


Utafiti ulioongozwa na timu toka Chuo Kikuu cha Ohio wavumbua masalia yasiyo ya kawaida ya kiumbe aliyeishi katika kipindi cha Creataceous
Katika toleo la wiki hii la Jarida la Nature wanasayansi ya Paleontolojia wanaatarifu; ugunduzi wa mifupa ya aina ya mamba wafananao na mammalia walioishi hapo kale toka katika Bonde la Rukwa lililomo katika Bonde la Ufa nchini Tanzania.
Aina hiyo ya kiumbe inaleta taswira mpya ya aina ya maisha inayosadikiwa wanyama waliyaishi zaidi ya miaka milioni 100 iliyopita.
“Kwa kutazama meno tu, ni vigumu kutambua moja kwa moja kuwa masalia haya ni ya mamba. Ungestaajabishwa mno na aina hiyo ya mammalia au tuseme mammalia afananae na reptalia,” ameeleza mtafiti kiongozi Patrick O’Connor, Mhaziri Mwandamizi wa mifupa wa Chuo Kikuu cha Ohio – Idara ya Tiba za Mifupa.
Wanasayansi hao wanamwelezea kiumbe huyo mpya kujulikana ajulikanaye kama notosuchian crocodyliform kuwa ni mdogo kwa umbo – “kichwa chake kinaenea katika kiganja cha mkono wako,” alielezea O’Connor.
O’connor na kundi lake la watafiti toka mataifa mbalimbali, wakifadhiliwa na, U.S. National Science Foundation na the National Geographic Society, mwaka 2008 walifanikiwa kuvumbua fuvu kamili la aina ya mamba na mpaka sasa wameshafanikiwa kufukua yapata sehemu saba za aina nyingine tofauti tofauti za jamii zingine za mamba toka nyanda hizi za juu za Tanzania.
Awali, aina ya meno ya kusaga chakula ya mamba hawa yalipovumbuliwa yaliwachanganya watafiti wengi. Kwa kawaida aina nyinginezo za mamba kama hawa wa kale huwa na meno ya kusagia yaliyochongoka, wanayotumia kukamata na kurarua mawindo; kisha humeza mapande makubwa bila kusaga. Hii ni tofauti na aina hii mpya ya mamba waliovumbuliwa katika tafiti hizi.
Meno ya kusagia ya jamii hii ya mamba, aitwaye Pakasuchus (Paka ni kwa kumfananisha na paka na souchos ni kiyunani kikimaanisha mamba), yana ncha za kulegeza na kulainisha chakula, kama ilivyo kwa mamalia wala nyama.
Meno ya kusagia ya jamii hii ya mamba, aitwaye Pakasuchus (Paka ni kwa kumfananisha na paka na souchos ni kiyunani kikimaanisha mamba), yana ncha za kulegeza na kulainisha chakula, kama ilivyo kwa mamalia wala nyama.
“Baada ya uchunguzi wa kina wa aina ya meno ya mamba hao, tukatambua tumevumbua aina ya kipekee na ya kufurahisha ya mamba”, alisema O’connor.
Uvumbuzi huu wa timu hii ya watafiti juu ya wanyama waliokuwa na magamba mazito mkiani huku ingali sehemu ya mwili iliyobaki ikiwa na bila ya magamba mengi na miguu ya kipole ikiashiria utembezi wao. Pia walikuwa wakitumia viganja kushikia kinyume kabisa na mamba waishio majini.
Aina hii mpya ya viumbe iliyogunduliwa si ya kufanana zaidi na aina ya mamba tuwaonao leo hii, ila inasadikika kuwa katika kundi la aina ya mamba waliofanikiwa sana katika kipindi hicho cha Mesozoic, alisema O’Connor.
Japo kwa ssa na muonekano wa aina hiyo ya wanyama inaonekana ya kushangaza, utafiti umeonyesha kuwa viumbe hao walikuwa wengi na wa kawaida mno kipindi hicho cha katikati ya Cretaceous – kati ya miaka milioni 110 na 80 iliyopita.
Japo kwa ssa na muonekano wa aina hiyo ya wanyama inaonekana ya kushangaza, utafiti umeonyesha kuwa viumbe hao walikuwa wengi na wa kawaida mno kipindi hicho cha katikati ya Cretaceous – kati ya miaka milioni 110 na 80 iliyopita.
“Kadiri tunavyofanya utafiti na kudundua aina mbalimbali za viumbe wa kale ndivyo uelewa wetu wa sayari yetu na viumbe wake walioishi nyakati hizo tunavyozidi kuzitambua” aligusia O’Connor.
Kwa mujibu wa masalia mengine ya viumbe waliopatikana katika Mradi wa Utafiti wa Bonde la Ufa la Rukwa (Rukwa Rift Basin Project), Pakasuchus aliishi pamoja na Saurop wakubwa wala mimea na theropod dinoso wala wnyama, aina nyingine za mamba, kobe na aina mbalimbali za samaki.
“Tunasadiki kwa mujibu wa tafiti notosuchiani walikuwa wenye mafanikio makubwa kusini mwa Ikweta kwa kuwa kiikolojia walishika maeneo maalumu, mojawapo ikiwa ni mle walimoweza kushindana na viumbe wengine wadogo kwa mwili waishio nchi kavu,” alisema O’Connor. “Na haya ndiyo mazingira ambayo yalikuwa ya aina yake mno ukilinganisha na tuliyoyazoea.”
Kuhusu mimea iliyokuwepo kipindi hichi si mengi yanafahamika, ila kwa mujibu wa utafiti wa kina wa kisedimentolojia wa bonde la ufa la Rukwa unaonyesha kuwa “bonde lilitawaliwa na mito mikubwa ya kudumu, na mabonde yenye kutakatana kwenye nyanda za chini iliyojaa mimea na kwa aina kutawaliwa na wanyama wenye uti wa mgongo,” alisema Eric Roberts, Mhadhiri Msaidizi wa Jiolojia toka Chuo Kikuu cha James Cook ambaye ni moja ya washiriki wakuu wa utafiti huu wakati akiwa katika Chuo Kikuu cha Southern Utah.
Katika kipindi cha Cretaceous, maeneo yafuatayo Afro-Arabia, along with India, Madagascar, Antarctica, Australia na Amerika ya Kusini, yalikuwa bado yameunagana yakiunda bara kubwa la kusini lililojulikana kama Gondwana. Kwa ujumla ni mamalia wachache sana waliovumbuliwa toka maeneo haya ya dunia na wachache waliopatikana wanamuonekano tofauti sana na wale wa leo hii. Aina ya mamba wajulikanao kama Notosuchiani yawezekana waliwazibiti kushamiri na kushika ,maeneo ya mamalia kipindi cha Cretaceous huko Gondwana.
“Moja ya sababu zinazopelekea tufanye kazi kusini mwa Ikweta, ikiwemo Afrika na Antarctica, ni uhaba wa tafiti zilizofanyika tayari katika maeneo haya. Hivyo bado tunaendelea kutafiti kutegua kitendawili cha jinsi gani maisha ya wanyama yalivyokuwa sehemu hizo,” anaeleza O’Connor. "Huenda ni kwamba bado hatujampata aina halisi ya mammalia."
Washiriki wakuu wa utafiti ni pamoja na: Nancy Stevens and Ryan Ridgely wa Chuo Kikuu cha Ohio - Marekani; Joseph Sertich wa Chuo Kikuu cha Stony Brook - Marekani; Eric Roberts wa Chuo Kikuu cha James Cook - Australia; Michael Gottfried wa Chuo Kikuu cha Michigan State - Marekani; Tobin Hieronymus wa Idara ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Northeastern Ohio - Marekani; Zubair Jinnah wa Chuo Kikuu cha Witwatersrand - Afrika ya Kusini; Sifa Ngasala wa Chuo Kikuu cha Michigan State University - Marekani and Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Tanzania; na Jesuit Temba Idara ya Mambo ya Kale ya Tanzanian.
Kwa maelezo zaidi juu ya mradi huu wa utafiti, tembelea tovuti hii: http://www.oucom.ohiou.edu/rukwa/index.htm
NA HII INAONYESHA KABISA HAPA BONGO NDIO MWANZO WA KILA KITU, BINADAMU WA KWANZA KATOKEA HAPA BONGO, LAKINI LEO HII??? NDIO WA KWANZA KUFA!!! LOO SALALA SIJUI WATU WATAAMKA LINI!
ReplyDeleteHongera Arkiologist Temba kwa kushiriki utafiti huo.
ReplyDeleteNi mimi Jiografa Subby pamoja na Akauntant Derby, ukisalimiwa na Injinia Njau
(mambo ya taito hayo, mjini mtatukoma)
Ile fulana ya green vesti ya kijani ya wanafunzi wa chuo kikuu cha university of Dar-es-Salaam iliyopitia operation Mlale ya JKT ipo wapi?
ReplyDeleteBADO NAJIULIZA SANA NN HATIMA YA TAFITI KM HIZI AMBAZO ZINAISHIA KUTANGAZA TU MAJINA YA WAHUSIKA NA SI AJABU KESHO TUTASIKIA WAMEPEANA MA-PHD NA HESHIMA ZINGINE KM HIZO WKT KAZI HIZO NATHUBUTU KUSEMA HAZINA FAIDA YOYOTE KWA MWANANCHI WA KAWAIDA LICHA YA KWAMBA ZINATUMIA GHARAMA NYINGI SN.
ReplyDeletematokeo ya tafiti hii na nyinginezo yanatakiwa kutoa majibu ya matatizo ya msingi ya njaa, umaskini, vita, maradhi yaliyotawala hasa nchi za dunia ya tatu vinginevo tafiti hizo zitakuwa ni nyimbo tena zisizo na wachezaji.
ReplyDeleteHalafu huko Mbozi kuna masalia kibao ya dinosaurs ambapo inasemekana watafiti huja kila mwaka na kuondoka na mifupa........jamani tunaibiwa!!!
ReplyDeletemdau hapo juu,,,tuibiwe kwani mara ngapi?mbona tushaibiwa saaana tu!!
ReplyDeleteyani kuna dino walishwamwibaga vipande weee adi kakamilika yuko ujeremani kule...
na bado lazima wapeane maPHD ndio si pesa yao na sie wala hatuoni umaana wa kuhifadhi hivi vitu?eti tuna makumbusho sijui uchafu gani..
kumejaa makaratasi tu na vipicha vya ukoloni ndo tulijualo
nyambaf sana uyu waziri husika
annon #2 toka juu
ReplyDeletemna pesa ya uhakika si ya kubabaisha au izo taito ukafukuzwa ofc nyie?investment gani?
tulia kijana life sio titlez izo
sioni jipya hapo zaidi ya mambo ya wazungu kujichukulia ujiko tu...ona walivopanga majina yao......af..na hao waswahili wenzetu nao vichwa hivyoo wanachekelea...kaaaaaaazz kwelikweli!!!nyie waswahili akili mukichwa
ReplyDeleteMimi ni Ahmed Mussa,(Geologist) nilishiriki katika ugunduzi huo kama field work june-july 2008.hiyo picha ya kati si kweli ni mimi Ahmed Mussa na Gabriel Masai (iweje Gabriel awe mwanamama?).Hao ni walikuwa field huko mwaka 2007....anyway for more information & pictures of dinosaurs bones, just email me: meddykambonjr@yahoo.com
ReplyDelete