Kamati kuu ya CCM imemuengua Bw. Husein Bashe ambaye aligombea kura za maoni ccm kupitia jimbo la Nzega, Tabora, na kumbwaga aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Bwana Lucas Selelii kwa jumla ya kura 14,200 za Bashe, dhidi ya 2700 za Selelii, kutokana na utata wa uraia wake ambapo inadaiwa si raia Tanzania

Hello,
Nimerekodi mahojiano ya BBC Swahili kipindi cha Dira ya BBC wakati bi Aisha Yahya anahojiana na Hussein Bashe kuhusu suala la uraia kisha mazungumzo ya Salim Kikeke na John Chiligati kuhusu suala hilo.
Linki ni hii:
http://bit.ly/abkuk6
Shukrani kwa timu nzima ya
BBC kwa mahojiano haya.
Subi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Ankal,

    Tafadhali tuwekee utangulizi wa habari japo kidogo.

    Hussein Bashe ni nani?

    ReplyDelete
  2. Mie nafikiri kuna mtu ndani ya ccm alitakiwa awajibike kwenye ili swala la Hussein,.ina maana Hussein asingeingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge hakuna ambaye angegundua kwamba si raia,au ndo tusema siasa kuna mchezo mchafu? huyu muungwa alikuwa na nyadhifa kwenye uvcc tabora,inanikumbusha mambo ya jeneral ulimwengu,.duh nchi hii bwana. Mbona Mustafa Mkulo ana kashfa ya uraia? alikuja na wazazi wake kama manamba toka Malawi, kheri ya Bashe aliyezaliwa hapa,. au ndio mambo ya mwenzetu tumlinde?

    ReplyDelete
  3. Rostam Aziz naye ni raia wa Tanzania? Uraia wake umetiliwa mashaka siku nyingi sasa na sijasikia hoja zozote, licha ya kuhusishwa na kashfa mbalimbali za ufisadi.

    ReplyDelete
  4. Sijawahi kusikia upuuzi wa maelezo uliotolewa wa CCM, juu ya huyu Kijana

    ReplyDelete
  5. Nyerere pia sio raia ni Mrwanda, baba yake anatokea Rwanda...

    ReplyDelete
  6. HILI LIWE FUNDISHO KWA WALE WANAODANDIA CCM NA KUJIONA KUWA WAMEFIKA, KWANI WANASAHAU KUWA WALISHA AMBIWA KUWA CCM INA WENYEWE. POLE BASHE WEWE SI WAKWANZA KUPATA DHORUBA YA KUNYANG'ANYWA URAIA WAKATI WA UCHAGUZI KWANI WAPO AKINA ULIMWENGU, DOKTA REMMY ONGALA NA WENGINE AMBAO HAIKUWEZEKANA KUNYANG'ANYWA URAIA SHUGHULI ZAO ZA KIMAISHA ZILIPIGWA KUFULI MPAKA WAKARUDI CCM NDIPO WAKAFUNGULIWA.

    ReplyDelete
  7. Hayo ndio mambo ya Sisim. Hata kama si raia wa Tz, ukiwa na hela tu na ukajiunga na Sisim, basi wewe utapata ubunge, uwaziri, nk. Watu wa aina hii wapo wengi. Hatari kweli

    ReplyDelete
  8. Wazee wetu wanatuaibisha sasa. Chiligati naye atuambie huo ushauri ameupata toka kwa wanasheria gani ili watupe ufafanuzi zaidi.
    Jamani mbona hiyo kitu ni rahisi sana ? Mtu kazaliwa Tanzania na wazazi wake hawakuwa wawakilishi wa nchi yoyote ile ya nje kama vile afisa wa ubalozi, huyo mtu ni raia. Haya yote sasa yanakuja vipi ?
    Na mhishimiwa sana Makamba kukataa barua rasmi ya uhamiaji ambayo imethibitisha uraia wake, inabidi atuambie yeye au hao wenzetu ni chombo gani wanakiamini na kukitumia katika mambo ya uhamiaji ambacho kikatiba kinashughulikia mambo hayo.Mbona wazee wanataka kutuburuza tu kila siku ?
    Idara ya Uhamiaji si idara harali ya Serikali ambayo CCM inaiunda ? Sasa leo hii Makamba kusema CC inavigezo zaidi ya hivyo, basi na watuambie hivyo vingine ni vipi. Ama la hapo ni kutuchezea zumbukuku na swaumu hii jamani.
    Nadhani nilimuona pia Mh. sana Mwakyembe mle ndani. Najua yeye ni mwalimu mzuri tu wa sheria. Hivi ni Constitutional lawyer right ? Sasa nini kimetokea mzee? Huku ndani shule yako yote taifa iliyokulipia imeshindwa kufanya kazi ? Umeshindwa kabisa kuwafadanulia wenzako? u mkiwa huko ndani mambo mnayaendesha kinyume? Sasa kama issue ndogo kama hiyo ile top cream ya Taifa inachemsha. Kwenye issue ngumu inakuwaje? Ndiyo maaana watzanzania hatuishi kuona vioja kila kukicha. Sasa mnatulazimisha kuchoka !!

    ReplyDelete
  9. Nawashangaa wanaolishangaa hili. Hii ndiyo CCM ndugu yangu ambayo baada ya kula nyama ya mtu ina kiu ya kurudiarudia kula kila siku.
    CCM ni wanafunzi wabaya kabisa wa Mwalimu na kwa kweli hawamuenzi kwa lolote ila unafiki wa waziwazi. Mwasisi wa chama chao hayati Baba wa Taifa aliwaonya dhidi ya rushwa; na sasa ndiyo vinara wa dunia kwa hilo. Aliwaonya dhidi ya ubaguzi akisisitiza kwamba dhambi ya ubaguzi haiishi na kuifananisha na mtu aliyeonja nyama ya mtu ambaye kwa kawaida hupagawa na kuitafuta kila kukicha bila kuridhika ...na sasa ndiyo vinara wa hilo. aliwaonya dhidi ya kujilimbikizia mali na sasa mali ndiyo kipimo cha kuheshimika ndani ya CCM, bila ya kuwa na chochote au kuwa wa jamii fulani (Ukoo wa vigogo) huwezi kupata nafasi ya kuwa hata mwenyekiti wa kitongoji kupitia CCM! kimbilio pekee la wanyonge sasa ni kile chama alichokipa dole akiwa hai alichosema kina sera "nzuri sana" ingawa kwa wakati ule alisema kilikosa mtu wa kuzitafsiri sera zao kwa wananchi - CHADEMA; - Nguvu ya umma. Nina uhakika kama angekuwa hai leo hii Nyerere angesharudisha kadi ya manyang'au hawa wezi wakubwa na wala rushwa CCM.
    Ni CCM imetuingizia utamaduni wa "kulinajisi" Bunge kwa kutoa visingizio vya kisheria ili kuruhusu vibakauchumi watuwakilishe kwenye nyumba ile takatifu na tukufu ati kwa kisingizio cha hawajahukumiwa, wakati mtuhumiwa wa wizi wa kioo cha gari anasimamishwa kazi hadi Mahakama iamue. sishangai kamwe kusikia wamewapitisha mafisadi (vibakauchumi) walewale kwani ni "wenyewe" katika CCM na ni "wenzetu" katika udokozi na uhujumu uchumi. Wananchi tuamke sasa CCM ni marehemu, amekufa, ameoza hana uwezo wa kutuongoza. Oktoba 31 tufanye uamuzi washtuke kama wamebanwa na mlango.
    Mungu ibariki Tanzania; CHADEMA oyee ...Peoples Power.

    ReplyDelete
  10. Hivi misupu kwenye katiba ya TZ haisemi kuwa mzaliwa wa Tz ni mTz? Nilikuwa nafikiria hivyo siku zote na sijawahi kuisoma hiyo katiba lakini nimewahi kusikia kuwa kuna wenzetu wengi tu ni raia wa kuzaliwa!!

    ReplyDelete
  11. Naomba nikusaidie. utangulizi ndio huo uliopo. Na ufafanuzi wa yeye kuondolewa ni kwamba alizaliwa Tanzania ndiyo lakini wakati huo baba yake alikuwa msomali. Na baba alipata uraia miaka kumi baadaye.
    Selelii aliyeshika nafasi ya pili katika kura za maoni naye ameondolewa na nafasi hiyo kupewa aliyeshika nafasi ya tatu kwa maelezo kuwa, mbunge aliyekuwa akiongoza jimbo hilo (Selelii) kuachwa mbali kwa kura zaidi ya 12,000 ni soo

    ReplyDelete
  12. kaka binadamu wote ni sawa hakuna cha msomali wala nini immigration wamesha clear issue nenda chadema mkutane jimboni wanakuchelewesha hao jimbo lako lile.

    ReplyDelete
  13. hawaja mtendea haki ccm bwana wanafiki sana cjui y,angalia watoto wao wamewapa madaraka je wakina rostam wao raia,ni vile tu rostam anaendesha nchi na pesa zake,sasa mwanae kabaka awaite nec na huko

    ReplyDelete
  14. Hii ni Double standard ya ccm, mbona kina kinana bado wanapeta na ukada?wakati uraia wake ni utata?
    Michuzi usichunie maana siajtuka mtu hapa just my thought

    ReplyDelete
  15. YOTE KWA YOTE, HIVI MWENYE MAMLAKA TANZANIA KISHERA KUTAMKA FULANI BIN FULANI SI RAIA WA TANZANIA AU NI RAIA WA TANZANIA NI NANI? CHILIGATI AU MKURUGENZI WA UHAMIAJI? HII NI HATARI SANA, VIONGOZI WANAPASWA KUWA MAKINI NA KAULI ZAO. MATOKEO YAKE WANACHEKESHA, HAYA SASA KIJANA KAWASILISHA UTHIBITISHO WAKE KUWA NI RAIA. JE YAKO WAPI?

    ReplyDelete
  16. Hussein Bashe si raia...

    kama baba yake ni raia wa tanzania kwa kujiandikisha... basi sheria inasema tu kwamba watoto wa raia huyo hawawezi kuwa raia automatically kwani baba yao hakuwa mtanzania wa kuzaliwa... ni baba mtanzania wa kuzaliwa ndiye pekee anaweza kumpasia mtoto wake utanzania na si vinginevyo...

    ReplyDelete
  17. Anony wa kwanza,
    Hussein Bashe ni kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, yumo kwenye Baraza Kuu. Ni mfanyakazi kwenye kampuni za Rostam Aziz. Wazazi wake walitoka Somalia, wakaja nchini na baada ya miaka 10 wakapata uraia. Yeye alizaliwa Tanzania kabla ya wazazi wake hawaja[ata uraia. Hata hivyo, mwaka jana alikwenda mahakamani na akaapa kukana uraia wa awali wa baba yake na Uhamiaji wamethibitisha hilo. Hivi sasa wazee wake wako Nzega, Tabora ambako ndiko alikoshinda kura za maoni dhidi ya Mbunge machachari kwenye kambi ya makamanda wa vita dhidi ya ufisadi.

    Huyu kijana ni majeruhi wa siasa chafu za Bongo. Tatizo limeanzia huko Umoja wa Vijana ambako kuna buzi dume limebarehe sasa linabashia kila mtu. Nenda mitaani kaulize hilo buzi dume ni nani.

    Lakini pia hakuna haja kuficha ukweli, dogo huyu naye hayuko peke yake.

    Tanzania ina kazi huko mbele.

    Michuzi weka hii watu wajue mambo.

    ReplyDelete
  18. Hawa sisiemu wanajiona wako juu ya mamlaka nyingine, mbona wanamuonea mtoto wa watu.Mkulo walipoambiwa ni raia wamemuacha lakini Bashe walipoambiwa ni raia Makamba anakataa. Tena huyu Makambe anaeelekea kuharibu Chama. Mwenyekiti muondoe haraka ataua Chama kwanza ana majibu ya Kibabe.

    ReplyDelete
  19. Kwa kweli sasa wazee wetu sasa wanazeeka vibaya na haki sasa haitendeki !
    Bashe namfahamu ni kijana wa kitanzania ambaye baba yake ni msomali mwenye uraia wa TZ!Amezaliwa, kukua kusoma mpaka chuo KIKUU MZUMBE na kufanya kazi NMB na kuwa na vyeo vingi kwenye chama cha CCM.
    MAMA YAKE MZAZI NI MTANZANIA na yeye ameukana uraia wa Somalia.

    SASA KUMKANA SASA HIVI HUO NDIO UONGOZI BORA KWELI????? NAOMBA CHAMA KIWE MFANO WA UONGOZI ULIOTUKUKA JAMANIIIIII wanbatufundisha nini sasa???

    ReplyDelete
  20. naombeni kuuliza wajameni, huyu jamaaa lazima atakuwa anasafiri ndani na nje ya africa,na kama inavyojulikana lazima mtu ukisafiri uwe na passport, sasa hiyo passport yake ni ya wapi? na kama ni ya kibongo, aliipataje ikiwa yeye sio raia kama wakubwa wanavyosema?
    nijuzeni

    ReplyDelete
  21. Wamarekani wakisema Obama ni Mkenya mnasema wabaguzi, sasa hii ni nini. Jamaa kazaliwa bongo ni mtz by birth sio by registration

    ReplyDelete
  22. ccm sasa hatuitaki narudisha kadi mchezo mchfu umezidi si makamba ,mwinyi hamna hta busara zilizotumika katika kuteua wabunge faulo nyingi tu ,na kama bashe kazaliwa tanania ni raia tayari hana haja ya kuomba wewe chiligati shule gani umesoma mbona unaaibisha kama hujaenda shule?na huyo sitta sijui mmemrudisha wa nini maana rushwa zilikua zinatawala hata hiyo takururu ilikua haifanyi kazi kashinda kwa nguvu ya pesa,ccm mafala

    ReplyDelete
  23. Michuzi ni raia wa Uganda, kwa hiyo bwana kuanzia leo sitambui michuzi blog, and you never existed in our mind, so do your blog.

    inabidi ubadilishe michuzi blog, to buganda blog, halafu michuzi blog umuachie eeh mmmmh!! michuzi lakini mdogo wako kwa sababu kazaliwa dar halafu baba ni raia wa uganda lakini tunampenda yeye kwa sababu ni CHADEMA, ambako matatizo haya hatuna.. I AM CONFUSED...

    ReplyDelete
  24. triki ya ccm ukiwazidi.

    mi hii nchi siipendi kabisa, yaani ukifanikiwa kidogo we sio raia.

    lini tutakuwa washindani wa kweli?

    ReplyDelete
  25. Yaani siku zote hawakumuona? vyeo vyote alivyoshika CCM miaka yote hawakuviona? leo hii ndio wanaquestion Uraia wake. Ondoka huku kaka achana na chama cha wazee hicho hakina HAKI Akili zao zimezeeka wanabaki kuwapa watoto wao madaraka. Achana nacho njoo CHADEMA CHAMA CHA WATU, peoples part na sio chama cha wenyewe! CCM inawenyewe na wenyewe si walala hoi. Njoo tupiganie haki CHADEMA Hoyyeeeee

    ReplyDelete
  26. Hivi Hussein Bashe naye akizaa mtoto, huyo mtoto atakuwa raia wa Tanzania au Msomali, maaana uraia kwa mujibu wa sheria za Tanzania haurithiwi, kama mtoto hawezi kurithi uraia wa hussein basi mtoto atakuwa hana uraia wa nchi yoyote.

    ReplyDelete
  27. NI NGUMU SANA KUWAELEWA CCM NA SERIKALI YAKE HASA KUHUSU SWALA LA RAIA WA KIGENI. KWAMBA CCM INAPOKUWA NA HAJA YA KUMTUMIA MTU KWA MANUFAA YA CHAMA , HAIANGALIA KWA UNDANI URAIA WA WANACHAMA WAO... ILA MWANACHAMA HUYO ANAPOTAKA KUINGILIA ULAJI WA WAKUBWA NDIPO URAIA WAKE UNAPOANGALIWA KWA UPANA ZAIDI ILI KUMWANGUSHA. HUO NI MCHEZO MBAYA SANA!!

    MFANO MZURI NI WA HAPA NCHINI ITALIA KUWA HUYO CHILIGATI ALIMPA BARAKA RAIA WA ITALIA NDUGU ADBULHARMAN KOSHI KUANZISHA TAWI LA CCM NAPOLI. ITALIA ILHALI AKIJUA WAZI KUWA HUYO BWANA SI RAIA WA TANZANIA NI RAIA WA ITALIA. KWA VILE ALITAKA TU CCM IFUNGULIWE NCHINI ITALIA... HATA KAMA MWENYEKITI WA TAWI HILO SI RAIA WA TANZANIA.

    TENA MWENYEKITI HUYO WA TAWI LA CCM NAPOLI ANAPOKUJA ITALIA HUPITIA KWENYE UBALOZI WETU WA TANZANIA ROMENA KUOMBA VISA YA KUINGIA TANZANIA. UBALOZI UNAJUA KUWA HUYO NI RAIA WA ITALIA ILA NI MWENYEKITI WA CCM TAWI LA NAPOLI ITALIA.
    LAKINI HAKUNA MTU ALIYEWEZA KUULIZA WALA KUKEMEA!!! KWA SABABU TU HUYO BWANA HAJAGUSA INTERESS ZA WAKUBWA.

    MWEZI WA SABA MWAKA HUU MWENYEKITI HUYO WA TAWI LA CCM NAPOLI - RAIA WA ITALIA NA KATIBU WA TAWI HILO - NDUGU NZANGU KAGUTA.. AMBAYE PIA KWA ASILI NI RAIA WA RWANDA, WALIKUJA TANZANIA KAMA KUWAKILISHA CCM MATAWI YA NJE KWENYE MKUTANO WA KUMPITISHA MGOMBEA WA CCM KWENYE UCHAGUZI MKUU UJAO. TENA BILA AIBU MWENYEKITI HUYO ALIPITA KULE UBALOZINI KWETU ROMA NA PASIPOTI YAKE YA KIITALIA KUOMBA VISA YA KUINGIA TANZANIA . BADO HAKUNA HAKUNA MTU ANAYEMSHANGAA KUVAA UENYEKITI WA CC NAPOLI.. NA LEO PICHA NYINGI ZIMEENEZ KWENYE BLOGU SPOTI YA WATANZANIA ITALIA AMBAPO AMEWEKWA MWENYEKITI WA CCM TAIFA MZEE KIKWETE AKISALIMIANA NA MWENYEKITI WA CCM TAWI LA NAPOLI ITALIA, RAIA WA ITALIA (AIBU) LAKINI HAKUNA MTU WA CCM KUANZIA CHILIGATI HATA MAAFISA WETU WA UBALOZI ITALIA WANAOULIZA UHALIA WA RAIA WA NJE KUWA MWENYEKITI WA CCM TAWI LA NJE. MAMBO SAWA! MSHIKEMSHIKE! CCM OYE!!! HII NI AIBU YA KIUTENDAJI KWA CHAMA CHA MAPINDUZI.

    ILA KESHO NDUGU ABDULHARMAN KOSHI AKIJA NA WAZO LA KUGOMBEA UBUNGE ... NDIPO PALE CHILIGATI ATAKAPOSITUKA NA KUJA NA HOJA YA KUWA HUYO SI RAIA WA TANZANIA.... KWA SABABU YA KUTAKA KUGUSA ULAJI WA WAKUBWA KWA KUGOMBEA UBUNGE!!!

    HUU NI UHUNI MKUBWA SANA KWA VIONGOZI WETU!!!!

    Mtanzania – Ascoli, Italy.

    ReplyDelete
  28. Hawa kina Chiligati na Makamba mbona wanachanganyana, Makamba anasema Uhamiaji wame mclear kua Raia lakini Chiligati anadai Uhamianji hao hao wamedhibitisha jamaa si raia sasa tuamini nini? Na kama CCM inachukua uamuzi wa kumuhukumu huyu kijana basi wawatume polisi wamkamate maana amaevunja sheria ya nchi kwa kukaa kinyume cha sheria. I love America kwa sababu haya mambo ya shetwani huwezi kuyasikia and i will never leave this country..God Bless USA...Amen

    ReplyDelete
  29. Kwanini mtoto anayezaliwa na mama wa kitanzania lazima akane uraia wa baba yake anapofikia umri wa miaka 18 ili aweze kuwa mtanzania, lakini yule wa baba wa kitanzani hahitaji kufanya hivyo? Kwanini Tanzania kusiwe na haki sawa kwa wanawake na wanaume? UWT fuatilia hili.

    ReplyDelete
  30. SASA NDIYO WANAMSHTUKIA BASHA WAKATI WAMESHAKUWA NAYE KWA MUDA MREFU. HII INAONYESHA UDHAIFU MKUBWA SANA KWENYE TAASISI ZETU.

    LAKINI PIA CCM WASILAUMIWE SANA. KWANZA, UKIANGALIA VIELELEZO VYA BASHA UTAONA AMEANZA KUSHUGHULIA URAIA WAKE KARIBUNI TU (2008). PILI, HUKU KWETU MASUALA YA KUTENGENEZA NYARAKA NA KUBACKDATE BADO YANAWEZEKANA. NDIO MAANA KILA MHUSIKA WA KARIBU NA MASUALA YA UHAMIAJI ANAJARIBU KUKWEPA.

    LAKINI KITU KIMOJA TUKUBALI, TUNAIWEKA NCHI REHANI - KWELI. KUNA UWEZEKANO MKUBWA KWAMBA KUNA SIKU TUTAKUJAMKABIDHI NCHI MTU AMBAYE SIYO RAIA.

    ReplyDelete
  31. This is totaly racism yani mi ni mgogo lakini naogopa nikijapata mafanikmio au kutaka nafasi flani flani nitaambiwa ni kutoka Chad..

    Mungu Tunaomba utuokoe na hii dhambi mbaya kabisa...

    ReplyDelete
  32. Ndugu yangu Hussein, kweli wewe ni mtu makini na kada kwelikweli na tunakufahamu hivyo kwa muda mrefu.
    Kama ulivyosema kuwa hili swala ni la kisheria zaidi, kaa chini na wanasheria wako mliangalie. Matokeo yeyote yale mtakayoyapata, kijulishe chama chako, then you will get a way forward. Wewe si wa kwanza kukutwa msukosuko kama huo, Castico alipata tatizo kama la kwako lakini alirekebisha mambo na then ameendelea na kukijenga chama.

    ReplyDelete
  33. KIjana makini sana huyu, yaani hana papara, haoneshi hasira pamoja na kushinda ushinda wa Tsunami.

    I am 100% he is legally a citizen na he will make a great politician.

    Good luck Mh. Bashe, siasa ndioo zilivyo, vikwazo na kero za hapa na pale is the order of the day.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  34. HII NI AIBU TUPU KWA CCM. JAMANI KWANI MTU AKIPEWA URAIA SI ANAPEWA PAMOJA NA WATOTO WAKE AMBAO HAWAJAKUWA WATU WAZIMA. HUYU KIJANA BABA YAKE ALIPATA URAIA WAKATI AKIWA MINOR SASA HUYO BABA ALITAKIWA AWAACHE WATOTO WAKE NCHI NYINGINE AU VIPI. JAMBO HILI LINATOKEA NCHI ZA KIDIKTETA PEKE YAKE. MIMI NINAVYO FAHAMU NI KWAMBA MTANZANIA NI YULE MTU AMEZALIWA TANZANIA AU MZAZI WAKE MMOJA AU WOTE WAWILI NI WATANZANIA. HUYU KIJANA JAPOKUA MZAZI WAKE HAKUA MTANZANIA ALIPOZALIWA LAKINI YEYE ALIZALIWA TANZANIA. SAFARI HII CCM MMEJIAIBISHA SANA. KWANINI MGEUZE CHAMA CHETU KUWA CHAMA CHA WAHUNI. KWAKWELI NINGEPENDA SANA RAISI KIKWETE AENDELEE NA KAZI YAKE NZURI ALIYOIFANYA KWAHIYO NAMSIHI ASHUGHULIKIE HILI JAMBO.

    ReplyDelete
  35. hongera michuzi kwa kutuletea issues kama hizi. haya ndio mambo yakuyaacha humu kwenye blog ili watu wayajadili.

    ReplyDelete
  36. HEBU ELEWENI SHERIA ZA URAIA UPANDE WA BASHE BABA NA MAMA WOTE SIO RAIA WA TANZANIA KWA HIYO NA YEYE HAWEZI KUWA RAIA WA TANZANIA KAMA MMOJA WA WAZAZI WAKE ANGEKUWA RAIA BASI BASHE ANGEPEWA URAIA SI KWA SABABU YA BABA YAKE HATA KAMA MAMA ANGEKUWA MTANZANIA BASHE ANGEKUWA RAIA TATIZO WAZAZI WOTE HAWAKUWA RAIA

    ReplyDelete
  37. .........ACHEN UPUUZI HUMU...NENDENI SOMALIA MKAOMBE URAIA MUONE BALAA LAKE !! KAMA BADALA YA KUPEWA WANAKUUA KABISA....

    BASHE SI RAIA , NA ARUDI SOMALIA ASIPEWE KABISA,

    CASE CLOSED!

    ReplyDelete
  38. Wewe ndio mpuuze, kutuletea ubaguzi. Watanzania wangapi wameenda majuu na wakajipa kisomali bila hao wasomali kuwasema? Mbona kuna raia wa kisomali wenye asili ya kitanzania huko somalia? Ndugu nchi haiendi mbele na ubaguzi.
    Tumewasaidia south africa na ukienda huko watakunyonga lakini sisi hatuwaoneshi hayo chuki raia wao.

    CCM inawatu wao na vijana so wao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...