JE, “ENGINEER” NI TITLE KAMA
ZILIVYO DOCTOR NA PROFESSOR?
Michuzi,
Miongoni mwa Watanzania wanaoishi ughaibuni pengine wanaweza kuwemo baadhi ambao hawajasikia au kusoma jambo hili lakini wale tulio Tanzania na wengineo tumeshasoma na kusikia kituko ambacho kwa kweli kinashangaza. Kumezuka mchezo mchafu miaka ya hivi karibuni wa watu kujipachika vyeo ambavyo duniani kote havipo, mfano utasoma kwenye magazeti au kusikia redioni na kwenye TV mtu akiitwa kwa mfano “Engineer James Mkama” (huu ni mfano tu wa jina).
Hakuna mahala popote duniani ambapo Engineer au Mhandisi ni title kasoro Tanzania. Titles zinazotambulika ulimwenguni ni kama Doctor, Professor, Captain (wa meli au ndege), vyeo vya jeshini, Justice na vinginevyo.Mfano, ukifikia kiwango fulani cha elimu (mfano Doctorate) katika taaluma fulani basi unatunukiwa title ya Doctor. La kushangaza ni kuwa wahandisi ni watu walioelimika lakini iweje wafanye vioja vya namna hii? Kwa kweli ni aibu pengine kwa taifa maana tunaonekana kama watu tusiojua maadili ya taaluma. Ajabu pia ni kwamba hata bungeni unasikia mtu anaitwa “Engineer Stella Manyanya”, vipi jamani, hivi watu wanatafuta nini?
Yuko mwingine anajiita “Advocate Nyombi”. Hivi kama Advocate na Engineer ni titles basi tuseme Accountant, Auditor, Teacher, Chef, Technician, Psychologist, n.k. nazo ni titles, maana yake basi watu wanaweza kuamua kujiita chochote wanachotaka ili mradi ndiyo taaluma yao.
Nilimuuliza mtu mmoja kutoka kwenye mojawapo ya magazeti ambayo yanawatambua watu hawa kwa titles hizo za miujiza na jibu alilonipa ni kuwa eti wenyewe hao ma-engineer ndiyo wameagiza waitwe hivyo. Swali langu lililofuata kwake ni kama amewahi kuona au kusikia mtu akiitwa Engineer Fulani popote duniani lakini upeo wake ulilazimu mjadala umalizike haraka.
Vyombo vya habari vinatumika kuielimisha na kuipa habari jamii, lakini nchi ipo hatarini iwapo vyombo vyenyewe vinakuwa mstari wa mbele kupotosha mambo, nchi inaangamia hii jamani.
Mdau Kim.
Michuzi,
Miongoni mwa Watanzania wanaoishi ughaibuni pengine wanaweza kuwemo baadhi ambao hawajasikia au kusoma jambo hili lakini wale tulio Tanzania na wengineo tumeshasoma na kusikia kituko ambacho kwa kweli kinashangaza. Kumezuka mchezo mchafu miaka ya hivi karibuni wa watu kujipachika vyeo ambavyo duniani kote havipo, mfano utasoma kwenye magazeti au kusikia redioni na kwenye TV mtu akiitwa kwa mfano “Engineer James Mkama” (huu ni mfano tu wa jina).
Hakuna mahala popote duniani ambapo Engineer au Mhandisi ni title kasoro Tanzania. Titles zinazotambulika ulimwenguni ni kama Doctor, Professor, Captain (wa meli au ndege), vyeo vya jeshini, Justice na vinginevyo.Mfano, ukifikia kiwango fulani cha elimu (mfano Doctorate) katika taaluma fulani basi unatunukiwa title ya Doctor. La kushangaza ni kuwa wahandisi ni watu walioelimika lakini iweje wafanye vioja vya namna hii? Kwa kweli ni aibu pengine kwa taifa maana tunaonekana kama watu tusiojua maadili ya taaluma. Ajabu pia ni kwamba hata bungeni unasikia mtu anaitwa “Engineer Stella Manyanya”, vipi jamani, hivi watu wanatafuta nini?
Yuko mwingine anajiita “Advocate Nyombi”. Hivi kama Advocate na Engineer ni titles basi tuseme Accountant, Auditor, Teacher, Chef, Technician, Psychologist, n.k. nazo ni titles, maana yake basi watu wanaweza kuamua kujiita chochote wanachotaka ili mradi ndiyo taaluma yao.
Nilimuuliza mtu mmoja kutoka kwenye mojawapo ya magazeti ambayo yanawatambua watu hawa kwa titles hizo za miujiza na jibu alilonipa ni kuwa eti wenyewe hao ma-engineer ndiyo wameagiza waitwe hivyo. Swali langu lililofuata kwake ni kama amewahi kuona au kusikia mtu akiitwa Engineer Fulani popote duniani lakini upeo wake ulilazimu mjadala umalizike haraka.
Vyombo vya habari vinatumika kuielimisha na kuipa habari jamii, lakini nchi ipo hatarini iwapo vyombo vyenyewe vinakuwa mstari wa mbele kupotosha mambo, nchi inaangamia hii jamani.
Mdau Kim.
Kwanza inabidi uainishe 'title' unamaanisha nini. Je, ni 'Professional title' ama 'Academic title'. Vyovyote vile ni sahihi kwa Engineer. Kama unamaanisha professional title; mtu kuweka Engineer kwenye jina ni sahihi, hata huku Ujerumani wanaweka. Ki'academic hasa wengi ninaona wanaandika B.Eng baada ya majina yao: mfano, M Luhanga, B.Eng
ReplyDeleteUpo?
hiyo ndio bongo......tambarare......utajiju.
ReplyDeleteSiku hizi hata kuoa ni cheo.MME James,au MKE Zuhura kama ilivyo bin Seyyid au ibn kwa kiarabu.
mdau kumbe umeona eeh.hii nchi wewe acha tu.wanafikiri ma-dr wengine ni wa hospitali ndio maana wahandisi nao wakaona ngoja na sisi tujipachike title.kuna vitu viko tanzania tu,subiri uone utakavyoshambuliwa.
ReplyDeleteSasa tutajuaje kama umesomea nini??
ReplyDeleteKatika hali ambayo bado binadamu tuna udhaifu (na hii ni asili yetu) ni lazima mtu utangulize nguvu fulani kuonyesha nafasi yako katika jamii.
Hii wataalamu wanaiita "borrowed strength". Kwa mtu aliyekamilika hana haja ya kuweka kitangulizi chochote mbele ya jina lake kwani wasifu au qulaification zake zinaonekana kwa matendo yake, maneno yake (au hata kwa ukimya wake), na haiba yake kwa ujumla alivyo.
Itakuwa ngumu kuwashawishi watu kuhusu jambo hili kwakuwa tumebobea sana kwenye hizi taratibu kiasi kwamba atakayekwambia tofauti utamwona ni chizi au punguani, au aliyeshindwa kupata hizo "titles".
Kama ilivyo vigumu kumsimulia samaki kuwa kuna maisha nje ya maji (hajawahi kuishi huko), ndivyo hivyo hivyo baadhi ya watu watashindwa kukubaliana nami kuwa, Just a name without any qualification can do".
Mpaka hapo tutakapozinduka, ruksa kuendelea kutumia hizo titles: Dr, Prof, Eng, Mwalimu, Mhasibu, "Fisadi", Mh. etc etc!!
Nafikiri mdau unajichanganya na kujikoroga mwenyewe. Mtu anafahamika kwa title yake zaidi nafiri hiyo ni heshima anayostahili kuitwa kama ana wadhifa huo, titles zote ni sawa inategemea ni wapi zinatumika. Kama title ya mwalimu Nyerere hata kama alikuwa rais wa nchi lakini aliendelea kuitwa mwalimu katika maisha yake kwa vile alikuwa mwalimu. Si lazima awe daktari wa filosofia fulani. Mtu kuitwa kwa title ya engineer mimi hapo sioni tatizo lolote, kwani kuwa engineer hiyo nayo ni taaluma mpaka kufikia kiwango cha engineer. Tatizo lako mdau una inferiority conflicts na unahitaji msaada one on one ili kuelimishwa kuhusiana na maswala ya title. Acha watanzania wawe watanzania na waitane kwa jinsi yoyote wanavyojisikia, Mheshimiwa mbunge wa Kyela...., mwanasaikolijia fulani, engineer Limo, Daktari Masawe, Mwalimu Kweka, Profesa Ndesamburo, Mwanazuoni Malecela nk. Wala usisumbuke kutafuta ushauri its the matter of using comon sense. To me I see no problem for someone to be called by his/her title! I am an Engineer myself, when I attend any meeting I introduce myself as an engineer so and so, and no body ever complained na nipo ughaibuni for decades.
ReplyDeleteAsante mdau ninamatumaini hautaendelea kusumbuka na title za watu tafuta yako.
MDAU WA DAMU USA
Accountant, Auditor, Teacher, Chef, Technician, Psychologist. Pia unaweza kutumia Kama kweli una vyeo hivyo sawa tu Teacher si Wengi Tunasema Mwalimu Mtiga au Mwalimu Cocu. USA mpaka aliyekuwa Mwizi anaitwa Former Thief. MZ.
ReplyDeleteKwani titles lazima zianzie ulaya kwani sisi hatuwezi hanzisha title hapa kwetu. hacha kuwa na mawazo ya kutawaliwa.
ReplyDeleteMhandisi Ali.
Wanataka heshima za kulazimishia ili waonekane nao wamesoma. Hilo pia linawasaidia kwenye kipato na hata kufikiriwa kwenye madaraka makubwa zaidi. lakini ukweli ni kwamba watu wanatushangaa na wanatuona hatuko serious na mambo ya muhimu.
ReplyDeleteWanafanya makusudi. Na huko bungeni ndiyo kabisa, siku hizi imekuwa ni kama mchezo wa kuigiza. Pamegeuzwa mahali pa watu kuhalisha ulaji wao na wanchi kuibiwa. Kazi mbona tunayo. Huruma inaenda kwa wale ambao upuuzi huu unawaathiri kwenye maisha yao. They are paying for it dearly. Mungu na awasaidie.
Engineer James Mkama au Eng. Stella Manyanya, Engineer /Eng. sio title bali ni salutation.
ReplyDeleteKwahio kama ukiamu kumwita mtu Advocate Kamata au Engineer Kamata Au Mwalimu Kamata, hakuna shida maadamu wanazo hizo taaluma. Mbona hujaulizwa kwanini yule alikuwa anambulika kama Mwalimu Nyerere?
Cha kuumiza ni pale mtu anaitwa/anajiita doctor ihali hana shahada ya juu ya 3 aka PhD.
Ntakupa mfano mwingine hapa nilipo Mkufunzi wa chuo kikuu anatambulishwa kama "Professor" kama hana PhD na mwenye PhD anatambulishwa kama "Doctor" Halafu kuingia kwenye "titles" huyo "Doctor" Anaweza kuwa "assistant Professor" au "Associate Professor" au "Professor".
Sasa sijui kinachokuumiza nini wewe Kim.
Salutations zipo nyingi sana tunaweza kuzijaza hapa kwenye page hii na tusipate muafaka.
SAMAHANI, TUAMBIE TAALUMA YAKO NINI BASI TUTAKUSALIMISHA NA WEWE
Main article: Professional Engineer
ReplyDeleteIn most Western countries, certain engineering tasks, such as the design of bridges, electric power plants, and chemical plants, must be approved by a licensed Professional Engineer, a Chartered Engineer, or an Incorporated Engineer. A licensed engineer often indicates the status with the use of post-nominal letters; PE or P.Eng is common in North America, EUR ING in Europe, while CEng and IEng is used in the United Kingdom and CEng in much of the Commonwealth.
Mdau mbona huna hoja!!! Kwani wewe ni nani alokukataza kuitwa Messenger Kim... Kama wametaka wao waitwe hivyo na mkakubaliana nao tatizo nini? Kama mnatamani na nyinyi mamesenja anzeni majina yenu na Ms... kama wewe vile ungeitwa 'Ms.Kim' hakuna anae kukataza... Usiwaonee wivu acha ma-advocate na ma-engineer waitwe kwa mujibu wa taratibu zao na wewe itwa kwa mujibu wa taratibu zenu.....
ReplyDeleteMada hii ni nzuri sana mdau. Nafikiri wadau watapokea vizuri na kuijadili.Utasikia muuguzi mwenya digree moja anitwa Doctor Rutachikozibwa(huu ni mfano)au Dr. Rutachokozibwa.Title hiyo haimtofautishi na yule mwenye Doctorate.Huyo muuguzi alitakiwa aandike jina lake "Rutachokozibwa MD" Yaani MD inasimama badala ya Medical Doctor.Mfano mwingine utasikia mtu anaitwa Mpiganaji Issa Michuzi bila kuonyesha alipigana vita ipi na nani. Mdau hii ni kasumba iliyoachwa na waingereza ya kuthamini sana title badala ya huduma yamtu kwa jamii.Kasumba hii ipo hata majumbani mwa wasomi wengi ambao utakuta wamebandika vyeti vyao ukutani ili kila anayeingia humo aone.Kupenda title kumekuwa pia ni tatizo kwa watoto wanaomaliza vyuo vikuu.Wanashindwa kujiajili,mfano,kwenda Singida kununua matenga ya kuku kwaajili ya kuuza Dar kwasababu hiyo kazi haina title.Wasomi wengi nchini wanaishindwa kubadilisha japo kidogo mazingira ya umasikini uliokithiri ndani ya jamii zinazowazunguka ingawa wana title kubwa.Title yako iende samaba na account yako ya benki,mahali unapolala na jamii inayokuzunguka.
ReplyDeleteI always laugh at that, but Nigerians do it too. Tena mpaka kwenye invites unaona imeandikwa Engineer ......., or at the end of the name kama vile PhD, MD etc.
ReplyDeleteCrazy!
Mkubwa uko sahihi kabisa. Unajua nchi hii tunakuwa kama wendawazimu, itafikia mahala hata taalum zinginezo zitaamua kujiita titles zao. Hii yote inapotoshwa na hizi board za hivyo vyombo husika. "Nguvu nyingi busara hakuna"
ReplyDeleteHilo ni kweli mdau, kwanni mimi nimeishi ulaya huu mwaka wa kumi lakini siwahi sikia hiyo tittle inavyotumika kama huko home. Kwa kweli inatia aibu. common ninyi waandishi tafuteni ukweli upo wapi badala ya kupotosha umma!
ReplyDeleteKim, Maelezo yako hayakuwa na utafiti wala uchambuzi wowote kabla ya kuandikwa. Sina muda wa kuandika imla ndefu kama yako ila nenda http://en.wikipedia.org/wiki/Professional_Engineer utaelimika.
ReplyDeletembona Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameitwa hivyo miaka yote hukuuliza, kwani wapi kwingine umewahi sikia 'teacher' inatumiak kama title?
ReplyDeletehii ndio bongo bwana!
Of course, waacheni wajiite "Engineer" kama wamesomea kazi hizo, mimi sioni tatizo, kama ni engineer mwacheni aitwe engineer, sioni tatizo kwenye hilo.
ReplyDeleteMdau
Finland
Hi Mdau,
ReplyDeleteHonestly mimi nafikiri mtu kutumia jina tangulizi la Eng. xxxxxx linahusiana na position yake katika hiyo fani ya Engineering,. normally watu ambao wako registered kama professional Engineers au consulting engineers huwa wanatumia hilo. It is very common in Middle East and Arab countries. Sidhani kama kuna tatizo hapo mtu kujiita hilo jina tangulizi kama ameweza kutimiza mahitaji ya kulitumia hilo jina tangulizi. Lakini sijawahi kuona mtu anatanguliza Teacher kama ulivyosema isipokuwa Mwalimu Julius K. Nyerere.... ambaye alitumia hilo jina ili aonekane mtu wa kawaida na pre-empty jina Mtukufu Rais J.K. Nyerere ambalo lilikuwa liwe automatic kwa position yake wakati huo. Maa-salaam
Ni kweli Mdau.
ReplyDeleteAcademic titles zina utaratibu wake na kamwe hakuna title kama hii ya kipuuzi ambayo iko Tanzania tu. Media zetu ni takataka zilizojaa mbumbumbu ambao hawaelewi maana ya doctor wala title yoyote ile na ndiyo maana wanamwita mtu yeyote tu, kama Dr. Mary Nagu kuwa ni doctor. Itakumbukwa hata mara baada ya JK kuingia madarakani na kumteau Masha, media ilianza kumwita Dr. Masha mpaka wajanja waliposema huu ni upuuzi ndiyo na yeye akaibuka na kukanusha kwamba yeye si doctor.
Kuna media ambazo mpaka zinaandika kwa Kiswahili, Injinia Mdudumtu. Ni upuuzi. Hakuna title kama hii duniani popote.
Aidha, niseme tu, kwamba wahandisi si wote ni wasomi. Kuwa na shahada moja siyo kuwa msomi hata kama wewe ni mhandisi. Hilo ndilo tatizo, wanataka kuheshimiwa. Nchi yetu ni ya kijinga sana, sijawahi kuona.
If are educated or not, Tanzanians have little understanding of the relevance of titles and honorific and also people like to keep their titles for life b'se in our poor country you can't go nowhere if you are nobody.
ReplyDeleteEngineer is not an honorific but a job title, however ignorance think it is a tittle and demand to be called an engineer with his/her job title.
People in development countries when introduced themselves you will never hear call themselves engineer so and so...normal they say I am so and so that is it. And if you have a long conversation and need to know what one is doing for living then that is the time you will here I am so and so and I am a civil engineer, mechanic engineer etc etc.
Also another thing that ticks me off so much is if at all, “ambassador” is a title that should never kept for life. It should be correctly used as “former ambassador” as he is no longer servicing. But you will hear ambassador so and so, mheshimiwa so and so.... Long after their jobs were over, either through defection and retirement they should hand over those titles to their successors too.. Why is it then that people who have left their offices long ago, or defected for that matter, think they are still holding on to their jobs? Still mhesimiwa for life! Those are not titles for life. ..
Engineer sio cheo cha kuwekwa mbele. Tanzania watu wanapenda sana misifa, hivyo sioni ajabu. Bungeni, wabunge ndo wameanzisha huu mchezo mchafu na sioni ajabu wakitunga sheria kuhalalisha kuitwa hivyo n kujikuta mbunge anatambulishw kwa kuitwa Mh Engineer MP stella Manyanya, MSC UK, Mbunge wa karatu ... lol. Hawa wengine wa makzini wamejiita kwa kufuata au kuona wabunge waliojitundika vyeo na pia kuona waganga wa kienyeji hawaulizwi.
ReplyDeleteKIM zamani Maengineer pale UDSM FOE walikuwa miungu watu wanaotisha kila mtu, wanapunch watu, wana meza yao hasa wale wa fourth year walikuwa wanaogopwa kweli kweli. Na tena walikuwa wanajiona wao ni muhimu chuo kizima, wengine wote hawana la maana wanalosoma.
ReplyDeleteBahati mbaya huku mtaani hakuna aliyekuwa anatambua huo ubabe wao, sasa naona ndio wakaamua kuwa ili na mtaani watambulike kuwa wao ni vijogoo wa kisomi bora waendelee kujiita Engineer So and So, na tena ni lazima wawe registered kwenye whatever society au sijui Registrar wao. Hao ndio maengineer wetu, lakini pamoja na kujitukuza kote huko mbona bado tunatumia wataalamu kutoka nje kwenye miradi yote ya Ujenzi wa barabara, madaraja, na hata sekta ya umeme na kemikali? Tunashindwa hata na mainjiia wa India ambao wamewezesha nchi yao kusonga mbele kwa sekta ya ujenzi na nyinginezo. Reli tu ya kati inawashinda mainjinia wetu!
Ilitokana na kuwaita ma- Medical assistant -Madaktari, na ma-civil technician- Mainginia.
ReplyDeleteHalafu siku hizi wsiokuwa na shule wanajipachika "aka" mataluma, maana hakuna cha kujiita ila jina jipya.
Haya mambo yangetakiwa yaanzie kwa ankal Michuzi. Mambo ya kuita watu my wife husband sijui nini sio kuelimisha umma ila ni kubomoa. Halafu watu wengine wanasupport kwa kusema hicho ni lugha ya hii blog...Hiyo sio kuelimisha watu na umma..Ni upotofu na mwishowe mazoea hujenga tabia...Does this mean that we should never correct our children's language mistakes? kama sisi wenyewe tunakumbatia na kusema hii ni langueage ya michuzi blog...
ReplyDeleteKwani hujawahi sikia mtu anaitwa Mwalimu Nyerere? Au Judge Judy au Sheriff/Cheif etc
ReplyDeleteKutumia cheo au Title ni inavyoonyesha jinsi ulivyokuwa proud of your title or archievment. Ni kama hapa USA, Register Nurse hutumia RN kujitambulisha, sawa na wanasheria, MD na Engeneers. Sasa si kosa kwa Engeneer kijitambulisha tena USA ndio inatumika kupita kiasi tena wanavuka mipaka zaidi kuonyesha ya kuonyesha amesajiliwa na board zipi. I am Engineer tena very proud of my title.
ReplyDeleteKaka, hongera kwa utafiti wako ulioweka kwenye blog, japo ww umeita swali la kizushi. Kuna mambo mengine huwa ukisikia unayachukulia juju bila hata ya kuwaza, lakini uvumbuzi huu ni mzuri kuelimisha jamii yetu hasa kwa wale wanaopenda kujikweza. Mtu utakuta ana "degree" kwa sababu eti kasomea uhandisi basi anajiita "engineer" hiyo degree haina tofauti na degree nyingine zozote zile. Kila mtu akiwa anajiita kwa title ya degree yake aliyosomea bai itakuwa balaa. Nawaomba wahusika hasa bodi ya elimu ya juu iitolee ufafanuzi maada hii ili kuwekana sawa. Mdau kuna mtu umemtaja humu kuwa anajiita "Advocate Nyombi" Ninamfahamu mtu huyu kwa ukalibu sana, hili ni jina lake tuu wala halihusiani na taaluma ya uwakili. Nakutakia kila rakheli mdau. Misupu tutafurahi kama tutapata ufafanuzi kutoka Elimu ya juu, kuhusu suala hili.
ReplyDeletenami nitaomba nitambuliwe Mkulima fulani......Mk.Funga Meza
ReplyDeleteyani hii aingii akilini kabisa huyo ndiyo ufinyu wa wanasiasa wet wenye elimu ndogo wanalazimisha vitu wako radhi kupata digiri kutoka kwa mashine ya kusagisha digirii.sasa tusubirie na lawyer
Hili jambo limekuwa likinisikitisha sana, Kuna ma-engineer wazito wa NASA, na taasisi nzito ulimwenguni, kuna wataalamu wa taaluma mbalimbali lakini hatujawahi kuona kitu kama hicho, je ni ugonjwa wa inferiority complex!
ReplyDeleteMdau Kim tupo pamoja, hii mada inaonekana ni ndogo lakini ni ya muhimu sana tusipotoshe vizazi. I don't know what happen to Ms,Mr, and Mrs.
ReplyDeleteWana haki ya kujiita "Engineer" fulani au "Advocate" fulani. Maana hata wabunge usipoanza kwa kumwita "Mheshimiwa Mbunge" fulani then utakuwa na kesi ya kujibu. Vivyo hivyo Meya wa mji fulani usipomwita "Mstahiki" au "His Lordship" pia una kesi ya kujibu. Na pia usipoanza kwa "Baba Mchungaji", "Baba Askofu", "Mtakatifu Papa", "Maalimu" "Shehe fulani" n.k..... pia unaonekana wewe una dhambi. Kwa mlokole usimwita "Mpendwa" pia unaonekana una pepo. Na wengine wengi tu. Basi watu waitwe kwa jinsi wanavyopenda wao. Tuwape uhuru na maadamu hakuna chochote kinachopungua kuwaita au kutowaita kwa titles ambazo ni halali au sio halali basi sioni tatizo lolote.
ReplyDeleteNawasilisha hoja.
Mdauz
Ndugu yangu Kim umeleta hoja ya maana. Tanzania mizaha imedizi. Siku hizi vigumeu kujua nani ana title ya kweli.
ReplyDeleteMganga wa kienyeji 'profesa' au 'dokta'. Unatinga online mwaka mmoja unaibuka na PhD unakuwa 'dokta'. Nasikia watangazi wa redio nao siku baadhi yao ni 'maprofesa'.
Hizo titles za engineers kabla ya jina is a joke!
NBAA na jumuia zingine za kitaaluma nao karibu watalazimisha upuuzi kama huo. Muda si mrefu utaanza kusikia watu wakitajwa kama surveyor mkama, geologist mkama, accountant mkama, sociologist mkama, historian mkama, teacher mkama na wengine wengi. What a mess???
Kuna rais mmoja wa Zanzibar aliwahi kujiita "komandoo". Pia kumekuwa na wimbi kubwa la waandishi wetu wa habari kujiita wapiganaji.Titles hizi zinatishia watoto. watoto wetu wataanza kuwakimbia,shauri zenu. kuhusu engineer Manyanya nafikiri angetengeneza japo sindano ya kushonea nguo ili vizazi vijavyo vijifunze kutokana na kazi ya elimu yake.Watanzania wengi tunapenda sana "eagle".Tujifunze kutoka kwa wenzetu kuwa humble kama wenzetu watatu wasiokuwa na title waliopo kwenye international space station hivi sasa ili dunia iweze kuwasiliana kwa simu na internet ambao majina yao hayaanzii na austonaut Matilda wala austronaut alex.Isipokuwa wanaitwa Matilda na Alex( huo ni mfano tu).Sasa angekuwa mtanzania katoka nje ya dunia nafikiri angeitwa Engineer-cum-austonout/circumnavigator aka the highest speed traveller Dr.Mwakipesile the Great/untouchable.Kupata elimu ni kitu kizuri maana elimu inatupa confidence ya kubadili maisha katika jamii zetu na ukitaka jamii ikujue kama umeenda shule tumia elimu yako kimatendo ili ulete mabadiliko na watu wajifunze kutoka kwako.
ReplyDeleteMimi nilijua mtu ukiwa na Degree ya Pili (Masters) kwenye taaluma fulani ndio unaweza kutumia jina la taaluma hiyo. Kama Engineer, Teacher Lawyer etc.
ReplyDeleteMdau,
ReplyDeleteKwa hili nadhani hata mimi nahitaji kuelimishwa.
Hoja yako ina maana miaka yote tulivyokuwa tunamuita Mwalimu J. K. Nyerere kumbe tulikuwa tunafanya makosa!! Au?
Tuelimishane wadau, tusiendelee kutia aibu!
Soames,
Reading, UK.
Watu wanapenda profession zao bwana, usiwaonee kijicho. Pia unaweza kuwaomba wakutambue kama 'Mbeba box' KIM, haina noma!
ReplyDeleteHuu ni urimbukeni wa watu wachache kujitafutia umaarufu kwa njia ya taaluma haswa wabunge na mawaziri ili wajitofautishe na watu wengi wapate kujijengea heshima na umashuhuri kiasi cha kwamba imesababisha watanzania tuwe na Phd au doctorate fake kama za Mawaziri wafuatao Mary Nagu,Deoratius Kamala,Emmanuel Nchimbi,Makongoro Mahanga na mbunge Raphael Chegeni
ReplyDeletePOSITION STATEMENT
ReplyDeleteUSE OF THE TITLE “ENGINEER”
Adopted by the IEEE-USA
Board of Directors, 17 Nov. 2006
IEEE-USA recognizes that the title, “Engineer,” has a multiplicity of meanings within the
context of laws of various U.S. jurisdictions. All jurisdictions protect the titles “Professional
Engineer”, “Licensed Engineer,” “Registered Engineer,” or some variation thereof, to refer to
individuals licensed in those jurisdictions to practice engineering. In addition, some jurisdictions
protect the title, “Engineer,” with no qualifying words added. The purpose of protecting these
titles is to ensure that the public can easily identify those individuals who possess the requisite
skill, knowledge and competence to protect public safety, health and welfare in the practice of
engineering. Generally, the public interprets the term, “Engineer,” to mean a person who is
qualified to practice engineering by reason of special knowledge and use of the mathematical,
physical and engineering sciences, and the principles and methods of engineering analysis and
design, acquired by engineering education and engineering experience.
It is our position that the title, “Engineer,” and its derivatives should be reserved for those
individuals whose education and experience qualify them to practice in a manner that protects
public safety and advances the health and prosperity of the public. Strict use of the title serves
the interest of both the IEEE-USA and the public by providing a recognized designation by
which those qualified to practice engineering may be identified. Such qualification is evidenced
by graduation with an engineering degree from an ABET/EAC accredited program of
engineering education (or equivalent*) and adherence to an applicable code of ethics in any
jurisdiction, and/or licensure as a Professional Engineer.
• Ing. in Ghana (for engineers holding a B.Sc. or higher with relevant engineering experience) and a registered member of the Ghana Institute of Engineers (GhIE)
ReplyDelete• Pr.Eng. or PrEng is used as a post-nominal in South Africa (for engineers holding a B.Eng., B.Sc. or B.Sc.Eng. with relevant experience). Pr.Tech.Eng. is used as a post-nominal in South Africa (for engineers holding a B.Tech. with relevant experience and three years of practicing in the engineering field)"Pr.Tech.Eng" standing for Professional Engineering Technologist; see Engineering Council of South Africa.
• R.Eng standing for Registered Engineer in Kenya (Holders of Four years post-secondary Engineering Education and four years of work experience)
• Eng. is used for engineers holding B. Eng (5 years degree) in Egypt and must be a member in the Egyptian Syndicate of Engineers.
• Engr is used as a pre-nominal in Nigeria (for holders of bachelor or higher degree in engineering with relevant experience and having successfully passed the Nigerian Society of Engineers (NSE) Professional Exams and fulfill other NSE and Council For Regulation of Engineering in Nigeria(COREN)requirements)" Please refer to http://www.corenng.org/ for more information.
• R.Eng or CEng is used as post-nominal for registered engineers in Nigeria after fulfilling both NSE and COREN requirements.Please refer to http://www.corenng.org/ for more information.
• Eng is used as a pre-nominal in Uganda for registered engineers. In Uganda, a registered Engineer must as a prerequisite be a member of the Uganda Institution of professional Engineers (UIPE) and must have a B.Sc. or higher in Engineering together with relevant engineering experience which must be documented, supported by 2-registered engineers and defended by the applicant in an interview with the Engineers' Registration Board (ERB) which has the power to confirm one as a Registered Engineer. Annual fees must be paid to the ERB by all registered engineers.The following links may provide more information on Uganda's engineering profession. UIPE: http://www.ugandaengineers.org/; UACE: http://www.uace.or.ug/
• Eur Ing, (EUR ING) (European Engineer) in Europe, used as a pre-nominal (similar to Dr. or Prof).
ReplyDelete• Ing.P.Eur (European Professional Engineer) in Europe, used as a pre-nominal
• Ing. (Ingeniero) in Spain, used as a pre-nominal, for the engineers who have the equivalent to a master's degree as they studied five or six courses in a Engineering Superior School. Also exists the Ingeniero Técnico (I.T.), who is a professional that holds a Degree and a minimum formation of three courses in an engineering official college. Both types of engineers have full competency in their respective professional field of engineering, being the difference that the three year Engineers have competence only in their speciality (Mechanical, Electrical, Chemical, etc.)and the "Engineering Superior School" Engineers have wider competences. The Bologna process will change this structure into a different one. The Degree will need four courses and the Superior Engineering School Engineers wil be equaled to the ones that hold a Master in Engineering.
• Eng. (Engenheiro) in Portugal, used as a pre-nominal. An Engenheiro is a full chartered professional in engineering who was awarded a masters' degree (2nd study cycle according to the Bologna process system) by an accredited engineering school. In Portugal there is also the Engenheiro Técnico who is a professional with a bachelor's degree (1st study cycle) in engineering or engineering sciences. Accredited masters' degrees in engineering are regulated and certified by the Ordem dos Engenheiros (Order of Engineers), and every professional full chartered engineer is registered at the Ordem.
• In Germany the Dipl.-Ing. (Diplom-Ingenieur, Diploma Engineer) is awarded by the educational ministries of the federal states (the Länder) after having completing an academic engineering education according to the German Engineer's Law (Ingenieurgesetz). The degrees Ing. grad. (Graduierter Ingenieur, Graduate Engineer) and Obering. (Oberingenieur, Supervisor Engineer) are not awarded any more. (pre-nominal letters)
• Ing. EurEta - used as a pre-nominal (similar to Dr. or Prof). An engineer registered with EurEta "European Higher Engineering and Technical Professionals Association" is called an "EurEta Registered Engineer", and has the right to use this title in Europe, [www.eureta.org/html/startframe.htm] .
ReplyDelete• State-certified Engineer BVT. These titles are the respective translations, authorised by the German Federal Government, of "Staatlich geprüfter Techniker", in Europe.[12]
• Ir. in the Netherlands (for engineers holding a Master's degree from a university) or Ing. (for engineers holding a Bachelor's degree from a professional school). (pre-nominal letters)
• Ir. in Belgium (for engineers holding a Master's degree in engineering/bio-engineering sciences from a university) or Ing. (for engineers holding a Master's degree in applied engineering from other institutes of higher education). (pre-nominal letters)
• Ing. in Italy (for engineers holding a Master's degree) or Ing.jr (Bachelor's) or Periti Industriali (from institutes of secondary education). A state exam is required. (pre-nominal letters)
• Siv. Ing. (Sivilingeniør, M.Sc) and ing. (Høyskoleingeniør, B.Sc) in Norway. The titled is used by persons holding degrees from accredited engineering colleges and universities.
• CEng (Chartered Engineer) and IEng (Incorporated Engineer) in the UK & Republic of Ireland. UK and Irish engineers may also carry post-nominal letters specific to their specialist engineering institute, such as MIET (professional engineers and graduate professionals registered with the Institution of Engineering and Technology). In the UK these are recognised as regulated professions.[13]
• Civ. Ing. in Denmark and Sweden (for engineers holding a Master's degree in Engineering, also M.Sc. Eng, master of science in engineering)and Högskoleingenjör in Sweden (for engineers holding a B.Sc degree).
• Ing. in Romania, used as a pre-nominal (similar to Dr. or Prof.).
• Ing. for engineers holding a Master's degree in Czech Republic and Slovak republic, used as a pre-nominal (similar to Dr. or Prof.).
• inż. and mgr inż in Poland, in Poland inż. is the title obtained after 4 years of studies (similar to B.Sc. degree); inżynier who obtain M.Sc. level use mgr inż (magister inżynier). The mgr level can be obtained through post-bachelor education usually 2 years of studies, or through integrated B.Sc/M.Sc. program that usually is 1 year shorter than the non-integrated program. Some (particularly in the USA) mistakenly believe that "mgr inż" is a separate title, while in fact it is two titles one "inż." indicating technical science 4 year education and the "mgr" indicating the advanced eductaion of 2 cycle regardless of how it was obtained. The degree in general includes license to practice, although some regulation may require additional registration to perform specific tasks. (pre-nominal letters)
ReplyDelete• маг. инж. (Mag. Inzh. from Magister (Master) Engineer) in Bulgaria (for engineers holding a Master's (Magister) degree) or инж. (for engineers holding a Bachelor's degree). (pre-nominal letters)
• "Inġ." in Malta (for engineers holding a university degree and at least 3 years of experience)
Sio lazima hadi waanzishe Marekani kutambua hivyo vyeo ndio na sisi tufuate. Na wao pia (Marekani, Ulaya, n.k) sio mbaya mara moja moja wakaiga toka kwetu (Tanzania na Afrika kwa ujumla).
ReplyDeleteVyeo vya watu lazima viheshimike. Watu wamevisotea hivyo vyeo (Titles). Kwa hiyo anayejisikia kujiita Advocate so and so (wengine badala ya kujiita Advocate, they just call themselves - so and so, Esq. - kwani hii ni NOBLE profession - they are the ONLY learned people - you know what I mean? - sasa kwa nini wasijitambulishe kwa umma kuwa wao ni wa somi? - hizo Degree waliziokota? Au walizitoa kwenye 'Mill' ya Yuniversity ya Nanihii ya kule Mologolo?), - anayetaka kujiita Engineer so and so pia Ruksa.
Shida wengine ukiwaita kwa vyeo vyao wanakasirika, sijui kwa nini? Utashangaa unamuita mtu 'wee Messenger njoo uchukue hizi docs upeleke somewhere, au Messenger niletee kitu fulani' anakasirika eti umemtukana kumuita Messenger wakati ndio cheo chake, sasa si a-upgrade tu? Same applies kwa Makatibu Mukhtasi, wengine unawatuma au unawapa kazi wanajishtukia, kisa? Sasa si ndio cheo chenu jamani. Ah' hembu WAKAJIBEBE zao huko!
Nawasilisha.
Ndiyio,
ReplyDeleteMfano Mwalimu Nyerere.
Ebu katafute watu wenye uelewa mpana na wenye exposure ya kutosha wakufafanulie kwanin mtu anaitwa Eng fulan au Architect fulan,usikurupuke tu kupost vitu bila kufanya research ya kutosha...
ReplyDeleteovyoo we umesoma ungwini nin wewe?
Ndio mdau Kim, Nafikiria aidha wabongo wanapenda hiyo tabia ya kujipachika hadhi, cheo au wadhifa ambao hawajafikia kuupata au kupewa. kuna wale Ma-Producer wa Bongo Flava utawasikia wanajiita Sound ''Engineers'' du mie huwa nachoka kweli. kwa mtazamo wangu Engineer sio Title kama Pro. au Dr. kuna anayeitwa Prof.Eng Jonson sasa hiyo ya kwanza ni Title yake kuonyesha ni upeo wa elimu yake na ya pili ni kuonyesha taaluma yake pia kuitwa Engineer sio lele mama ni taaluma ya hali ya juu, na ndio maana kuna Engineer, na pia kuna Technician, pia inategemea ni Engineer katika area ipi? kuna wajenzi, mafundi magari, Electronics nk. inawezekana Watanzania hawaelewi hapo, wanachanganya, au wanajitafutia umaarufu tu wa jambo fulani. ila inaboa.
ReplyDeleteMdau Ughaibuni
Alamsiki
hata mi sijawahi sikia title kama hiyo, mwenye elimu ya juu jamani atujuze, ili waTZ tuache huu ushamba ndo maana tupo nyuma kimaendeleo
ReplyDelete"Advocate" nyombi ni jina lake,wewe ulitaka aitweje?
ReplyDeleteMBONA JAPAN NA GERMANY WANATUMIA HIYO TITLE YA "ENG. SOMEBODY.....". UNAVOSEMA NI BONGO TU UNAWAONEA WABONGO WENZAKO. UMEKURUPUKA NDUGU MAANA INAONYESHA HUJAFANYA UTAFITI.
ReplyDeleteWATANZANIA BADO TUKO MBALI MNO.
ReplyDeleteHUMU NDANI WATU WAMEJICHANGANYA ILE MBAYA. WAMEBEBA MAMBO YA WIKIPEDIA WAMEWEKA HUMU BILA HATA KUELEWA.
ENGINEER AU PE AU VYOVYOTE VILE, NI PROFESSIONAL QUALIFICATION AMBAYO MTU ANAWEZA KUWEKA KWENYE JINA, KAMA HIVI, JUMA JOSEPH, PE, AU JUMA JOSEPH, ENG. IWAPO ANAHITAJIKA KUONESHA SIFA HIYO, SIYO KWENYE MAMBO YA PUBLIC.
MFANO MAREKANI UKIWA MUUZA NYUMBA, YAANI REAL ESTATE AGENT, KWENYE BUSINESS CARD YAKO YA BIASHARA HIYO UNAPASWA KUWEKA SIFA ZAKO ZA VYETI ULIVYONAVYO NA USAJILI WAKO. HALI KADHALIKA KWA WATU WENYE CERTIFICATION KAMA ZA MAMBO YA FEDHA AMBAYO HUWA CFA YAANI CHARTERED FINANCIAL ANALYST. PIA MTU MWENYE UHASIBU TANZANIA, KAMA ANAHITAJI KUONESHA SIFA ZAKE, LABDA KWENYE ORODHA MAALUM, ANAWEZA KUWEKA CPA NA WALE WA UINGEREZA WANAWEKA ACCA.
HIZI SIFA HAZIMFANYI MTU KUJIITA ACCOUNTANT MAJI KUMALIJA, AU ENGINEER MASENGE SENGA.
TITLES ANAZOZUNGUMZIA KIM NI ZILE AMBAZO NI LAZIMA UWEKE NA INATAKIWA IWE HIVYO. HUYU JAMAA ALIYETOA MFANO WA UJERUMANI KALEWA MWENYEWE TU. HAKUNA TITLES KAMA HIZO. NA MWINGINE KADAI ETI MAREKANI ZIMEJAA, NI MWONGO, HAKUNA KITU KAMA HIKI. MIMI HUU MWAKA WA NNE MAREKANI, SIJAONA HIYO.
PROFESSIONAL TITLES AMBAZO PIA NI ACADEMIC TITLES ZINAJULIKANA NA NDIZO ZINAZOTAKIWA KUWEKWA HAPO. SI KILA TITLE.
SASA JE, WOTE WENYE UTAALAMU UNAOHITAJI KUSAJILIWA AU WENYE DIGRII ITABIDI WAFANYE HIVYO?
TUMIENI AKILI WABONGO.
WAHANDISI HATUPASWI KUITWA HIVYO, ILA TUNAPOJITAMBULISHA KWENYE MAKONGAMANO YETU, TUNAWEZA KUWEKA HIVYO TENA MBELE YA JINA KUONYESHA KWAMBA TUMESAJILIWA. SI KILA ALIYESOMEA UHANDISI AMESAJILIWA PIA.
ACADEMIC TITLES (KAMA KITANGULIZI CHA JINA) ZINAZOKUBALIKA NI PROFESA WA CHEO SIYO WA MAJUKUMU SHULENI/CHUONI NA PIA DAKTARI WA SHAHADA YA UZAMIVU BASI (UDAKTARI WA FALSAFA).
PROFESSIONAL TITLES (KAMA KITANGULIZI CHA JINA) NI DAKTARI WA BINADAMU (SIYO NA WA WANYAMA) NA HAKUNA NYINYINE YOYOTE INAYOBEBWA NA ELIMU.
BAADA YA HAPO, KUNA HIZI ZA MCHUNGAJI AMA SHEHE AMBAZO ZINATOKANA NA KAZI. PIA YA UBALOZI NAYO IMO HUMO HUMO NA HATA YA MHESHIMIWA MBUNGE NA MTUKUFU RAIS. KUMBUKA HIZI NI ZA KAZI, SIYO ELIMU. (HIZI HUTANGULIA KABLA YA JINA). MNAZIJUA.
KWENYE ZILE ZINAZOKAA MBELE YA JINA, MATHALANI, MWAJUMA SAIDI, RN, YAANI MUUGUZI ALIYESAJILIWA KAMA VILE MAREKANI, INATEGEMEA NA FANI INAVYOLAZIMU. NIMETOA MFANO WA WAUZA NYUMBA, MADALALI. UHANDISI UNAHITAJI HIYO IWAPO TU UNATAKIWA KUONESHA KUWA UMESAJILIWA, MATHALANI KWENYE KUOMBA KAZI ZA MIRADI, N.K.
KWENYE JUMUIYA, KAMA BUNGENI NA KWENYE VYOMBO VYA HABARI HUTAKIWI KUONESHA UPUUZI WA KUITWA ENGINEER AU MHANDISI AU INJINIA. NI USHAMBA TU WA WATU WALIOTOKA BUSHI KUJA KUVAMIA ELIMU DAR NA SASA WANAJIPACHIKA VITUKO.
MIMI NI MHANDISI NA NINAPINGA MAMBO YA KIJNGA KAMA HAYA. MWAKANI NAMALIZIA PHD YANGU YA UHANDISI NA NDIYO NITAANZA KUJITAA DKT AMA KUWEKA KIBWAGIZO PHD BAADA YA JINA LANGU. HIYO SINA LAWAMA NA MTU.
PIA, KUWEKA PHD AU MD MBELE YA JINA INAKUJA BADALA YA MTU KUTANGULIZA DR. NA HII HUTUMIWA MAREKANI ZAIDI LAKINI HAINA MAANA ENGINEER NA SISI TUWEKE KIDOKEZO CHETU. HAKUNA.
HAO WANAOJIITA HIVYO NI USHAMBA NA INFERIORITY TU.
HAKUNA TITLE YA ENGINEER IWE KWENYE ACADEMIA AY KWENYE PROFESSIONS HATA KAMA UMESAJILIWA KILA NCHI.
KIM UNA AKILI SANA WEWE. UMESAIDIA.
BAADHI YENU MMESEMA VYEMA. LAKINI WENGI MNAHITAJI DARASA HADI MTOA MAADA MWENYEWE. INAVYO ONEKANA MTOA MAADA HUNA TAALUMA YOYOTE YA SAYANSI NA HUJAJUA BADO KWANI UNAFIKIRIA WATU WANAJIMEGEA TUU NA KUJIPACHIKA VYEO.
ReplyDeleteTANZANIA HUWEZI KUTUMIA HILO JINA KAMA HUJAPEWA KIBALI NA MAMLAKA HUSIKA NA SIO KWA SABABU UMEMALIZA DEGREE YAKO PALE MLIMANI.
NI HESHIMA NA KITAMBULISHO PROFFESIONAL PENGINE ZAIDI YA KUITWA DOCTOR AU PROFESSOR.
UNATAKIWA KUJUA VILE VILE KUWA VITU HIVI SIO UNIVERSAL TITLES KWANI ZIPO NCHI AMBAZO HATA KAMA UNA PHD HUTAITWA DR KIM BALI UTAITWA MR (MFANO NI UFARANSA). ANAYE ITWA DR NI MGANGA TUU WA HOSPITALI.
KWA HIYO KWA TANZANIA HADI UFIKIE KUTWA ENGINEER KIM NI SAFARI NDEFU HATA KAMA YOU HAVE A VERY GOOD ENGINEERING DEGREE FROM A REPUTABLE INSTITUTION.
KWA MAELEZO ZAIDI WAONE ENGINEERS BORD OF REGISTRATION (TANZANIA).
Mdau amekaa akatafakari atajenga vipi nchi yake akaona awashambulie wahandisi kwa kujitambulisha kwa fani yao. Tena basi akaona kwamba ni sahihi kwa madaktari wanaotutibu kujitambulisha kama madaktari ila mhandisi akijiita mhandisi ni kosa kubwa sana la kujikweza. Hii hali ni ya kawaida sana nchini mwetu. Mhandisi anadharaulika. Maji yakikatika mwanasiasa lazima amfokee mhandisi wa Dawasco ili aonekane amefanya kazi.
ReplyDeleteSikia mdau. Tanzania sio nchi pekee ambayo mhandisi anajitambulisha kwa fani yake. Hata Wadachi wanafanya hivyo. Vilevile nchi nyingine kutofanya kitu haina maana kwamba sisi tusikifanye, inabidi tujiangalie kwa nafasi yetu. Suala la wahasibu kutojitambulisha kwa fani yao nchini mwetu ni la wahasibu lakini wakiamua kujitambulisha kwa fani yao hapatakuwa na kosa lolote.
Mdau ungenigusa ungehoji suala la wabunge kuitwa waheshimiwa maana nchi yetu tunasema inajengwa kwa misingi ya ujamaa na usawa kwa hiyo kila mtu ni mheshimiwa. Sifa ya ubunge ni kujua tu kusoma na kuandika.
Mdau ungeweza pia kuzungumzia suala la madokta feki wanaonunua shahada za uzamivu mtandaoni. Wapo serikalini, tena ni mawaziri.
Lakini pia kuna kaushamba fulani hapo.Nimesoma Finland kwenye polytechnic(University of applied siences), na hawa jamaa wameendelea sana tu kati ya nchi za Ulaya.Pale chuoni nilikaa kwa miaka 4 na sikuwahi kujua walimu wangu wamesoma kwa kiasi gani, yaani hizo degrees zao maana kule tunawaita kwa majina yao, tena ya kwanza kama watoto wetu vile!!
ReplyDeleteA Professional Engineer, Engineer is an engineer who is registered or licensed within certain jurisdictions to offer professional services directly to the public.
ReplyDeletenaona wooote mumemsahau DR.REMMY ONGALA!
ReplyDeletewewe hapo juu unaye sema unasoma engineering phd marekani naona na wee unachemsha. Unataka kuona wewe ndooo unajua kuliko wengine an unafikiri wanajua wapo tuu huko marekani. taratibu mkubwa. Sheria ya nchi ndoo inaruhusu watu kuitwa engineer Twihesage na sio ulimbukeni. Ni heshima ambayo engineers wamepewa na registration bord of engineers ambayo ipitishwa na Bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hizo title Dr, Prof sio kila mahali zinatumika. Angalieni msitutie aibu huko nje.
ReplyDeleteMdau umechelewa kuleta hiyo mada lakini nimegundua kuwa umepata changamoto ya kuwa kwanini na wewe usianze kuitwa kwa post nominal yako, Engineers tunaheshimika ndiyo maana tunaitwa hivyo.Nenda kwenywe mkutano wowote wakati watu wanajitambulisha ukisikia mtu akijimbulisha Eng somebody watu wote walioko mbele lazima waangalie nyuma ili wafahamu kumbe tupo na Engineers hapa. Shule yake ngumu ndiyo maana wewe hujafanikiwa kuisoma. Nenda jaribu uione cha moto. acha kutuonea wivu kaka FOE ilitutesa.
ReplyDeletemimi sioni shida, acha mtu aitwe kwa Title yake, mfano: Ankal Michuzi
ReplyDeletehii ndiyo bongo Dar es salaam tumeanza kutoka kivyetu na wale wanaojiita computer vipi!!!!
ReplyDeleteKwa upuuzi kama huu, natamani sana adhabu ya viboko irudishwe mpaka maofisini.
ReplyDeleteLabda na wewe tungejua taaluma yako!!! ni sawa kabisa mtu kuitwa Eng. Fulani kwa sababu hiyo ni proffessional na uenzi kupewa bila kufanya practice hata usome kiasi gani. TATIZO TANZANIA BADO MAMBO HAYA NI MAGENI, KUNA TITLE NYINGI AMBAZO HAJUI KAMA VILE QS MOSHA, ARCH PETER NA KADHALIKA please rudi kafanye utafiti tena
ReplyDeleteSina matatizo na mtu kuitwa title yake ya elimi ilimradi umesajiliwa na bodi husika, vyovyote vile ni sawa lakini kwa Tanzania watu wanatuymia hizo title kwasababu watu kutafuta utambulisho kwenye jumuia wanayoishi, lakini siyo hivyo Uk, kwani uwezi ukawa kwenye taasisi za elimu kama University ukamuita mwalimu Dr mala nyingi hawa jamaa hawataki wanapendwa kuitwa majina yao kama Andy parker, hii ni kwasababu ni wengi muno watu na PhD, na taaluma nyingine, ila kama anaandika barua ni lazima ajitambulishe na title zake mwisho wa majina yake, mchangiaji mmoja amesema ni surveyor nao wataanza kujiita hivyo, ni kweli surveyor wanajiita lakini lazima huwe tayari umefuzu kuitwa hivyo sio digrii tu, lazima uwe awarded na RICS, BAADA YA MITIHANI YAO TITLE YAKO ITAKUWA NI MRICS, hapa huyu unajua ni survryor, hakuna matatizo mtu kuitwa kwa title yake tatizo linakuja watu wanavyojipa digrii ambazo hawana.
ReplyDeleteHivyo jamaa aliyeanzisha mada ni nzuri na haina madhara kwa pande zote mbili kwani mara nyingi tukiwa kwenye mikutano introduction yangu ni jina langu na mimi ni MRICS, HIVYO WATAJUA KUWA HUYU NI CHARTERD SURVEYOR.
Mdau
Wazee wa ma-structures wamejichanganya.
ReplyDeleteKuna rafiki yangu mmoja nikimuita bila kutanguliza neno engineer jamaa anaviiimba.
Kazi kweli kweli.
Mzee Kim najua tatizo unataka kutafsiri vitu kwa kutumia elim ya ngumbaru std 4 chini ya mwembe..kiasi kwamba kama itatoke kuna mvua au kimbunga basi shule/ inapata likizo ya dharura....titles kama mwalim,engineer n.k ni za kawaida na sio kweli kama ni bongo pekee tunaotumia title hizo...tatizo unapata habari toka TBC na magazeti ya CCM ndo maana unakurupuka...unafaham kama muasisi wa taifa letu aliitwa Mwalim JK Nyerere? au unadhani title ya mwalim anapewa rais au waziri mkuu?kama hunasifa za kushika chaki huwezi itwa mwalim..
ReplyDeleteWe unata watu waliopewa kibali cha ithibati ya ERB( Engineering Registratin Board) Tuwaite wauza kahawa au KIM?
Ukiona wakati mwingine huna mada ya akili basi usitake kupotosha watu.
NGWINI keleleeeeee!!!!!!!!
ReplyDeletesioni tatizo lolote mkuu,acha wivu wako inaoneka huna title yeyote kwa hiyo inakuuma nenda kajinyonge au kanywe sumu au rudi shule nawe upate title,daima Engineer kamau
ReplyDeleteMimi sioni tatizo lolote la Engineers kuwa na hizo titles. Kama wadau wengine walivyosema, hizo ni Academic titles na watu wa Ujerumani, Austria na nchi nyingine za Ulaya wanatumia, mfano Dipl.Ing. John au Ing. John. Lakini sio lazima kutumia hizo titles, ni uamuzi wako tu. Lakini wanaweza kutumia hizo titles kama wakitaka. Please do more research kabla ya kuanza kusema “ Hakuna mahala popote duniani ambapo Engineer au Mhandisi ni title kasoro Tanzania“
ReplyDeleteSasa kama watanzania wanataka kutumia hizo titles, tatizo ni nini? As long as wako within the regulations. Cha muhimu ni kuangalia regulations za titles in Tanzania na kufuata hizo. Kama zinasema Engineer wanaweza kuweka Academic title Eng. John au John, Eng, basi hizo ndio regulations inabidi engineers wa Tanzania wafuate.
Lakini tukianza kusema kufuata nchi nyingine, hii ndio inakuwa kasumba isiyo ya maana. Tuwe proud watanzania jamani. Kama engineers wetu wanataka kutumia titles, and under Tanzania regulations they can do that, tatizo ni nini? Mambo ya kuiga na kusema ooh wamarekani hawafanyi hivi au wajerumani wanafanya vile. Cha kujiuliza ni kufuata sheria na kanuni za Tanzania kuhusu hizi titles. Sasa hata daktari akishamaliza chuo anaweka title Dr. hata kama ameshaanza kutibu au bado. Kwahiyo kuanza kusema sijui hao engineers wame-accomplish nini hiyo ni juu yao.
I have been doing my job in UK for eleven years now and it is a common and official practice for professionals to be called putting their titles before. By the way I am a Computer Analyst and I have worked with many engineers in BP. Hata ulaya unakosema wanajiita engineers na lazima aoneshe title ili kujua wajibu wake. Nadhani unahitaji kwenda mahala pengi pa kazi za kuhandisi utajua kwanini inakua ivo. Kama mtu kaenda shule akijitambulisha lazima aoneshe ana ufahamu gani. Ni sahihi, na si lazima ianzie Ulaya. Wazungu wenyewe wanapenda kuitwa eng fulani. Wewe umesoma nini?
ReplyDelete