Tangazo la Mradi wa Maji wa Luis Mbuya Masaera Kilema Kusini,Moshi Vijijini.


Raia wa Kilema Kusini, Bw Louis Mbuya, [aliyekuwa Diwani wa CCM, lakini aliyekosa kura za maoni za CCM] ametangaza rasmi kwa bango hili linaloonekana katika ofisi zake binafsi, zilizopo katika kijiji cha Kilema -Chini, katika barabara ya Kilema, kuwa anamiliki mradi wa maji
na anatangazia umma kuwa mradi huu alifadhiliwa na ROTARY INTERNATIONAL na
SERIKALI YA UJERUMANI .

Amefungua ofisi ya maji katika eneo lake la biashara, Masaera Grocery na Soko la Pamoja! Raia wasioelewa wanakwenda kwake kulipia ada ya kuunganishwa maji kwa shs 130,000/, naye anachukua pesa hizo na kuziweka mfukoni.

Wengine waliuziwa mita za maji bila kuunganishiwa na kulipa shs 130,000/- wana mita hizo majumbani mwao. Maofisa watendaji wa kijiji na kata wanajua jambo hili lakini wameshindwa kulidhibiti!

Mkurugenzi Mtendaji wa Moshi Vijijini Mhandisi Mwahalende na Mkuu wa Wilaya wa Moshi, [ DC] Bw Samizi wanaelewa jambo hili! Mradi wa Maji ya Chele una hati miliki ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Parokia ya Mandaka.

Jumuiya Halali ya Watumia Maji wa Kilema Kusini iliyoundwa kisheria [na kusimamiwa na Mhandisi wa Maji Bw Macha na Mtendaji wa Kata wakati huo, Bw S Mrema] inahujumiwa na huyo BW LUIS MBUYA NA AMEWAFUNGULIA KESI ZA MADAI WANAJUMUIA KUWATISHA KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA YA MOSHI.

Viongozi wote wa Wilaya na Mkoa wamekaa kimya. Wajenzi wa Mradi huu TPP Trust chini ya uongozi wa Mheshimiwa Peter Kisumo na ambao haujakabidhiwa rasmi wanajua jambo hili! Taarifa hizi zipo kwa viongozi wahusika Mkoani na Wilayani na kwa Kituo cha Polisi Himo tangu tarehe 14/08/2009.

Mimi binafsi Nimewasilisha Taarifa hizi kwa TAKUKURU Moshi. Bwana Luis Mbuya ameshtakiwa kwa wizi akiwa Diwani kituoni HIMOref HI/RB/2644/09 tangu 2009 lakini jambo hili linasuasua .

Sasa Bw LuisMbuya amechochea Ofisi ya kijiji cha Masaera imilikiwe na Mama Lucia Aloyce Lyimo kwa kisingizio cha uongo kuwa ilijengwa mahali pasipo halali wakati nyaraka zote zinaonyesha kuwa serikali ya Kijiji ilipata eneo hilo kihalali!

KUNA NINI ?

Wasalaam,
Canute W Temu
Raia wa Kilema Kusini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. nilipoanza kusoma tu heading nilijua ni kanuti temu kaandika, kazi ipo...............

    ReplyDelete
  2. Kanuti Temu unachafua chama chetu cha CHADEMA hatukutaki masaera tunataka Chama kimteue mtu mwingine propaganda zako za kujipatia umaarufu zimegonga mwamba... huna lolote wamasaera wanapenda amani tunajua unataka kushika madaraka ili nawe ulete ufisadi wako tunaoujua tangu miaka ya nyuma usitake tukuumbue kwenye vyombo vya habari... Mradi wa Maji ni initiatives za Louis Mbuya hilo linajulikana wewe umefanya nini domo kaya????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...