4. Zawadi NgodaAugust 02, 2010

    Chukua au acha, lakini kazi kubwa iliyosubiriwa kwa zaidi ya miaka 30 imefanyika. Hii ndio demokrasia ya kweli toka kisiwa cha Zanzibar kizaliwe.

    Pongezi za kwanza kabisa napenda kumpelekea Rais wa jambhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar, Abei Karuma, Katibu wa CUF, Sheikh Maalim Seif, Wanachama na viongozi wa CCM na CUF, NA Wananchi wote wa Zanzibar.

    Huu si ushindi kwa Zanzibar tui bali kwa Tanzania nzima.

    Tanzania imezaliwa upya, Tanzania OYEEEEE!!!

    ReplyDelete
  5. ASIEJUA MAANA HAAMBIWI MAANA UKIMWAMBIA MAANA ATASEMA UMEMTUKANA,,,MWACHENI HUYO ALJUNUN FUNUN....

    ReplyDelete
  6. wazanzibari kwa maneno? ngoja sasa tuone kama mnajua vitendo na kujifanya mnasifia 'KURA ZA NDIO"

    Eti na ushindi kwa Tanzania nzima, nani kasema........ kama ni tanzania nzima mbona huku bara hatukupiga kura? hayo ni yenu tu na mambo yenu yasiyo isha ... haya tuone sasa kama mtaelewana. Yetu macho na masikio!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...